Jaji Warioba ambana Jussa kuhusu Muungano wa mkataba

Kwa kuengezea tu, Bwana Butiku mwisho anasema Jussa umeelewekwa, sasa kama wewe wadhani honest hakuwa wazi, sijuwi kwasababu zipi? Magazeti nayo kupotosha kama alivyotaka mzee arioba kutaka kupotosha kwa kumuambia Jussa kapotosha wakati yeye anafahamu historia ya nchi zetu mbili kila mmoja anasema kivyake. Haina maana nikisema nakuheshimu ndio wewe univunjiye heshima na alimuambia mbele yake kamba tuheshimiane.

Lazima ufahamu kamba mzee warioba muungano huu anaupenda kupindukia na hii ni kutokana na kumuamini sana mwalimu. Lakini tatizo la watanganyika mumekuwa wagumu mno kufahamu kilio chetu wazanzibari. Sisi hata tupate msaada India, basi kupata ile barua tu, utasumbulia weee na mwisho hupewi. Na tena inaweza kua haihusiani kabisa na mambo ya muungano. Sawa mambo ya nje ya muungano basi nikija na dhiki yangu usinibane nibane ikiwa ni kitu cha muungano. mambo ni mengi na yanazidi kuwa mengi.

Mzee Warioba muungano huu anaupenda.

Msioupenda mmefanya nini mpaka sasa kuuvunja? Maana isiwe zogo na malalmishi tu.
 
AllyZenj,

..sasa kama hakutakuwa na serikali ya muungano, hili suala la "muungano wa mkataba" linatoka wapi?

..hivi unajua kwamba hata huu muungano tulionao sasa hivi ulitokana na mkataba wa muungano uliosainiwa na Mwalimu Nyerere na Sheikh Karume??

..tuseme tu kwamba tunavunja muungano. atakayeingiwa na hofu tutamueleza kwamba masuala ya uhamiaji, biashara, etc etc yatashughulikiwa kupitia mikataba mbalimbali.

NB:

..halafu kwanini unafikiri watu wataingiwa na HOFU ikiwa muungano utavunjika?? kama muungano ni hasara na mateso kwa wa-Zanzibari kama ambavyo mmekuwa mkihubiri, basi bila shaka wananchi watafurahi wakisikia kwamba viongozi wao wamedhamiria kuuvunja.
 
Last edited by a moderator:
KWani hatukutaka. Ilikuwa miaka nyuma kutamka tu muungano basi ni kosa kama kosa kwa kutilia shaka holocaust dhini ya jews au hujui hilo. Ubabe na nguvu na kuhahalisha ka nguvu ndio tumefika hapa tulipo fika. Kani scotland si hawautaki jeee na wao wauvunje tu si kuna taratibu zake. Nyinyi si munataka katiba mpya si na mufanye tu kama rahisi! Tatizo vichwa vyenu vizito ndio maana munauliza masuala ya kitoto. Hivi Nyerere alikuwa anakenda UK kufanya nini wakati anajua Tanganyika ya watanganyika? Hivi Afrika nzima wakijuwa ni ya kwao kwanini wakakubali kupangiwa siku ya kupewa uhuru kiasi kwamba Nyerere alikua akichelewesha kupewa Tanganyika ili wakipewa wapewe kwa pamoja. Si ilikuwa kazi rahisi kwame, nyerere, kenyata na wengine wakutane na kusema hawa wazungu wataondoka ka nguvu tu!
 
Jokakuu,

Zanzibar haitakuwa kwenye dhiki yoyote na Tanganyika kwa upande wa viongozi wanajuwa hilo.Wanafahamu siku Tanzania itakapo vunjika na Tanganyika ikawa huru, basi nanyi mutakuwa kama Uganda, Nigeria na nchi zilizo kuba na mapinduzi. Kunusuri haya basi bora tubakiye hivi hivi.

Zanzibar wakati inaungana na Tanganyika ilikuwa na kila kitu chake. Ilifanikiwa kufanya yaliyo mazuri ambayo Tanganyika imeyafanya kuanzia 1990 tena baada ya Ali Hassan Mwinyi kuachana na Ujamaa ati leo mwajifanya muna upenda ujamaa. Zanzibar ilifika hata kuisaidia SMT kama hujuwi!

msikilize tena Jussa kwa kituo. Ya Znazibar tuachiyeni sisi wazanzibari kwasasa jiandaeni kwa Tanganyika. Sijui itakuaje wafuasi wa CDM na CCM na akina NCCR na TLP yaani fujo tu. Sisi tushaonesha mfano kwamba tunaweza kufanya kzi pamoja na tuna SUK, nyinyi hata hamuja itafuta. Kasheshe tupu.
 
