Jaji Samatta awalipua Polisi


A

abdulahsaf

JF-Expert Member
Joined
Aug 31, 2010
Messages
859
Likes
4
Points
0
A

abdulahsaf

JF-Expert Member
Joined Aug 31, 2010
859 4 0
Jaji mkuu mstaafu Bw Barnabas Samatta
Barnabas-Samatta.jpg

[h=2]Saturday, December 1, 2012[/h]

Aeleza wanavunja haki za binadamu .
Asema wana mtazamo wa chama kimoja

Na Mwinyi Sadallah

Jaji Mkuu mstaafu, Barnabas Samatta, amelishukia jeshi la Polisi na kusema linachangia kuchochea uvunjaji wa haki za binadamu nchini.

Amesema miongoni mwa haki zinazovunjwa na jeshi hilo ambalo kimsingi, linapaswa kuwalinda raia na mali zao, ni kuzuia uhuru wa kutoa maoni na kuandamana.

Jaji Samatta alisema hayo jana wakati akifungua kongamano la wasaidizi wa sheria, lililoandaliwa na Kituo cha Huduma za Sheria Zanzibar (ZLSC), ikilenga kujadili mambo mbalimbali kisiwani Pemba.


Kauli ya Samatta imekuja siku chache baada ya Rais Jakaya Kikwete, kulihusisha jeshi hilo na harakati za kisiasa za Chama Cha Mapinduzi (CCM) ambacho yeye (Kikwete) ni Mwenyekiti wake.

Akifungua Mkutano Mkuu wa CCM mjini Dodoma hivi karibuni, Rais Kikwete, pamoja na mambo mengine, alikaririwa akitoa rai kwa chama hicho kujibu hoja za upinzani badala ya kuwategemea polisi.

Kauli ya Rais Kikwete ilitafsiriwa kwa namna tofauti, huku ikihusishwa na malalamiko ya siku nyingi ya upinzani na asasi za kiraia, kwamba CCM inasaidiwa zaidi na vyombo vya dola kubaki madarakani.

Ingawa Jaji Samatta hakugusia ama kulihusisha jeshi hilo dhidi ya chama cha siasa, alisema polisi ni moja ya vyombo vinavyotumika kunyima uhuru wa kutoa maoni na kuandamana kwa raia. “Polisi bado wana mitazamo ya mfumo wa chama kimoja, wanakataza maandamano hata pale ambapo ni wazi kabisa kuwa hakuna hatari, usumbufu au amani kuvurugwa,”alisema Jaji Samatta.

Alisema mtazamo huo ni potofu kwa sababu unasababisha wananchi kubakia (moyoni) na mambo yanayowasumbua.

Kwa mujibu wa Jaji Samatta, uhuru wa mawazo ni haki ya msingi isiyotokana na fadhila ya watawala kwa raia. Alisema haki hiyo na ile ya kuandamana ni za msingi na kwamba kuwazuia kufanya hivyo ni mtazamo potofu.

Aliwakumbusha polisi wanaominya uhuru wa kutoa maoni na kuandamana, wakumbuke kwamba katika mfumo wa demokrasia ya kweli, si lazima wananchi waimbe wimbo mmoja. “Katika demokrasia sio lazima kila mtu aimbe wimbo huo huo...uhuru wa mawazo ni wa msingi sana… unachukuliwa kama kitu cha kawaida, kila mtu ana haki ya msingi juu ya suala lolote linalogusa watu kwa jumla,” alisema.

Jaji Samatta alisema maandamano sio mtazamo potofu kama inavyodhaniwa na polisi, ndio maana katika nchi za mabara ya Ulaya, Amerika na Asia, ‘upepo’ huo unaendelea kutumiwa na wananchi kudai haki zao.

Alisema kuzuia maadamano kunaminya fursa kwa watawala kufahamu mambo mengi kutoka kwa waliowaweka madarakani, hasa kuhusu kitu wanachokitaka na wasichotaka. “Kwa nini wananchi wasiruhusiwe kutumia maandamano, kuwajulisha watawala kuhusu mambo yanayowakera ili yapatiwe ufumbuzi,” alihoji.

