Jaji Warioba ambana Jussa kuhusu Muungano wa mkataba | JamiiForums | The Home of Great Thinkers

Dismiss Notice
You are browsing this site as a guest. It takes 2 minutes to CREATE AN ACCOUNT and less than 1 minute to LOGIN

Jaji Warioba ambana Jussa kuhusu Muungano wa mkataba

Discussion in 'Jukwaa la Siasa' started by mtwana, Oct 15, 2012.

 1. mtwana

  mtwana JF-Expert Member

  #1
  Oct 15, 2012
  Joined: Oct 13, 2012
  Messages: 399
  Likes Received: 85
  Trophy Points: 45
  Mwenyekiti wa Tume ya Mabadiliko ya Katiba Jaji Joseph Warioba amembana Mwakilishi wa Jimbo la Mji Mkongwe Mkongwe (Cuf), Ismail Jussa aeleze kuhusu mfumo wa uendeshaji wa Muungano wa mkataba unavyopaswa kuwa na mgawanyo wake wa madaraka .

  Jaji Warioba alichukua hatua hiyo baada ya Jussa kusimama na kutoa maoni ya kutaka mfumo wa Muungano wa mkataba, wakati Tume ya Mabadiliko ya Katiba ilipokuwa ikichukua maoni ya Wawakilishi mjini Zanzibar jana.

  Alimtaka Jussa atoe mfano angalau mmoja au miwili ya uendeshaji wa serikali ya mkataba ili Tume yake ipate ufahamu katika mapendekezo yake.

  Jussa alisema anayo mifano zaidi ya 100 lakini akadai wakati ukifika serikali zinazohusika zitakaa na kuja na fomula ya mgawanyo huo pamoja na uendeshaji wake kimadaraka.

  Hata hivyo, Jaji Warioba kwa upande wake akionekana kutoridhika na maelezo hayo ya Jussa alimtaka kuiambia Tume alivyojiandaa na Muungano wa mkataba kinyume na mfumo dola uliopo.

  “Bwana Mwakilishi hebu tupe lau mfano mmoja au muundo wa uendeshaji wa Muungano wa serikali ya mkataba ili uweze kukidhi haja yako na kutuonyesha njia” alisema Jaji Warioba.

  “Hebu tuweke wazi juu ya utashi wa mpango unaofikirika wa kuwa wa serikali ya mkataba, nafikiri unachokusudia ni kutaka kuvunja Muungano uliopo” alisema Warioba.

  Hata hivyo, Jussa alibaki katika msimamo wake huku akisisitiza kuhusu kukaa kwa serikali mbili na kutoa mfumo wa uendeshaji wa serikali ya mktaba.

  Akifafanua, Jaji Warioba alisema kimsingi kudai Zanzibar iwe na mamlaka kamili, huku Tanganyika nayo ikiwa na mamlaka yake ni sawa na kuvunja muungano kwa kuwa kila upande utalazimika kuwa na kiti Umoja wa Mataifa (UN).

  “Tanganyika na Zanzibar zikiwa kila moja ina mamlaka yake hakutakuwa na neno Muungano, ndiyo maana nasema nisaidiwe juu ya kupata mfumo wa kuendesha Muungano unaotakiwa chini ya mkataba” alisema Jaji Warioba.

  Akiwekea mkazo katika hoja iliyotolewa na Jaji Warioba, mmoja wa Makamishna wa Tume hiyo, Paramagamba Kabudi, alisema inasikitisha kuona hadi sasa wanaotaka Muungano wa mkataba wanashindwa kutoa rasimu ya mfano wa serikali ya mkataba ili kuisaidia Tume juu ya kile wanachokitetea.

  Wakitoa maoni yao mbele ya Tume ya Mabadiliko ya Katiba, wajumbe wa Baraza la Wawakilishi wa CCM na CUF waligawanyika pande mbili huku wale wa CCM wakitetea mfumo wa serikali mbili na wa CUF wakitaka Muungano wa mkataba.

  Waziri wa Ulinzi na Jeshi la Kujenga Taifa Shamsi Vuai Nahodha alisema muundo wa Muungano wa serikali mbili ndiyo muafaka kwa kuwa umeonyesha faida katika masuala ya ulinzi na usalama lakini pia ukijenga umoja wa kitaifa.

  Akishauri Nahodha alisema hata hivyo ni vyema ikafika mahali kukawa na mabunge mawili , moja dogo litakaloshughulikia mambo ya Muungano na jingine lishughulikie mambo ya Tanganyika.