Na iwe hivyo anataka kuvunja muungano kwani geni hilo? Kwanini wangapi washasema hayo tena huko huko bara? kwanini iwe ni kiroja kwa Jussa? EU wana sovernenity na wana raha zao. maana m-swedish akitamanikwenda kuishi Netherland hakatazwi na atapa mahitajio yake yote kama sheria inavyo sema. Britsih anaeza kwenda kuishi Italy na wala habugudhiwi... sasa hili ndio tunalo taka sisi kama tuwe huru kwa mambo yetu. Mwanzoni wakati tunaungana, Nyerere aliweka passport kwa watanganyika kuja Zanzibar halikadhalika wazanzibari pale wanapotaka kweda bara. Iliondoshwa ilipo onekana hakuna haja...
 
AllyZenj,

..usitoke nje ya mada kuanza kumjadili Nyerere.

..kama umemuelewa Mh.Jussa tueleze kwanini tusivunje muungano na kushirikiana kupitia East African Community.

..kuhusu masuala ya undugu, hata Kenya,Uganda,Msumbiji,Rwanda,Burundi,Malawi,Zambia,DRC, wote hao ni ndugu zetu lakini hatuna muungano nao.

NB:

..sasa hivi wa-Zanzibari mmeanzisha vitambulisho ambapo Mtanganyika atakuwa sawa na Muingereza,Mmarekani, Mkenya, etc etc anapokanyaga ardhi ya Zanzibar. wakati huohuo mnasema mnataka mkataba kama wa EU ambapo suala la makazi ni huria.

..hii hoja ya Jussa siyo ya kuungwa mkono kwa kutoa sauti za NDIYOOO!! Lazima tuuulize maswali ili kuwekana sawa na kuondoa sintofahamu, na hofu za aina yoyote ile.
 
Jokakuu,

Zanzibar haitakuwa kwenye dhiki yoyote na Tanganyika kwa upande wa viongozi wanajuwa hilo.Wanafahamu siku Tanzania itakapo vunjika na Tanganyika ikawa huru, basi nanyi mutakuwa kama Uganda, Nigeria na nchi zilizo kuba na mapinduzi. Kunusuri haya basi bora tubakiye hivi hivi.

Zanzibar wakati inaungana na Tanganyika ilikuwa na kila kitu chake. Ilifanikiwa kufanya yaliyo mazuri ambayo Tanganyika imeyafanya kuanzia 1990 tena baada ya Ali Hassan Mwinyi kuachana na Ujamaa ati leo mwajifanya muna upenda ujamaa. Zanzibar ilifika hata kuisaidia SMT kama hujuwi!

msikilize tena Jussa kwa kituo. Ya Znazibar tuachiyeni sisi wazanzibari kwasasa jiandaeni kwa Tanganyika. Sijui itakuaje wafuasi wa CDM na CCM na akina NCCR na TLP yaani fujo tu. Sisi tushaonesha mfano kwamba tunaweza kufanya kzi pamoja na tuna SUK, nyinyi hata hamuja itafuta. Kasheshe tupu.
AllyZenj,

..mimi nilitegemea utanitia MOYO na MATUMAINI kwamba kuachana na huu muungano ni jambo la KHERI kwa WATANGANYIKA. sasa badala yake unaanza kuniambia tutakuwa kama Nigeria, au Kenya. Je, huoni kwa kufanya hivyo utapelekea tuendelee kuwangangania, wakati wenzetu mnataka "kupumua"??

..Hivi ni nani aliyekwambia kwamba Tanganyika ilikuwa na hali mbaya kabla au hata baada ya muungano?? Hujui kwamba wakati tunaungana Tanganyika ilikuwa kinara ktk uzalishaji wa mazao kama Katani,Kahawa,na Korosho?

..Sasa pamoja na kusema hayo, yapo makosa ambayo tuliyafanya sisi Watanganyika ambayo yalisababisha uchumi wetu kuporomoka. Makosa hayo hayakutokana na siasa za Ujamaa 100%, bali yalitokana na mahusiano yetu na vyombo vya fedha vya kimataifa mara baada ya vita vya Kagera.

..Unajua tofauti yetu sisi wa-Tanganyika na ndugu zetu wa Zanzibar ni kwamba hatulaumu kwamba matatizo yetu yamesababishwa na muungano, au Wazanzibari.

..Sasa tukirudi kwa upande wa Zanzibar, ni kweli mlikuwa na hali nzuri ya uchumi kabla ya muungano, na muda mfupi baadaye. Tatizo lilotokea ni kwamba uchumi wenu ulikuwa ukitegemea zao la KARAFUU. Uzalishaji wa karafuu ulianguka na hivyo kupelekea mtikisiko mkubwa ktk uchumi wa Zanzibar. Kama mngekuwa mmeendeleza UTALII, au VIWANDA, mngeweza kuhimili mtikisiko uliotokana na kuanguka kwa zao la karafuu.

..Kusaidiana ni jambo jema sana, tafadhali usilitumie kama njia ya kubezana au kusutana. Hata sisi wa-Tanganyika pamoja na umasikini wetu tumesaidia nchi nyingi sana majirani zetu na nyingine hata siyo majirani zetu, Zanzibar ikiwa moja wapo.