Hata hivyo, Jaji Samatta alisema ingawa haki ya kuandamana ina mipaka yake, lakini mipaka hiyo imewekwa na sheria na wala si jeshi la polisi. Hata hivyo, Jaji Samatta, alisema ipo haja kwa wananchi kutii sheria, kwa vile hali hiyo inachochea kustawisha demokrasia na uhuru.

“Vyombo vya serikali vinawajibika kwa sheria, kama ilivyo kwa mwananchi,” alisema.

AONYA KULIPIZA VISASI

Jaji Samatta alisema vitendo vya kulipiza kisasi si utamaduni unaoendana na ustaarabu wa taasisi za umma hususani vyombo vilivyo chini ya serikali, badala yake kuwajibika kwa mujibu wa sheria.

Alisema inapotokea vyombo hivyo kuipinda au kuidharau sheria, ‘tiba’ si vurugu, bali kuziomba mahakama zitamke juu ya uhalali wa vitendo hivyo na kuchukua hatua nyingine za kisheria.

AHIMIZA UWAJIBIKAJI ASASI ZA KIRAIA

Jaji Samatta alisema asasi zisizo za serikali, zinazoshughulikia haki za binadamu zinapaswa kuwajibika zaidi, zikisaidiana na vyombo vingine ndani ya nchi.

Chanzo - Nipashe


Imewekwa na MAPARA at 9:37 AM
 
luvcyna

luvcyna

JF-Expert Member
Joined
Feb 24, 2009
Messages
1,472
Likes
1,120
Points
280
luvcyna

luvcyna

JF-Expert Member
Joined Feb 24, 2009
1,472 1,120 280
ningelikuwa mwandish ningetafuta nafasi ya kumuuliza yeye alichukua hatua gani pale wastaafu wa E.A.C walipopigwa na kudhalilishwa na polis wakidai haki zao angali yupo madarakani kama jaji mkuu
 
don-oba

don-oba

JF-Expert Member
Joined
Dec 8, 2011
Messages
1,387
Likes
20
Points
135
don-oba

don-oba

JF-Expert Member
Joined Dec 8, 2011
1,387 20 135
Asante baba SAMATTA.
 
Mawenzi

Mawenzi

JF-Expert Member
Joined
Sep 21, 2010
Messages
1,257
Likes
12
Points
0
Mawenzi

Mawenzi

JF-Expert Member
Joined Sep 21, 2010
1,257 12 0
Wapemba walipouawawa na Mkapa alikuwa ni jaji mkuu. Alifanya nini?
 
M

mringi

Member
Joined
Apr 4, 2012
Messages
99
Likes
1
Points
0
M

mringi

Member
Joined Apr 4, 2012
99 1 0
Tuwashukuru wastaafu wetu ambao kila wanapopata jukwaa hawasiti kukumbusha jamii kwa ujumla wake pale walopopotoka,je tulitaka afungue mashitaka, apeleke ushahidi na atoe hukumu mmwenyewe,Big up Ex Chief Judge
 
KAZIMOTO

KAZIMOTO

JF-Expert Member
Joined
Aug 19, 2010
Messages
1,073
Likes
1
Points
0
KAZIMOTO

KAZIMOTO

JF-Expert Member
Joined Aug 19, 2010
1,073 1 0
mzee anazeeka vizuri. historia itawahukumu wanaompuuza
 
Jiwejeusi

Jiwejeusi

JF-Expert Member
Joined
May 3, 2011
Messages
754
Likes
2
Points
0
Jiwejeusi

Jiwejeusi

JF-Expert Member
Joined May 3, 2011
754 2 0
ningelikuwa mwandish ningetafuta nafasi ya kumuuliza yeye alichukua hatua gani pale wastaafu wa E.A.C walipopigwa na kudhalilishwa na polis wakidai haki zao angali yupo madarakani kama jaji mkuu
Soma criminal procedures acts ya tz, then uliza ulichouliza kama utatoa sauti.
 
