Jaji Mkuu na Jaji Kiongozi, shughulikieni majipu kwenye Mhimili wenu

Mangi wa Shy

New Member
May 2, 2019
3
2
WanaJF,

Uzi huu ni mahsusi kwa kutoa dukuduku na ushauri juu ya utendaji wa Mhimili wa Mahakama. Napenda niamini kwamba Jaji Mkuu na Jaji Kiongozi, wao wenyewe au kwa kupitia wasaidizi wao, watasoma haya nitakayoandika na ambayo yataandikwa na wengine kwenye uzi huu.

Kwa wale ambao, kwa sababu moja au nyingine, wamewahi kuwa na shauri kwenye mahakama zetu, naamini watakubaliana nami kwamba Mhimili wetu wa Mahakama mara nyingi unasababisha kero kubwa kwa wale wote wanaotafuta haki yao mahakamani.

Kwanza, wengi wanaostahili haki hawapati haki zao, kwa sababu ya kukithiri kwa rushwa kunakopelekea sheria kupindishwa. Pili, mashauri hayasikilizwi na kuamuliwa kwa wakati, licha ya kwamba maamuzi mengi yanaishia kutokutenda haki. Tatu, kupata nakala ya hukumu na mwenendo wa shauri ni awamu nyingine ya kero kwa mwananchi. Watumishi wa masijala wala rushwa wanajua hicho ni kitegauchumi chao. Bila kutoa kitu, mtu atafuatilia hivi vitu hata kwa miezi mitatu!

Mheshimiwa Jaji Mkuu na Mheshimiwa Jaji Kiongozi, uwekeni kwenye rada utendaji kazi wa mahakama zenu zote ili mueze kutuondolea kero sisi wanyonge. Jengeni utamaduni wa kuzitembelea mara kwa mara kanda zote za Mahakama Kuu. Msiishie kusoma reports zilizojaa upotoshaji kutoka kwenye maeneo husika.

Nisingependa kumaliza bila kutoa mfano wa mahakama inayosababisha kero kubwa kwetu sisi wananchi wanyonge na ambayo ninafahamu fika madhaifu yake. Mahakama Kuu Kanda ya Shinyanga, iliyofunguliwa miaka kama mitatu iliyopita, haijaleta kabisa manufaa yaliyotarajiwa. Kila siku ya kazi, Naibu Msajili yuko busy kweli, akiahirisha mashauri mbalimbali, kwa sababu wanazozijua wao wenyewe, kana kwamba wananchi wenye mashauri wana kazi moja tu ya kwenda mahakamani, kama walivyo watumishi wa mahakama. Na kwa bahati mbaya sana, mlitupangia naibu msajili ambaye ni kihiyo wa sheria; sijui hata degree yake ya sheria aliipataje. Inawezekana ya pichu! Ueledi wake pia uko karibu na zero; hana kabisa uwezo wa kujiepusha na mgongano wa maslahi. Msema kweli ni mpenzi wa Mungu; huyu dada yangu, S.P. Mwaiseje, hana sifa hata ya kuwa hakimu wa wilaya (sembuse sifa ya kuwa naibu msajili). Ikiwapendeza wakuu wake wa kazi, mpangieni kazi inayolingana na sifa zake.

Shime shime viongozi wetu, ufanyeni Mhimili wenu kuwa kimbilio letu sisi wananchi wanyonge, sio mahali pakwenda kununua haki au kupatia shinikizo la damu kwa kupokwa haki na wenye uwezo!
 
Umenikumbusha niliwahi fatilia hukumu ya kesi kwa mahakama moja hivi hapa hapa dar, nilikoma aisee mpaka noti zilinitoka ndiyo nikapewa pia kwa kucheleweshwa kiasi
 
Ni shida sana, mkuu! Hakika ni aibu kubwa kwa chombo cha utoaji haki kuwa ndicho kikwazo kikubwa cha upatikanaji wa haki.
 
WanaJF,

Uzi huu ni mahsusi kwa kutoa dukuduku na ushauri juu ya utendaji wa Mhimili wa Mahakama. Napenda niamini kwamba Jaji Mkuu na Jaji Kiongozi, wao wenyewe au kwa kupitia wasaidizi wao, watasoma haya nitakayoandika na ambayo yataandikwa na wengine kwenye uzi huu.