..Kuhusu CDM,CCM,NCCR kufanya kazi pamoja naamini hatuwezi kushindwa kama kutakuwa na nia ya dhati. Mbona nyinyi wenzetu mmeweza? Halafu Zanzibar siyo mbali kwa sisi wa-Tanganyika kuja kuchota BUSARA ikiwa tutataka kuanzisha serikali ya umoja wa kitaifa.
 
Last edited by a moderator:
KWani hatukutaka. Ilikuwa miaka nyuma kutamka tu muungano basi ni kosa kama kosa kwa kutilia shaka holocaust dhini ya jews au hujui hilo. Ubabe na nguvu na kuhahalisha ka nguvu ndio tumefika hapa tulipo fika. Kani scotland si hawautaki jeee na wao wauvunje tu si kuna taratibu zake. Nyinyi si munataka katiba mpya si na mufanye tu kama rahisi! Tatizo vichwa vyenu vizito ndio maana munauliza masuala ya kitoto. Hivi Nyerere alikuwa anakenda UK kufanya nini wakati anajua Tanganyika ya watanganyika? Hivi Afrika nzima wakijuwa ni ya kwao kwanini wakakubali kupangiwa siku ya kupewa uhuru kiasi kwamba Nyerere alikua akichelewesha kupewa Tanganyika ili wakipewa wapewe kwa pamoja. Si ilikuwa kazi rahisi kwame, nyerere, kenyata na wengine wakutane na kusema hawa wazungu wataondoka ka nguvu tu!

Wewe mpaka sasa hivi ushafanya nini kuuvunja muungano, binafsi.
 
masopakyindi Mkuu iupdate basi hii VIDEO kwenye Main (1st Post yako)

Jusa anaanza kuongea dakika ya 8:40

Majibizano na Warioba ni kuanzia dakika ya 15:40

Last edited by a moderator:
Jokakuu,

Alaa umesahau kamba wewe umesema sisi Zanzibar munatuonea huruma tukitoka kwenye muungano tutakuwa na matatizo!

Karafuu haijapatapo kushuka bei, wakuu wa serikali tu katika kutaka kuwanyonya wanyonge wakawa wanatubana kwenye kuinunuwa. Wimbo huo huo umedumu mpaka 2010. Kuja kwa SUK na CUF kuingia madarakani, karafuu ikatoka kwenye bei ya 4000Tzs kwa kilo ambayo serikali ilikuwa ikitowa mpaka 12,000Tzs. Ikagundulika Mombasa Kenya wao wanatowa 14,000Tzs kwa kilo na Kenya ikitambulika kwa mba wao ndio wanaongoza kwa uuzaji wa zao la karafuu kwa afrika nzima cha ajabu Kenya hawana mkarafuu hata mmoja! Hapo tu ikitoshe kwamba zao la karafuu halijapatapo kushuka bei.

Au unataka kuniambia kufika 2010 ndio hizi karafuu zimeanza kupanda bei? Tokea Waziri Mazrui Nassor waziri wa Biashara kupandisha bei na kusema atakaye towa taarifa juu ya watu wa magando basi tunzo yake 1,000,000Tzs. Sasa hivi tunaambiwa karafuu kilo 15,000Tzs, askari wa magendo wametulia hawana haja ya kuhangaika kwasababu hakuna anaye hangaika kwenda Mombasa na karafuu.

Ka upande wa Serikali, ilipanga kutowa miche 500,000 kwa mwaka huu. Na wametowa tenda kwa watu kufanya shughuli na serikali itayanunuwa. Hii ni kuonesha serikali ipo makini na inajuwa thamani ya karafuu, kwa hiyo sio hasara kununuwa miche na kuyatowa bure. Lengo ni 500,000, lakini tunaambiwa yametolewa mpaka sasa miche 700,000!

Mbali ya karafuu sasa hivi tunazungumzia Utalii shirikishi kwamba kila mmoja anashiriki kwa hili. Utalii tuutakao si huu wa vishuka, sin ahaja ya kukuelezea zaidi. Lakini hata kwa hili licha ya kuwa si la Muungano, mambo mengi tunapotaka kufunga mikataba, lazima tumshirikishe Membe na yeye ndiye anaye weka saini kama hataki ndio haweki na hiyo ndio kawaida ya Mawaziri wetu wa Muungano. Mhe. Hamad Masoud, aliyekuwa waziri wa miundo mbinu, alikwenda India akataka msaada mambo mengi na India wakakubali. Membe kakataa kuweka saini. Kumbuka sisi ni watu wa visiwa tulikuwa na mahusiano mazuri na wenzetu hata hii karafuu mteja wetu mkuu alikua Indonesia. Tukawa na ofisi zetu na nyumba zetu Dubai EAU mpaka karibu miaka ya 2000. Hivi sasa tunakosa fursa nyingi za kibiashara na wenzetu kwasababu ya muungano huu. Muungano sio tatizo kama tuna nia njema. Mimi nasema hivi. Wacha Mambo ya nje yawe ya muungano. Wizara isiyo ya muungano kama kilomo kwa Tanganyika ikitaka kwenda kuomba msaada China Membe awakilishe na sisi Kilimo tukipata msaada kutoka India na tuwakilishwe na Membe isiwe kikwazo na haya ndio kilio chetu lakini nyinyi hamupo wakweli hata kuwaeleza viongozi wenu.