BHULULU

BHULULU

JF-Expert Member
Joined
Jun 28, 2012
Messages
4,907
Likes
145
Points
160
BHULULU

BHULULU

JF-Expert Member
Joined Jun 28, 2012
4,907 145 160
Hivi vizee ni vinafiki, enzi zake kuna maovu mengi tu yalitendeka lakini hakukemea.Vinasubiri vikishastaafu ndiyo vinajifanya kuona makosa na kukosoa.
 
C

Chibenambebe

Senior Member
Joined
Mar 27, 2012
Messages
148
Likes
0
Points
33
C

Chibenambebe

Senior Member
Joined Mar 27, 2012
148 0 33
Tusimshambulie sana huyu mzee kwa sababu kuu mbili 1. Hunda ameshatambua kuwa alikuwa hatendi haki na amekosa nafasi ya kutubu na hivyo kujaribu kukosoa zile kasoro ambazo hata yeye alizifanya 2. Kukosea kwake hakumpotezei yeye uhalali wa kuhoji na kukemea maovu though yeye aliyafanya!
 
Duduwasha

Duduwasha

JF-Expert Member
Joined
Nov 3, 2010
Messages
5,223
Likes
2,306
Points
280
Duduwasha

Duduwasha

JF-Expert Member
Joined Nov 3, 2010
5,223 2,306 280
Hivi bado wana bifu na Mkw3re?
 
K

KIRUMO

JF-Expert Member
Joined
Sep 25, 2012
Messages
376
Likes
5
Points
35
K

KIRUMO

JF-Expert Member
Joined Sep 25, 2012
376 5 35
Hivi vizee ni vinafiki, enzi zake kuna maovu mengi tu yalitendeka lakini hakukemea.Vinasubiri vikishastaafu ndiyo vinajifanya kuona makosa na kukosoa.
Hujui usemacho.
 
M

Mgelukila

JF-Expert Member
Joined
May 27, 2012
Messages
224
Likes
0
Points
0
M

Mgelukila

JF-Expert Member
Joined May 27, 2012
224 0 0
Hivi bado wana bifu na Mkw3re?
Sammata, J ukipitia hukumu zake zimesimama sana, usimlaumu kwa matukio maana the court can't move her self you must sue the govt in clear allegation the Judge shall Act upon those allegation. Haki ni gradual change it need right time, like now awareness is big.
 
Candid Scope

Candid Scope

JF-Expert Member
Joined
Nov 8, 2010
Messages
11,889
Likes
137
Points
160
Candid Scope

Candid Scope

JF-Expert Member
Joined Nov 8, 2010
11,889 137 160
jaji%20na%20polisi.jpg

Aeleza wanavunja haki za binadamu
Asema wana mtazamo wa chama kimoja

Jaji Mkuu mstaafu, Barnabas Samatta, amelishukia jeshi la Polisi na kusema linachangia kuchochea uvunjaji wa haki za binadamu nchini.
Amesema miongoni mwa haki zinazovunjwa na jeshi hilo ambalo kimsingi, linapaswa kuwalinda raia na mali zao, ni kuzuia uhuru wa kutoa maoni na kuandamana. Jaji Samatta alisema hayo jana wakati akifungua kongamano la wasaidizi wa sheria, lililoandaliwa na Kituo cha Huduma za Sheria Zanzibar (ZLSC), ikilenga kujadili mambo mbalimbali kisiwani Pemba.

Kauli ya Samatta imekuja siku chache baada ya Rais Jakaya Kikwete, kulihusisha jeshi hilo na harakati za kisiasa za Chama Cha Mapinduzi (CCM) ambacho yeye (Kikwete) ni Mwenyekiti wake. Akifungua Mkutano Mkuu wa CCM mjini Dodoma hivi karibuni, Rais Kikwete, pamoja na mambo mengine, alikaririwa akitoa rai kwa chama hicho kujibu hoja za upinzani badala ya kuwategemea polisi.