Kwa wale ambao, kwa sababu moja au nyingine, wamewahi kuwa na shauri kwenye mahakama zetu, naamini watakubaliana nami kwamba Mhimili wetu wa Mahakama mara nyingi unasababisha kero kubwa kwa wale wote wanaotafuta haki yao mahakamani.

Kwanza, wengi wanaostahili haki hawapati haki zao, kwa sababu ya kukithiri kwa rushwa kunakopelekea sheria kupindishwa. Pili, mashauri hayasikilizwi na kuamuliwa kwa wakati, licha ya kwamba maamuzi mengi yanaishia kutokutenda haki. Tatu, kupata nakala ya hukumu na mwenendo wa shauri ni awamu nyingine ya kero kwa mwananchi. Watumishi wa masijala wala rushwa wanajua hicho ni kitegauchumi chao. Bila kutoa kitu, mtu atafuatilia hivi vitu hata kwa miezi mitatu!

Mheshimiwa Jaji Mkuu na Mheshimiwa Jaji Kiongozi, uwekeni kwenye rada utendaji kazi wa mahakama zenu zote ili mueze kutuondolea kero sisi wanyonge. Jengeni utamaduni wa kuzitembelea mara kwa mara kanda zote za Mahakama Kuu. Msiishie kusoma reports zilizojaa upotoshaji kutoka kwenye maeneo husika.

Nisingependa kumaliza bila kutoa mfano wa mahakama inayosababisha kero kubwa kwetu sisi wananchi wanyonge na ambayo ninafahamu fika madhaifu yake. Mahakama Kuu Kanda ya Shinyanga, iliyofunguliwa miaka kama mitatu iliyopita, haijaleta kabisa manufaa yaliyotarajiwa. Kila siku ya kazi, Naibu Msajili yuko busy kweli, akiahirisha mashauri mbalimbali, kwa sababu wanazozijua wao wenyewe, kana kwamba wananchi wenye mashauri wana kazi moja tu ya kwenda mahakamani, kama walivyo watumishi wa mahakama. Na kwa bahati mbaya sana, mlitupangia naibu msajili ambaye ni kihiyo wa sheria; sijui hata degree yake ya sheria aliipataje. Inawezekana ya pichu! Ueledi wake pia uko karibu na zero; hana kabisa uwezo wa kujiepusha na mgongano wa maslahi. Msema kweli ni mpenzi wa Mungu; huyu dada yangu, S.P. Mwaiseje, hana sifa hata ya kuwa hakimu wa wilaya (sembuse sifa ya kuwa naibu msajili). Ikiwapendeza wakuu wake wa kazi, mpangieni kazi inayolingana na sifa zake.

Shime shime viongozi wetu, ufanyeni Mhimili wenu kuwa kimbilio letu sisi wananchi wanyonge, sio mahali pakwenda kununua haki au kupatia shinikizo la damu kwa kupokwa haki na wenye uwezo!

My brother, Mangi wa Shy, the malfunctioning of the judiciary system in Tanzania is pandemic. Traverse the country from south to north, from east to west, and you certainly will hear the same familiar song!

...I personally happen to be aware of several civil cases that have been navigating the judiciary system for more than ten years, with no closure in sight. In the circumstances, folks at the age 70+ who decide to seek remedies from a Tanzanian court have to think twice, because they face a real risk of dying before their cases are determined. It’s a harsh reality that their legal representatives may have to inherit their perennial legal battles. Ni urithi wa ajabu, lakini ndiyo uhalisia wenyewe.

I hope wakulu wamesikia kilio chako, kinachofanana na vilio vinavyosikika kila kona ya nchi. Vinginevyo, ni maumivi kwa kwenda mbele.
 
Ndiyo nchi yetu tuliyopewa na Mungu wetu. Hatutaikatia tamaa maadamu kuna uwezekano wa kuibadilisha, hata kama madiliko ni ya mtu mmoja baada ya mwingine.
 
Back
Top Bottom