Msikilize waziri wetu wa Fedha hao wengine wala usiwaguse uone madhila yenu kwetu sisi: Kamati ya Maridhiano Six: Semina ya BLW Kuhusu Marekebisho ya Katiba; July 2012; Part 4 - YouTube

Kuhus Tanganyika hiyo ni khofu yangu inawezekana ikawa sipo sahihi. Sasa ni juu yenu kuizingatia au kuachana nayo. Lakini dalili zinaonesha hivyo. Watu hawatokuwa tayari kuwachia sura za CCM kuendelea kudumu serikalini na ukweli lazima mume na Serikali ya mpito ambayo itajumuisha vyama vyote vilivyopo: hapo tayari kuna mgogoro maana TADEA hatokubali kuambiwa wewe mdogo au ulikuwa huna wabunge, kwa hiyo Dr Makaidi atacharukwa. Mrema mlalamishi, CDM mamaaaa watataka kuwapa wachaga tu na wawasahau wa maeneo mengine kama akina Zitto...
 
At last Ismael Jussa ameanza kufundishwa somo la Muungano the hard way!

Katika mchakato wa kukusanya maoni juu ya katina mpya, Mweneyekiti wa Tume ya Mabadiliko ya katiba Jaji Warioba imebidi atoe "tuition" kwa Bwana Jussa, ambaye kwa muda mrefu sasa amekuwa anonelea mifumo ya Muungano isiyo na tija.

Kulingana na taarifa kutoka gazeti la Nipashe, la leo 15/10/2012 nanukuu:

" Mwenyekiti wa Tume ya Mabadiliko ya Katinba Jaji Joseph Warioba amembana Mwakilishi wa Jimbo la Mji Mkongwe(CUF) Ismael Jussa aeleze kuhusu mfumo wa uendeshaji wa Muungano wa mkataba unavyopaswa kuwa na mgawanyo wa madaraka"
Jussa alikuwa ametoa maoni yake mbele ya Tume hiyo akijinadi kwa kutaka muungano wa mkataba.

Ndipo Jaji Warioba akamtaka atoe mifano ya mikataba kama hiyo inayotumiwa duniani, ambapo mheshiiwa huyu alianza kuweweseka na kudai kuwa ana mifano zaidi ya mia moja.

Baada ya kutoridhik na maelezo,Jaji Warioba alimbana zaidi na kumweleza kuwa nia ya Mwakilishi huyo hasa ilikuwa kuvunja muungano na si vinginevyo.

My Take
Muda wa kubwabwaja inaeleka mwisho kwa Bwana Jussa, he is meeting proffessionals katika field hiyo.

Haya ndio wasomi wetu wakiwa ktk nchi za magharibu hujikuta papara zao zikinyauka haraka.Wengi huishia lalama kuwa wamebaguliwa, utasikia Jussa akipata angle atakavyobwabwaja na kuomba round ingine.HIvyo ndivyo wazanzibar wengi wanavyofikiri mara wapatapo vyeti vya darasani na material zilizopindishwa zikiwa na heading siri nzito basi wao hukomaa navyo sana.

Mtanganyika yoyote naweza andika habari yoyote akaunganisha kanisa katoliki,freemason, Nyerere ,israel, Vatican halafu akaandika pale juu siri huku akisema matukio yanayoitwa siri.then unaweka mazingira muislam anaweza ona na kuiba,next friday misikiti yote bara na pwani itakuwa na copy na majukwaani watakuwa wampanda sana.Hivyo hivyo ndivyo dunia ya waarabu inavyochezewa na makfir wakubwa wa magharibi.
 
Jokakuu,

Alaa umesahau kamba wewe umesema sisi Zanzibar munatuonea huruma tukitoka kwenye muungano tutakuwa na matatizo!

Karafuu haijapatapo kushuka bei, wakuu wa serikali tu katika kutaka kuwanyonya wanyonge wakawa wanatubana kwenye kuinunuwa. Wimbo huo huo umedumu mpaka 2010. Kuja kwa SUK na CUF kuingia madarakani, karafuu ikatoka kwenye bei ya 4000Tzs kwa kilo ambayo serikali ilikuwa ikitowa mpaka 12,000Tzs. Ikagundulika Mombasa Kenya wao wanatowa 14,000Tzs kwa kilo na Kenya ikitambulika kwa mba wao ndio wanaongoza kwa uuzaji wa zao la karafuu kwa afrika nzima cha ajabu Kenya hawana mkarafuu hata mmoja! Hapo tu ikitoshe kwamba zao la karafuu halijapatapo kushuka bei.

