Jaji Mkuu Masaju nae halijui hili?

Jaji Mkuu Masaju nae halijui hili?

kavulata

JF-Expert Member
Joined
Aug 2, 2012
Posts
16,247
Reaction score
16,169
Kama Jaji na hakimu wakiamua kesi kwa haki na haki imeonekana ikitendeka mbele ya jamii, kazi ya Jaji na hakimu itakuwa kazi kama kazi nyingine tu. Hakuna haja ya hofu kwa majaji.

Ujira mdogo hauathiri utoaji haki kwa majaji na mahakimu tu bali hata kwa wafanyakazi wa fani zote. Huwezi kuwa Jaji na hakimu bila kuwepo kwa mkunga mzuri aliyemzalisha mama vizuri vizuri na kwa moyo ili kupata mtoto mwenye afya ya mwili na akili ambae atakuwa Jaji na hakimu ukubwani. Lakini huwezi kuwapata majaji na mahakimu kama hakutakuwa na walimu wanaofundisha wanafunzi kwa moyo, furaha na uadilifu; wote hawa hawa ni muhimu sana kama walivyo majaji, madakatari, askari, wafanya usafi, wafugaji na wakulima mashambani.

Katika ngazi ya kuwa Jaji Mkuu wa nchi unapaswa kujua kazi zote ni muhimu sana na zinategemeana na zinastahili malipo yenye uwiano fulani. Fedha nyingi lazima pia ziende kwa wakulima kwa njia ya ruzuku ya pembejeo, maji, barabara na masoko kwa wakulima ili wazalishe vyakula vya majaji na mahakimu. Sio kwa majaji tu bali Kila mtu ana wajibu wa kutoa haki kwa anaemhudumia. Mwalimu asiyefundisha vizuri, asiyeeleweka kwa wanafunzi na asiyetoa marks kwa haki kwa wanafunzi wake au anaetoa marks kwa upendeleo/rushwa nae hatendi haki.

Majaji wanatenda kazi ya Mungu kuliko madaktari? nani alipwe zaidi ya mwenzake?

Kila kazi inastahili malipo mazuri ili huduma itolewe kwa haki, hata mzibua mitaro akigoma mahakamani hapatakalika kwa harufu mbaya. Kama Jaji ameamua kesi kwa haki na haki ilionekana ikitendeka mbele ya jamii sidhani kama Jaji huyo ana haja ya kuwa na hofu ya kuumizwa na aliowahukumu.

Huduma nzuri na malipo mazuri ni kama kuku na yai kianze kipi. Huduma nzuri inasababisha ukuaji wa uchumi; na uchumi mkubwa na pesa nyingi zinasababisha utoaji wa huduma nzuri. Hivyo tunachohitaji kama taifa ni usalishaji mkubwa ili tulipane ujira mkubwa wote.

Kazi yenu ya msingi ni kuhakikisha kuwa wanaofuja fedha zetu, wezi na wabadhilifu wanaathibiwa vya kutosha, maana hawa ndio wanaosababisha fedha zisifike kwetu. Pili tuhakikishe kuwa kila mtu anafanyakazi na analipa kodi halali. Kusema majaji na mahakimu hawafanyi kazi kwasababu ya malipo madogo, na kukosa usafiri na nyumba kwenye low density area ni sawa lakini sababu hizo ni cross cutting kwa watumishi na wafanyakazi wote.
 
Jazba kwa jaji mkuu
Kwani jaji mkuu anawakilisha nani? Yeye anawakilisha uamuzi kisheria, na uongozi pamoja ya mahitaji ya mahakimu na majaji. Unataka jaji mkuu aanze kuongelea uchumi? Au wizara ya afya au chama cha walimu?
 
Yeye ni mkuu wa mhimili, sawa na speaker na Rais. Kama kuna madai angeweza kupiga hodi Ikulu kimyakimya kuzungumza na mhimili mwingine (serikali) ofisini, sio hadharani kama vile. Yaani na speaker nae apige kelele kama zile hadharani mbele ya Rais kudai maslahi ya wabunge wake?
 
Kinachonishangazamimi ni kulia lia Kwa jaji ambaye ni mkuu wa mihimili kulialia maslahi makubwa Kwa mihimili mwingine wa urais.Sasa hapo Kuna mihimili kweli?Maana kama ni mihimili unaojitegemea angesema tu kuwa kuanzia Sasa nabadilisha Sheria ili wakili jaji walipwe milioni MIAMOJA Kwa mwezi.Au Huwa tunadanganywa tu kuwa Kuna mihimili mitatu ya Bunge ,mahakama na serikali?
 
Back
Top Bottom