  Aidha alitaka nafasi ya Rais wa Muungano itolewe kwa zamu kila upande uwe na kipindi cha miaka kumi.

  “Mgawanyo wa mapato usiangalie idadi ya watu kwa vile hata kama Serikali moja ikiwa na watu wawili bado ina jukumu la kuwapatia maisha bora na huduma wananchi wake” alisema.

  Naye Waziri wa Habari, Utamaduni, Utalii na Michezo wa Zanzibar Said Ali Mbarouk alisema mfumo wa sasa wa Muungano una matatizo kwakuwa kuna mambo ambayo si ya Muungano lakini yanasimamiwa na Muungano kinyume na makubaliano ya mwaka 1964.

  Aliyataja baadhi ya mambo aliyodai yanayoleta mkanganyiko kuwa ni utalii, maliasili, habari na michezo ambayo alisema yanahitaji kuwekewa utaratibu na kuzungumziwa kwake katika medani za kimatifa.

  Waziri asie na Wizara Maalum Machano Othman Said alitaka mfumo wa Muungano wa sasa uendelee na kutaka Rais wa Zanzibar kubaki kuwa Makamu wa Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania.

  Mwakilishi wa Jimbo la Uzini Mohamed Raza alitaka Rais wa Zanzibar awe na mamlaka sawa na Rais wa Muungano pamoja na Zanzibar kupata nafasi ya kujiunga na jumuiya ya OIC na nyingine za kiuchumi duniani.

  Tume ya mchakato wa ukusanyaji wa maoni inayoongozwa na Jaji Warioba ipo visiwani Zanzibar na tayari imekutana na wananchi katika mikoa ya Kaskazini Unguja na Pemba.

  Hivi kwani isiwezekane na kama tukivuna muungano nyinyi mutadhurika na nini ama tuseme munatupenda sna sisi wazanzibari..Tuwacheni tupumueeeeeeeeeeeeeeeeeeeeeeeeeeeeeeeeeeeeeeeeeeeeeeeeeeeeeeeeeeeeee Laana impate yule ambae asieitakia mema zanzibar yetu looooooooooooooooo
   
 2. Ndahani

  Ndahani JF-Expert Member

  #2
  Oct 15, 2012
  Joined: Jun 3, 2008
  Messages: 14,335
  Likes Received: 1,797
  Trophy Points: 280
  Nahodha anaonekana kujua anafanya nini na sio mroho wa urais wa zanzibar mpya baada ya kuvunja muungano.
   
 3. Ngongo

  Ngongo JF-Expert Member

  #3
  Oct 15, 2012
  Joined: Sep 20, 2008
  Messages: 12,155
  Likes Received: 3,634
  Trophy Points: 280
  Swali la Jaji Warioba kwa Jussa na wajinga wenzake kamwe hawana uwezo wa kulijibu Barubaru ebu wasaidie CUF wamepewa nasi ya kutetea hoja zao wameshindwa mbele ya tume sasa tuwasaidie nini ?.
   
  Last edited by a moderator: Jan 4, 2016
 4. masopakyindi

  masopakyindi JF-Expert Member

  #4
  Oct 15, 2012
  Joined: Jul 5, 2011
  Messages: 13,918
  Likes Received: 2,348
  Trophy Points: 280
  At last Ismael Jussa ameanza kufundishwa somo la Muungano the hard way!

  Katika mchakato wa kukusanya maoni juu ya katina mpya, Mweneyekiti wa Tume ya Mabadiliko ya katiba Jaji Warioba imebidi atoe "tuition" kwa Bwana Jussa, ambaye kwa muda mrefu sasa amekuwa anonelea mifumo ya Muungano isiyo na tija.

  Kulingana na taarifa kutoka gazeti la Nipashe, la leo 15/10/2012 nanukuu:

  " Mwenyekiti wa Tume ya Mabadiliko ya Katinba Jaji Joseph Warioba amembana Mwakilishi wa Jimbo la Mji Mkongwe(CUF) Ismael Jussa aeleze kuhusu mfumo wa uendeshaji wa Muungano wa mkataba unavyopaswa kuwa na mgawanyo wa madaraka"
  Jussa alikuwa ametoa maoni yake mbele ya Tume hiyo akijinadi kwa kutaka muungano wa mkataba.