Au unataka kuniambia kufika 2010 ndio hizi karafuu zimeanza kupanda bei? Tokea Waziri Mazrui Nassor waziri wa Biashara kupandisha bei na kusema atakaye towa taarifa juu ya watu wa magando basi tunzo yake 1,000,000Tzs. Sasa hivi tunaambiwa karafuu kilo 15,000Tzs, askari wa magendo wametulia hawana haja ya kuhangaika kwasababu hakuna anaye hangaika kwenda Mombasa na karafuu.

Ka upande wa Serikali, ilipanga kutowa miche 500,000 kwa mwaka huu. Na wametowa tenda kwa watu kufanya shughuli na serikali itayanunuwa. Hii ni kuonesha serikali ipo makini na inajuwa thamani ya karafuu, kwa hiyo sio hasara kununuwa miche na kuyatowa bure. Lengo ni 500,000, lakini tunaambiwa yametolewa mpaka sasa miche 700,000!

Mbali ya karafuu sasa hivi tunazungumzia Utalii shirikishi kwamba kila mmoja anashiriki kwa hili. Utalii tuutakao si huu wa vishuka, sin ahaja ya kukuelezea zaidi. Lakini hata kwa hili licha ya kuwa si la Muungano, mambo mengi tunapotaka kufunga mikataba, lazima tumshirikishe Membe na yeye ndiye anaye weka saini kama hataki ndio haweki na hiyo ndio kawaida ya Mawaziri wetu wa Muungano. Mhe. Hamad Masoud, aliyekuwa waziri wa miundo mbinu, alikwenda India akataka msaada mambo mengi na India wakakubali. Membe kakataa kuweka saini. Kumbuka sisi ni watu wa visiwa tulikuwa na mahusiano mazuri na wenzetu hata hii karafuu mteja wetu mkuu alikua Indonesia. Tukawa na ofisi zetu na nyumba zetu Dubai EAU mpaka karibu miaka ya 2000. Hivi sasa tunakosa fursa nyingi za kibiashara na wenzetu kwasababu ya muungano huu. Muungano sio tatizo kama tuna nia njema. Mimi nasema hivi. Wacha Mambo ya nje yawe ya muungano. Wizara isiyo ya muungano kama kilomo kwa Tanganyika ikitaka kwenda kuomba msaada China Membe awakilishe na sisi Kilimo tukipata msaada kutoka India na tuwakilishwe na Membe isiwe kikwazo na haya ndio kilio chetu lakini nyinyi hamupo wakweli hata kuwaeleza viongozi wenu.

Msikilize waziri wetu wa Fedha hao wengine wala usiwaguse uone madhila yenu kwetu sisi: Kamati ya Maridhiano Six: Semina ya BLW Kuhusu Marekebisho ya Katiba; July 2012; Part 4 - YouTube

Kuhus Tanganyika hiyo ni khofu yangu inawezekana ikawa sipo sahihi. Sasa ni juu yenu kuizingatia au kuachana nayo. Lakini dalili zinaonesha hivyo. Watu hawatokuwa tayari kuwachia sura za CCM kuendelea kudumu serikalini na ukweli lazima mume na Serikali ya mpito ambayo itajumuisha vyama vyote vilivyopo: hapo tayari kuna mgogoro maana TADEA hatokubali kuambiwa wewe mdogo au ulikuwa huna wabunge, kwa hiyo Dr Makaidi atacharukwa. Mrema mlalamishi, CDM mamaaaa watataka kuwapa wachaga tu na wawasahau wa maeneo mengine kama akina Zitto...
kwani miaka yote hamkuwa na mawaziri wazanzibar?hao majangili si nyie ndio mnawasaidia kwa njaa zenu,karafuu inakwenda kenya kupitia Mombasa mshirika wenu katika (umoja wa mabasha na mashoga) kuliko bara.Tena muombe Mungu Watu wa bara wakiamua anza rasmi zilima imekula kwenu.Hayo magugu mnyoyaacha yajiunze yenyewe kama kuku wa kienyeji,bara watageuza kuwa mazao yanayolimwa kisasa ,huo uchafu hatonunu mtu.

We unadai hela imeongezeka hembu nenda forodhani na mzee mmoja halafu mkanunue kipande cha pweza,halafu umuulize alinunu bei gai siku zi nyingi.Hiyo hela ya madafu haina dhamani tena wewe kijana kula kulala na kuswali, na subsidy ya serikali ikijaziwa na kuongezeka viwanda vya ndani vinavyotumia tengenezea madawa na vitu vingine.
 
AllyZenj,

..hakuna mahali nimeitabiria Zanzibar shida/machafuko ikiwa muungano utavunjika.

..kwa mtizamo wangu huu muungano ukivunjika wa-Zanzibari mtajifunza kujitegemea tena, na naamini hicho ni kitu kizuri.

..kuhusu karafuu, hakuna mahali nimezungumzia bei. kilichotokea Zanzibar ni kwamba uzalishaji wa karafuu ulianza kupungua miaka ya 70 na kuendelea. Mataifa mengine yalianza kuzalisha karafuu nyingi na yenye ubora kuliko iliyokuwa ikizalishwa Zanzibar.

