Jaji Mutungi: Namtambua Profesa Lipumba

Ufipa-Kinondoni

JF-Expert Member
Jan 3, 2012
4,582
2,783
Hii ni taarifa iliyochapishwa na gazeti la Mwananchi leo asubuhi.

Je CUF ipi itasimama?

=====

Dar es Salaam. Hatimaye Msajili wa Vyama vya Siasa nchini, Jaji Francis Mutungi amesema anamtambua Profesa Ibrahim Lipumba kama Mwenyekiti wa CUF na Maalim Seif ni Katibu Mkuu.

Amesema hana hofu ya kuchafuliwa kutokana na tuhuma zinazotolewa dhidi yake.

Kauli ya Jaji Mutungi imekuja baada ya taarifa na kauli za matusi na kejeli zilizomuhusisha yeye na ofisi yake kusambaa kwenye mitandao mbalimbali ya kijamii baada ya kuidhinisha zaidi ya Sh300 milioni za ruzuku kwenda kwenye akaunti ambayo kamati ya uongozi ya CUF ilidai siyo ya chama hicho.

Taarifa za msajili kuingiza fedha hizo kwenye akaunti hiyo na baadaye kutolewa kwa njia inayoonekana kutia shaka zilitolewa na Mwenyekiti wa Kamati ya Uongozi ya CUF, Julius Mtatiro ambaye alilinganisha suala hilo na uchotwaji wa zaidi ya Sh300 bilioni zilizokuwa kwenye akaunti ya Tegeta Escrow.

Chanzo: Mwananchi
 
Kada wa ccm anatumika vibaya lakini hawatafanikiwa maana wananchi tupo na maalim Seif Sharif Hamad
 
Jaji Mtungi usifanye watanzania wote mazuzu, na hiyo dhambi unayo ifanya itatafuna mpaka kizazi chako.
 
Back
Top Bottom