  Ndipo Jaji Warioba akamtaka atoe mifano ya mikataba kama hiyo inayotumiwa duniani, ambapo mheshiiwa huyu alianza kuweweseka na kudai kuwa ana mifano zaidi ya mia moja.

  Baada ya kutoridhik na maelezo,Jaji Warioba alimbana zaidi na kumweleza kuwa nia ya Mwakilishi huyo hasa ilikuwa kuvunja muungano na si vinginevyo.

  My Take
  Muda wa kubwabwaja inaeleka mwisho kwa Bwana Jussa, he is meeting proffessionals katika field hiyo.
   
 5. W

  WildCard JF-Expert Member

  #5
  Oct 15, 2012
  Joined: Apr 22, 2008
  Messages: 7,477
  Likes Received: 70
  Trophy Points: 145
  KATIBA ya JMT inachezewa na akina Jussa. Walioapa kuilinda wako kimya.
   
 6. Myakubanga

  Myakubanga JF-Expert Member

  #6
  Oct 15, 2012
  Joined: Oct 3, 2011
  Messages: 5,781
  Likes Received: 333
  Trophy Points: 180
  Akili ndogo Vs akili kubwa!
  Jussa ataweza?
   
 7. Fredrick Sanga

  Fredrick Sanga JF-Expert Member

  #7
  Oct 15, 2012
  Joined: Jan 27, 2011
  Messages: 3,148
  Likes Received: 19
  Trophy Points: 135
  Jusa katoa maoni yake, ulitaka akae kimya? Kumnyanyapaa kunatia wasi kama tume ni huru.
   
 8. Democracy999

  Democracy999 JF-Expert Member

  #8
  Oct 15, 2012
  Joined: May 26, 2012
  Messages: 947
  Likes Received: 1
  Trophy Points: 0
  Bora serikali Mota tu
   
 9. Kiranga

  Kiranga JF-Expert Member

  #9
  Oct 15, 2012
  Joined: Jan 29, 2009
  Messages: 34,607
  Likes Received: 6,197
  Trophy Points: 280
  On the one hand, Jussa kusema ana mifano 100 kunatakiwa kumfanye awe na urahisi zaidi wa kutoa mfano hata mmoja.

  Anachokosea Jussa ni kusema ana mifano 100 bila kutoa hata mmoja.

  Angeweza kusema tu "Muungano nnaoutaka haupo duniani, na si lazima kuwa na mfano, kwani hata Muungano wa sasa wa Tanzania wa nchi mbili kuungana na kubaki na serikali mbili, ya muungano na ya nchi moja zilizoungana, haujawa na mfano sehemu nyingine yeyote duniani"
   
 10. Barubaru

  Barubaru JF-Expert Member

  #10
  Oct 15, 2012
  Joined: Apr 6, 2009
  Messages: 7,162
  Likes Received: 30
  Trophy Points: 0
  Hakika JUSSA anawakosesha usingizi waTanganyika na hata kumuona ni mwiba mkuu.

  Hongera sana Jussa hakika wewe ni kichwa.
   
 11. Kiranga

  Kiranga JF-Expert Member

  #11
  Oct 15, 2012
  Joined: Jan 29, 2009
  Messages: 34,607
  Likes Received: 6,197
  Trophy Points: 280
  Barubaru,

  Bado sijaona mtu mwenye mifano 100 na kushindwa kutaja hata mmoja anakosesha watu usingizi kivipi.
   
 12. Ngoromiko

  Ngoromiko JF-Expert Member

  #12
  Oct 15, 2012
  Joined: Sep 15, 2011
  Messages: 559
  Likes Received: 68
  Trophy Points: 45
  "Mgawanyo wa mapato usiangalie idadi ya watu kwa vile hata kama Serikali moja ikiwa na watu wawili bado ina jukumu la kuwapatia maisha bora na huduma wananchi wake" alisema.

  Hii haina mantiki. Anataka kumaanisha kuwa iwapo Bara kuna watu 10, na Zenj watu 2, na iwapo mapato ni vitumbua 12, mgawo uwe ni vitumbua 6 kila upande? kama ikiwa hivyo Zenj si watavimbiwa wakati Bara wakibaki kupiga miayo ya njaa?
   
 13. Watu8

  Watu8 JF-Expert Member

  #13
  Oct 15, 2012
  Joined: Feb 19, 2010
  Messages: 47,347
  Likes Received: 2,683
  Trophy Points: 280
  suala la katiba halipaswi kufanywa kwa ushabiki au matakwa binafsi kwa kuwa matokeo yake hulenga jamii nzima ya Watanzania.
   