..kuna uzi uliletwa hapa kuhusu hatua alizochukua Dr.Shein kuongeza bei ya karafuu ili kushindana na wafanya magendo na watoroshaji wa karafuu. mimi ni kati ya wachangiaji wa hapa JF waliopongeza hatua alizochukua Dr.Shein na serikali yake.

..kuhusu masuala ya Wizara ya Mambo ya Nje, kwa uelewa wangu Naibu Waziri ktk wizara hiyo anatoka Zanzibar. Sasa kama kuna mambo ya Zanzibar yanakwamishwa mnapaswa kumuuliza waziri huyo. Mkiona hampati majibu ya kutosha mnatakiwa kwenda kwa Makamu wa Raisi, na hata kwa Raisi mwenyewe.

..Mwisho, naomba turudi kwenye msingi wa hoja alizotoa Mh.Ismail Jussa. Mimi naona kama vile alishindwa kujieleza katika muda aliopewa. Sasa kutokana na hasira zake amekwenda kwenye facebook na kuanza kuporomosha matusi.

..Kwanini Mh.Jussa asitumie muda wake huko facebook kufanya jambo la "mbolea" kwa kuandika makala au rasimu inayoelezea huo "muungano wa mkataba" utafanya kazi namna gani?? Mbona ktk suala la serikali 3, CUF waliandika rasimu nzima ya katiba inayofuata mfumo huo??
 
Last edited by a moderator:
hana sera uyo mwarabu wa pemba kaishiwa na washajulkana kama wanataka kuvunja muungano ili CUF ipate kutawala wanamini ndani ya Muungano CUf haina lake
 
[h=1][/h]

SubmitCancel

Imetumwa Jumatano,Oktoba31 2012 saa 15:7 PM
Kwa ufupi
Viongozi wa Serikali ya Umoja wa Kitaifa Zanzibar (SUK) wanafikiri ukiwapo Muungano wa mkataba hawataukwaa tena ukubwa, na kwa dhana hiyo wanaamini ili waendelee kubaki kwenye madaraka watatumia vitisho vya kuwavua uanachama wenzao kwa kisingizio cha kuyasaliti Mapinduzi, au kwamba wanataka kuvunja Muungano.

SHARE THIS STORY

BAADHI ya watu ndani ya Chama cha Mapinduzi (CCM) wanadhani kwamba wanatawala badala ya kuongoza, ndio maana pamoja na tambo za majigambo na porojo nyingi majukwaani, bado hali halisi inawasuta kuhusu suala zima la Wazanzibari kutaka mabadiliko katika muundo wa Muungano. 

Miongoni mwa wana CCM hao, wengine ni viongozi katika Serikali ya Umoja wa Kitaifa Zanzibar (SUK) wanafikiri ukiwapo Muungano wa mkataba hawataukwaa tena ukubwa, na kwa dhana hiyo wanaamini ili waendelee kubaki kwenye madaraka watatumia vitisho vya kuwavua uanachama wenzao kwa kisingizio cha kuyasaliti Mapinduzi, au kwamba wanataka kuvunja Muungano. 

Mara nyingi wapo madarakani kutetea maslahi yao na matumbo yao pekee kiasi kwamba wanadiriki hata kusahau kwamba kinachowafanya waitwe viongozi ni kwa sababu ya Uzanzibari wao, na wala si kitu kingine. 

Watetezi wa mfumo wa sasa wa Muungano wanashindwa kuisemea Zanzibar katika kugawana rasilimali ya gesi asilia ambapo tangu kuanza kupatikana katika Mikoa ya Tanzania Bara, Zanzibar haijapata hata senti moja licha ya kuelezwa na kuandikwa kwenye katiba ya sasa kwamba jambo hilo ni la Muungano.

Wazanzibari wanaotaka Muungano wa mkataba wana hoja na kwa sababu ya hoja yao ndio maana kila siku idadi ya waumini wa mfumo huo wamekuwa wakiongezeka.

Ipo siku hali halisi itawasuta, ingawa hawatasutwa hadharani, lakini watajisuta wenyewe kwenye nafsi zao pale ambapo raia watakapoamua kuachana na muundo mkongwe wa Muungano na kuingia katika mfumo mpya.

Tunampongeza sana Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania na Mwenyekiti wa Chama cha Mapinduzi, Rais Jakaya Kikwete kwa uamuzi wake wa kuunda Tume kuwauliza wananchi wanataka Katiba ya aina gani au iliyopo iendelee. Huu ulikuwa uamuazi wa busara kwa Mkuu wa nchi, hata hivyo tunashangazwa na virukia waliochipuka kutaka kuwashurutisha wananchi kusema au kutoa maoni ambayo sio wanayoyaamini wananchi.