Kauli ya Rais Kikwete ilitafsiriwa kwa namna tofauti, huku ikihusishwa na malalamiko ya siku nyingi ya upinzani na asasi za kiraia, kwamba CCM inasaidiwa zaidi na vyombo vya dola kubaki madarakani. Ingawa Jaji Samatta hakugusia ama kulihusisha jeshi hilo dhidi ya chama cha siasa, alisema polisi ni moja ya vyombo vinavyotumika kunyima uhuru wa kutoa maoni na kuandamana kwa raia. “Polisi bado wana mitazamo ya mfumo wa chama kimoja, wanakataza maandamano hata pale ambapo ni wazi kabisa kuwa hakuna hatari, usumbufu au amani kuvurugwa,”alisema Jaji Samatta. Alisema mtazamo huo ni potofu kwa sababu unasababisha wananchi kubakia (moyoni) na mambo yanayowasubua.

Kwa mujibu wa Jaji Samatta, uhuru wa mawazo ni haki ya msingi isiyotokana na fadhila ya watawala kwa raia. Alisema haki hiyo na ile ya kuandamana ni za msingi na kwamba kuwazuia kufanya hivyo ni mtazamo potofu. Aliwakumbusha polisi wanaominya uhuru wa kutoa maoni na kuandamana, wakumbuke kwamba katika mfumo wa demokrasia ya kweli, si lazima wananchi waimbe wimbo mmoja. “Katika demokrasia sio lazima kila mtu aimbe wimbo huo huo...uhuru wa mawazo ni wa msingi sana… unachukuliwa kama kitu cha kawaida, kila mtu ana haki ya msingi juu ya suala lolote linalogusa watu kwa jumla,” alisema.

Jaji Samatta alisema maandamano sio mtazamo potofu kama inavyodhaniwa na polisi, ndio maana katika nchi za mabara ya Ulaya, Amerika na Asia, ‘upepo’ huo unaendelea kutumiwa na wananchi kudai haki zao. Alisema kuzuia maadamano kunaminya fursa kwa watawala kufahamu mambo mengi kutoka kwa waliowaweka madarakani, hasa kuhusu kitu wanachokitaka na wasichotaka. “Kwa nini wananchi wasiruhusiwe kutumia maandamano, kuwajulisha watawala kuhusu mambo yanayowakera ili yapatiwe ufumbuzi,” alihoji.

Hata hivyo, Jaji Samatta alisema ingawa haki ya kuandamana ina mipaka yake, lakini mipaka hiyo imewekwa na sheria na wala si jeshi la polisi. Hata hivyo, Jaji Samatta, alisema ipo haja kwa wananchi kutii sheria, kwa vile hali hiyo inachochea kustawisha demokrasia na uhuru. “Vyombo vya serikali vinawajibika kwa sheria, kama ilivyo kwa mwananchi,” alisema.

AONYA KULIPIZA VISASI
Jaji Samatta alisema vitendo vya kulipiza kisasi si utamaduni unaoendana na ustaarabu wa taasisi za umma hususani vyombo vilivyo chini ya serikali, badala yake kuwajibika kwa mujibu wa sheria. Alisema inapotokea vyombo hivyo kuipinda au kuidharau sheria, ‘tiba’ si vurugu, bali kuziomba mahakama zitamke juu ya uhalali wa vitendo hivyo na kuchukua hatua nyingine za kisheria.

AHIMIZA UWAJIBIKAJI ASASI ZA KIRAIA

Jaji Samatta alisema asasi zisizo za serikali, zinazoshughulikia haki za binadamu zinapaswa kuwajibika zaidi, zikisaidiana na vyombo vingine ndani ya nchi.
 
Mzalendo80

Mzalendo80

JF-Expert Member
Joined
Oct 30, 2010
Messages
2,481
Likes
416
Points
180
Mzalendo80

Mzalendo80

JF-Expert Member
Joined Oct 30, 2010
2,481 416 180
Unafiki kama huu ndio nisioutaka kuusikia, alikuwa wapi miaka yote mpaka anastaafu ndio anajifanya kuzungumzia haki za binaadam. Amekosa nafasi za wale majaji waliostaafu kuajiriwa tena naona hasira zake anaziwekeza kwa Serikali ya kichovu inayoongozwa Vasco. Kama angepatiwa ajira yoyote na Vasco asingezungumza chochote kuhusu haki za binaadam.
 