 14. simplemind

  simplemind JF-Expert Member

  #14
  Oct 15, 2012
  Joined: Apr 10, 2009
  Messages: 11,813
  Likes Received: 2,584
  Trophy Points: 280
  Mchakato wa uundaji wa katiba lacks legitimacy. Constituion making process must be participatory and all inclusive. Kinachoendelea ni CCM sponsored katiba review process.
   
 15. sembuli

  sembuli JF-Expert Member

  #15
  Oct 15, 2012
  Joined: Feb 3, 2012
  Messages: 762
  Likes Received: 29
  Trophy Points: 45
  haya ndio madhara ya kufanya mambo kwa kuiga, jussa kila kitu anaiga !
   
 16. n

  ngwendu JF-Expert Member

  #16
  Oct 15, 2012
  Joined: Jun 7, 2010
  Messages: 1,967
  Likes Received: 6
  Trophy Points: 0
  wazanzibari changamkeni muda wenyewe ndo huu, daini kila mkitakacho kwenye roho zenu, hatutaki mlalamike tena, kikwete siyo mbishi, ukimjengea hoja atakubali tu, anyway, zubaeni aje rais mwengine mtata muone yatakayowakuta, msije kimbilia shimoni-kenya tena na kuiaibisha nchi kwa mara ya pili. narudia tena, muda ndo huu, hatujui 2015 anaweza kuja rais chizi, msije kujuta.
   
 17. Kiranga

  Kiranga JF-Expert Member

  #17
  Oct 15, 2012
  Joined: Jan 29, 2009
  Messages: 34,607
  Likes Received: 6,197
  Trophy Points: 280
  Granted.

  Lakini hata hiyo CCM sponsored process, once ukishakubali kushiriki, umeshai legitimize.

  Na hapa tunaona muwakilishi wa upinzani -CUF- anajiumauma, anasema anataka muungano wa mkataba, anaulizwa mkataba wa aina gani, ooh nina mifano 100, haya tupe mfano mmoja basi tuusome tujue unamaanisha nini.

  Anajiuma.

  Watu wanaulizwa wanataka katiba ibadilishwe vipi, wanasema mambo ya ajabu huko, mara nchi iwe na muhimili wa dini kama nyongeza ya executive, legislature and judiciary. Watu wanataka katiba iruhusu kuoa wake mitala wakati haki za kikatiba kufanya hivyo zipo tayari.

  Huwezi kuwa na a meaningful constitutional review process kama watu wako hawajui hata kusoma na kuandika kwa viwango vinavyotakiwa.

  Na hapo ndipo CCM inapopata ushindi, mpeleke Warioba aende kusikiliza Waswahili wanaobishana mambo legal kwa unazi.

  Matokeo yake mtu anasema ana mifano 100, anaambiwa taja mmoja, ananywea.

  Ny father is stronger than your father style!
   
 18. Barubaru

  Barubaru JF-Expert Member

  #18
  Oct 15, 2012
  Joined: Apr 6, 2009
  Messages: 7,162
  Likes Received: 30
  Trophy Points: 0
  nafikiri ingekuwa busara sana kuweka mjadala maalum wa wazi ikiwezekana kwenye TV na Radio kati ya JUSSA na Warioba mtajua uwezo mkubwa wa Jussa dhidi ya Warioba.
   
 19. Kiranga

  Kiranga JF-Expert Member

  #19
  Oct 15, 2012
  Joined: Jan 29, 2009
  Messages: 34,607
  Likes Received: 6,197
  Trophy Points: 280
  My father is stronger than your father style, nilishaona hili. Mtoto akipigwa heshi kutishia baba yake ana nguvu zaidi ya baba ya aliyempiga, ni mchezo wa kitoto huu.

  Hatuzungumzii uwezo wa Warioba na Jussa, wote ni watu tu. Great minds discuss ideeas bwana, hatu discuss watu hapa.

  Tunazungumzia fate ya Muungano.

  Mfano mmoja kati ya 100 ya Jussa ni upi?
   
 20. Ndoa

  Ndoa JF-Expert Member

  #20
  Oct 15, 2012
  Joined: Dec 2, 2011
  Messages: 985
  Likes Received: 12
  Trophy Points: 35
  Jusa yuko sawa kutaka zanzibar yake. Ajipange ajenge hoja.
   
Loading...