Ikiwa Serikali imeunda Tume ya kuchukua maoni ili kukuza demokrasia katika nchi, vipi wazuke watu wanaotaka kuichezea demokrasia kwa kulazimisha jambo ambalo kila mtu ana haki nalo kulitoleaa maamuzi? Ikiwa Mwenyekiti wa CCM Taifa ameeleza bayana siku ile alipozindua Tume ya Jaji Warioba pale Ikulu, Dar es Salaam kwamba kila mmoja awe huru kutoa maoni yake na wala usichukie pale mwenzako anapotoa maoni ambayo wewe hayakupendezi maana hata yako pia kuna watu hawayapendi, kwanini watu walazimishwe kutoa maoni ya aina fulani?

Katiba ya nchi katika nchi yoyote ya kidemokrasia ikiwemo Jamhuri ya Muungano wa Tanzania ni mali ya wananchi na hivyo ni wananchi pekee ndiyo wenye haki ya kuibadili na sio genge kama la mahafidhina ambalo halina haki kuwashurutisha raia wenzao kufuata matakwa yao.

Na kama si hivyo, hizi chuki za wazi zinazooneshwa dhidi ya wananchi wa Zanzibar sababu yake nini? Sauti tunazozisikia kutoka kwa mahafidhina kila kukicha ni kwa niaba na maslahi ya nani? Na kama watadai kuwa wanatumia haki yao ya msingi kama raia katika kutoa maoni kuhusu mambo ya nchi, ni lini wananchi wa Zanzibar walinyang'anywa haki hiyo ili wasiwe na uwezo wa kufanyia marekebisho Katiba ya Jamhuri ya Muungano wa Tanzania pale wanapoona inafaa kama hili la kutaka Muungano wa mkataba.

Hivyo, Katiba ya Jamhuri ya Muungano wa Tanzania ni mali ya Watanzania na si vinginevyo, ni Wazanzibari na Watanganyika pekee wenye haki ya kuibadili, na sio kiongozi wa Chama cha Siasa, muhafidhina atakayeweza kutoa agizo la kuzuia nguvu ya umma kutoa maoni wayatakayo.

Ni kawaida ya wakati kuwa ndio muamuzi wa kweli na huu ni wakati wa ukweli na uwazi, kwa hivyo ni wakati muafaka kuachana na tabia ya ubabe,vitisho na kusingiziana mambo yasiyokuwepo. Tuachane na ngonjera, Propaganda za wanasiasa vitimbakwiri.

Katiba ya Tanzania ni ya wananchi wote na katu si ya chama tawala cha CCM, hivyo si sahihi suala la mabadiliko ya kabla ya nchi yakafanywa ni agenda ya kujadiliwa na kuamuliwa na wana-CCM tu kwani CCM kwa sasa sio tena Chama Dola, ule wakati wa Chama Dola ulishapita tangu mwaka 1992.

Azma ya Wazanzibari kutaka mabadiliko ya muundo wa Muungano kuwa wa mkataba ni jambo ambalo halina ubishi kuwa lina mantiki ndani yake na wala isichukuliwe kuwa ni usaliti wa Mapinduzi au mfumo wa Muungano wa kikatiba. Tumesikia maoni yaliyotolewa na baadhi ya Wajumbe wa Baraza la Wawakilishi walipokutana na Tume ya Jaji Warioba walipotaka mamlaka kamili ya Zanzibar.

Wadadisi wa mambo Zanzibar wanasema hawakuamini pale walipowasikia baadhi ya Wawakilishi wa CCM wakiitetea nchi yao kutaka mamlaka kamili.Pengine kilichowafanya kuchukua uamuzi mgumu na sahihi ni uzalendo wao kwa Zanzibar maana pamoja na yote hayo wao watabaki kuwa Wazanzibari maana Muungano umekuja baadaye tu, Zanzibar ilikuwepo, itakuwepo na itaendelea kuwepo iwe katika Muungano au nje ya Muungano.

Suala linaloulizwa kigenge cha mahafidhina kinasimamia upande upi ikiwa Mnadhimu na Mjumbe wa Kamati Kuu anapendekeza Zanzibar isimamie yenyewe uhusiano wa kimataifa na mamlaka kamili ya uendeshaji wa mambo yake kama vile kujiunga na OIC, Waziri wa Ulinzi na Jeshi la Kujenga Taifa ambaye pia ni mjumbe wa Kamati Kuu ya CCM, Shamsi Vuai Nahodha anataka orodha ya mambo ya Muungano kupunguzwa na pia gawio la asilimia 4.5 Zanzibar liongezwe hadi angalau asilimia 15, wewe mpigakura wa Pongwe, Kinduni, Matemwe, Kitope,Wawi, Chake Chake, Umbuji na kwingineko unasubiri nini kutaka mamlaka kamili ya Zanzibar?

Au kwa kuwa wengi wanaounga mkono mabadiliko ya muundo wa Muungano ni watu walioanzisha na kuunga mkono maridhiano ya kisiasa Zanzibar yaliyosababisha marekabisho ya 10 ya Katiba yaliyozaa SUK, hivyo kuendeleza hulka ya kupinga hata kwa jambo zuri lenye manufaa kwa nchi?

