Jaji Mkuu: Tusijifananishe na Kenya, Mahakama zetu zipo huru zaidi

Asante Mkuu, hili swali hata mimi nilijiuliza. Anaonekana kabisa kutoka "body language" kuwa he was extremely uncomfortable inside kana kwamba alilishwa yale maneno. Ni wazi alikuwa katika juhudi za kumridhisha aliyemteua.
Kwanza wala si busara kumsema jirani yako kiasi kile kuhusu ukabila kwenye press conference. It is simply not a wise thing to do. Huu u-Professor hauna maana huku kwetu nini? Profesa huongelea kitu alichokifanyia utafiti na wazo litokalo kwa Profesa ni lazima liwe linatekelezeka. Napata kichefuchefu kusikiliza mawazo ya ma-Profesa wa Tanzania au ndiyo tunao wengi kina maji marefu nini????
Naomba kufahamu ali graduate wapi huyu? Uprof ni UDSM? loh!
Hii ni aibu kwa Taifa letu.
Huyu ameshatishwa. Mahakama itakuwa compromised. hakuna haki tena mahakama.
 
Prof, si kweli kuwa Kenya admires Tanzania judiciary! Usipotoshe Prof.
Sasa wewe hata kuhoji juu ya matumizi mabaya ya michango ya Kisu unashindwa halafu leo bila aibu eti unadai eti Prof. tena wa Sheria tena Jaji mkuu wa nchi wewe unadai amepotosha. Wewe ni Chadema hakika watu feki.
 
Huyu ameshatishwa. Mahakama itakuwa compromised. hakuna haki tena mahakama.
Nikisema keshachukuliwa Msukule nitakuwa nakosea? Maana naona kama hili jambo lipo kwenye uongozi wa nchi yetu! Nani angeniambia Polepole angekuwa alivyo sasa niamini?
 
Mi nilikuwa hata simfahamu wakati akikaimu. Hebu tumpe muda inawezekana ni strategy yake ili ajulikane, u never know. I dont see the light at the end of the tunnel.
 
Oooooooh!! My goodness! wamefanya nini huyo mzee. Mbona hapo kabla hakuwa hivyo?
Au unapokaimu nafasi, kuna vitu unatakiwa kuongea na kuna ambavyo hutakiwi kuongea?
Alikua hajaHAKIKIWA
 
Hivi huyo jaji wa serikali tena professor anawezalinganisha Uhuru wa mahakama ya Kenya na Tz, Hata Mtoto wa chekechea ukimuuliza bila kuchelewa atasema Kenya wako mbali sana.nawacwac na uprofessor wake.kusoma hajui hata picha haoni mpaka kuingia choo cha kike?
 
Nikisema keshachukuliwa Msukule nitakuwa nakosea? Maana naona kama hili jambo lipo kwenye uongozi wa nchi yetu! Nani angeniambia Polepole angekuwa alivyo sasa niamini?
Haya majina ya Ibra naanza kuwa na mashaka nayo! Msukule tayari. Hakupashwa kufanya press conference katu kama mahakama!
 
Sasa wewe hata kuhoji juu ya matumizi mabaya ya michango ya Kisu unashindwa halafu leo bila aibu eti unadai eti Prof. tena wa Sheria tena Jaji mkuu wa nchi wewe unadai amepotosha. Wewe ni Chadema hakika watu feki.
Fake mama yako
 
Jaji mkuu wa Tanzania Ibrahim Juma amaesema sio sahihi kufananisha mahakama zetu na mahakama za Kenya na kusema mahakama zetu zipo huru zaidi


Anasena tujivunie sheria zetu ili tuendelee kupata haki. Je ni haki ipi wakati katiba inasema matokeo ya uchaguzi yakishatangazwa na tume ya uchaguzi hayawezi kuhojiwa mahakamani?
 
Inategemea jaji Mkuu alimaanisha uhuru gani. labda alimaanisha uhuru wa kutafsiri sheria au wa uhuru wa kupanga mda wa kusikiliza kesi (kalenda) au uhuru wa kuajiri watumishi wa mahakama. Lakini kiukweli uhuru wa mahakama kwa tanzania ni neno la kusadikika.

Ni bora kabisa mahakama za mwanzo na mahakama za wilaya zina chembe chembe ya uhuru wa mahakama. Lakini ukifikia Mahakama za Mahakimu wakazi, Mahakama Kuu na Mahakama ya Rufaa uhuru wa mahakama haupo. Ndio kuna kesi mahakimu na majaji wanaamua kwa utashi wao, tena bila kuhofia chochote. Lakini kuna kesi mahakimu na majaji wanaamua si kwa utashi wao wala si kwa kufuata misingi ya kisheria, bali wanaamua kwa misingi ya matakwa ya Serikali kuu (executive).

Kuna kesi nyingi sana tu (sitazitaja hapa kwa makusudi maalumu) mahakama ilitoa maamuzi hata kabla ya kusikiliza kesi hizo, kilichofanyika ni kutekeleza utaratibu tu ili kuonesha utaratibu umefuatwa. Nina mifano kibao ya kesi ambayo majaji (zilizokuwa mahakama kuu) na mahakimu (kwa kesi za mahakama za wilaya na mkoa) walifuatwa faragha na kuambiwa waharakishe kusikiliza kesi hizo, au zile walizoambiwa wacheleweshe usikilizwaji wa kesi hizo kwa makusudi, na zingine waliambiwa wafanye wafanyalo lakini uamuzi wa mwisho uwe na muelekeo fulani.

Hivi kuna anaejua kuwa hakuna kesi ambayo serikali (executive) ina interest nayo ambayo hupangiwa kusikilizwa na jaji au hakimu wa hovyo au wasiuyempenda? Ni utaratibu uliopo majaji hupangiwa kesi kulingana na yeye alivyo na mtizamo wake kwenye serikali, na mahakimu wanapangiwa kesi kulingana na kesi yenyewe.
Ungezitaja hizo kesi hoja yako ingekaa vizuri sana. Uneharibu kuzificha kesi hizo......!
 
Yaani msitarajie uteuzi wa Bwana yule utawaleta watu wanaojielewa ktk nchi hii.. Wote akili zao zinarudi nyuma, hujui huyu ni Prof. Dkt. Wala Bashite... Wote fix tupu... Hatuna watu makini kwa serikali hii
 
Back
Top Bottom