Kiranga
Platinum Member
- Jan 29, 2009
- 71,284
- 105,516
Kwa kuengezea tu, Bwana Butiku mwisho anasema Jussa umeelewekwa, sasa kama wewe wadhani honest hakuwa wazi, sijuwi kwasababu zipi? Magazeti nayo kupotosha kama alivyotaka mzee arioba kutaka kupotosha kwa kumuambia Jussa kapotosha wakati yeye anafahamu historia ya nchi zetu mbili kila mmoja anasema kivyake. Haina maana nikisema nakuheshimu ndio wewe univunjiye heshima na alimuambia mbele yake kamba tuheshimiane.
Lazima ufahamu kamba mzee warioba muungano huu anaupenda kupindukia na hii ni kutokana na kumuamini sana mwalimu. Lakini tatizo la watanganyika mumekuwa wagumu mno kufahamu kilio chetu wazanzibari. Sisi hata tupate msaada India, basi kupata ile barua tu, utasumbulia weee na mwisho hupewi. Na tena inaweza kua haihusiani kabisa na mambo ya muungano. Sawa mambo ya nje ya muungano basi nikija na dhiki yangu usinibane nibane ikiwa ni kitu cha muungano. mambo ni mengi na yanazidi kuwa mengi.
Mzee Warioba muungano huu anaupenda.
Msioupenda mmefanya nini mpaka sasa kuuvunja? Maana isiwe zogo na malalmishi tu.