Mwamba Usemao Kweli

Mwamba Usemao Kweli

JF-Expert Member
Joined
Oct 5, 2012
Messages
745
Likes
51
Points
45
Age
98
Mwamba Usemao Kweli

Mwamba Usemao Kweli

JF-Expert Member
Joined Oct 5, 2012
745 51 45
Hivi vizee ni vinafiki, enzi zake kuna maovu mengi tu yalitendeka lakini hakukemea.Vinasubiri vikishastaafu ndiyo vinajifanya kuona makosa na kukosoa.
Kwahiyo tuache makosa yaendelee au tujisahihishe sasa?
 
Mzalendo80

Mzalendo80

JF-Expert Member
Joined
Oct 30, 2010
Messages
2,481
Likes
416
Points
180
Mzalendo80

Mzalendo80

JF-Expert Member
Joined Oct 30, 2010
2,481 416 180
Kwahiyo tuache makosa yaendelee au tujisahihishe sasa?

Tunachosema ni kuwa alikuwa wapi kipindi chote cha haya mtukio mpaka anakuja kusema sasa baada ya kustaafu? mbona alikuwa hasemi huu ukweli wakati yupo active? Ni mnafiki tu hana jipya
 
BHULULU

BHULULU

JF-Expert Member
Joined
Jun 28, 2012
Messages
4,907
Likes
145
Points
160
BHULULU

BHULULU

JF-Expert Member
Joined Jun 28, 2012
4,907 145 160
Kwahiyo tuache makosa yaendelee au tujisahihishe sasa?
Tatizo langu kuu ni "UNAFIKI" wa hivi vizee,vikiwa kwenye system vipofu, vikitoka vinakuwa na macho matatu.Fikiria kama angekuwa amepewa "mfupa" baada ya kustaafu, kama angesema hayo ambayo amesema.
 
K

Kindimbajuu

JF-Expert Member
Joined
Jul 8, 2009
Messages
710
Likes
16
Points
35
K

Kindimbajuu

JF-Expert Member
Joined Jul 8, 2009
710 16 35

Tunachosema ni kuwa alikuwa wapi kipindi chote cha haya mtukio mpaka anakuja kusema sasa baada ya kustaafu? mbona alikuwa hasemi huu ukweli wakati yupo active? Ni mnafiki tu hana jipya
kila atakae kosoa jambo baadahi ya wananchi kazi yetu ni kuuliza alikuwa wapi siku zote hizi. sasa siku zote hizi zitaisha lini?. amezungumzia tatizo la polisi kuto kubadilika na wakati. hajasema kuwa enzi yake polisi waliwai badilika. wala hajajitenga na hilo tatizo la ugumu wa polisi kutobadilika. ametoa wito wa polisi kubadilika kwakuwa amejua hawajabadilika. tutaendelea kuuliza siku zote ulikuwa wapi... wakati umasikini na ubinafsi utazidi kututafuna hata milele
 
L

lufungulo k

JF-Expert Member
Joined
Apr 19, 2012
Messages
1,754
Likes
820
Points
280
L

lufungulo k

JF-Expert Member
Joined Apr 19, 2012
1,754 820 280
nalia na wanazuoni kama huyu, nadhani amemasikia Tundu lissu , akilalamika juu ya uteuzi wa majaji, ktk hili hana mchango kweli? mpaka atuzuge kwenye issue ya polisi, binafsi nadhani anapaswa afafanue hili kwanza maana linaihusu fani ya kutoa haki, ambayo yy anaona polisi wanaiminya. Tundu Lissu yy haoni tatizo polisi anaona haki ya watanzania inataka au inachakachuliwa na fani ya sheria hususani uteuzi wa majaji tafadhali Mh Samatta achana na polisi ,muunge mkono MH LISSU au mponde kwa data, kisha kosoa polisi.
 

Forum statistics

Threads 1,235,535
Members 474,641
Posts 29,225,925