Genge hili naliona ni lenye donge dhidi ya watu wenye fikra ya mabadiliko katika siasa za Zanzibar na wengine wana chuki binafsi na aliyekuwa Rais wa Zanzibar, Amani Abeid Karume na Makamu wa kwanza wa Rais Maalim Seif Shariff Hamad ambao ni manahodha wa maridhiano ya kisiasa Zanzibar yaliyosabisha nchi kupata utulivu wa kisiasa.

Kundi la pili, ni wale watu hasa wa upande wa Tanganyika wasiopenda kuona Zanzibar kuwa na mamlaka yake kamili, hawataki kuitambua kuwa Zanzibar iliingia katika Muungano mwaka 1964 ikiwa ni nchi yenye mamlaka kamili na kwamba iliingia kwa makubaliano na siyo kutekwa au kulazimishwa na kubaki na mamlaka ya mwisho juu ya masuala fulani chini ya Serikali yake.

Huu si wakati tena wa wanasiasa, wasomi, wakulima, wafanyakazi au wakwezi kuendelea kukwepa ukweli, lazima tubadili mambo kutegemea na wakati uliopo, muundo wa Muungano wa mkataba ndio tiba sahihi kwa Muungano wetu, na ikiwa kuna watu wa kulaumiwa katika hali hii ya udhaifu wa muundo wa Muungano tuliyonayo ni wale waliochangia au kusababisha kuwepo kwa hali.

Ni dhahiri sasa kuwa waasisi wa muundo wa Muungano wa kikatiba ambao wengine tumewasikia wakitamka katika mikutano ya hadhara katika uchaguzi mdogo wa Jimbo la Bububu, kuwa muundo wa Muungano utabaki kama ulivyo watu watake wasitake hautabadilika, na kula viapo kuulinda kwa gharama zozote kama ulivyo, kila mmoja alikuwa na sababu nyingine za ziada zilizomfanya aukubali Muungano kwa wakati ule.

Baba na muasisi wa Taifa la Zanzibar, marehemu Mzee Abeid Amani Karume kama angekuwa hai hivi leo sidhani kama angeweza kupingana na mawazo ya wanaotaka mabadiliko ya muundo wa Muungano, bali angeunga mkono fikra za kuwa na Muungano wa mkataba kwani siku za mwanzoni mwa kuundwa kwa Muungano alisikika akisema wananchi (Wazanzibari) wasiwe na shaka, Muungano ni kama koti, likikubana unalivua.

MWISHO.
 
kama tatizo la zanzibar ni muungano na wanzanzibar wengi wanaamini hivyi.kwa vile waswahili mara nyingi wanasema anayekanyagwa ndo apigae kelele asiye kanyagwa hunyamaza kimya.hapo inaonesha wanzanzibar muungano ni tatizo jee?serikali tatu ndo zinakuja hzo zanzibar mutaimudu?
 
Zanzibar yenye Malaka Kamili Kitaifa na Kimataifa ikifuatiwa na Muungano wa Mkataba na Tanganyika itaitwa Jamhuri ya Watu wa Zanzibar na italinda na kuheshimu yafuatayo:
Zanzibar itakuwa ni Nchi ya Kidemokrasia.
Zanzibar italinda na kuheshimu haki za binaadam.
Zanzibar italinda haki za makundi mbalimbali na makundi yenye mahitaji maalum.Zanzibar itaridhia Mikataba mbalimbali ya kimataifa.
Zanzibar itapinga ugaidi.
Zanzibar haitokuwa chaka la magaidi.
Zanzibar itapiga vita madawa ya kulevya.
Zanzibar itajiunga na Jumuiya za Kikanda na Jumuiya za Kimataifa.
Zanzibar haitoruhusu ardhi yake itumike kushambulia Nchi jirani.
Zanzibar itaendelea kuwa mlizi wa Mwambao wa Afrika Mashariki.
Zanzibar haitokuwa chaka la magaidi.
Zanzibar italinda haki ya kuabudu.
Zanzibar itaruhusu vyama vya siasa na Mgombeya Binafsi.
Zanzibar haitoingilia Uhuru wa Mahkama.
Zanzibar Mamlaka ya kuendesha nchi yatakuwa mikononi mwa wananchi.
Zanzibar itaheshimu vyombo vya habari.
Zanzibar itaheshimu Uhuru wa kujieleza, uhuru wa mawazo na maoni.
Zanzibar itarudisha hadhi yake ya kuwa kitovu cha elimu.
Zanzibar itakuwa ni kituo cha biashara duniyani.
Zanzibar ni njema mwenye heshima zake aje.
Zanzibar itayahashimu haya na mengine kama haya ilikuendena na mahitaji ya duniya ya sasa.
Jamhuri ya Watu wa Zanzibar – KWANZA!
 
Hayo ni maoni yako binafsi au maoni ya kikatiba ya wananchi wa Zanzibar?
 
Jamhuri ya Muungano wa Tanzania kwanza. Moja shika si kumi ndnda uje. Mkataba huo ni kucheza kamari.
 
Back
Top Bottom