Jaji Mkuu Kushiriki Hukumu ya Lema

Jaji Mkuu Kushiriki Hukumu ya Lema

Khakha

JF-Expert Member
Joined
Jul 15, 2009
Posts
2,981
Reaction score
1,013
wadau wa JF,
Ninasikiliza kipindi cha magazeti cha RFA nimesikia kuwa jaji Chande atasikiliza kesi ya lema akishirikiana na jaji Kimaro na jaji Masati.

kwa hiyo yule mwanafunzi wa open university ndg Mbarouk Mbarouk kapigwa chini.

kumbe Tundu Lisu alisema kweli.

viva CDM!

[TABLE="width: 879"]
[TR]
[/TR]
[TR]
[TD][/TD]
[/TR]
[/TABLE]

na Grace Macha, Arusha

JAJI Mkuu wa Tanzania, Mohamed Chande Othman, ataungana na majaji wa Mahakama ya Rufaa, Natalia Kimaro na Salum Massati, kusikiliza rufaa ya kupinga kuvuliwa ubunge ya aliyekuwa Mbunge wa Jimbo la Arusha Mjini, Godbless Lema (CHADEMA), akichukua nafasi ya Jaji Mbarouk Salim Mbarouk.


Kwa mujibu wa ratiba ya vikao vya mahakama hiyo iliyosainiwa na Naibu Msajili wa Mahakama ya Rufaa, Malewo, ambayo imebandikwa kwenye ubao wa matangazo inaonyesha kuwa mabadiliko hayo yataanza Septemba 20, mpaka mwisho wa vikao hivyo Oktoba mosi mwaka huu.

Kwa upande wake, wakili wa Lema, Method Kimomogoro, alisema atashirikiana na wakili mwenzake Tundu Lissu katika shauri hilo litakalosikilizwa kwa siku moja na kupangiwa tarehe ya kusomwa hukumu, aliongeza kuwa tayari alishaitaarifu mahakama juu ya suala hilo tokea Agosti 28, mwaka huu.


Uamuzi huo wa Lissu kumwakilisha Lema kwenye shauri hilo utamkutanisha mahakamani hapo na kaka yake, Wakili, Alute Mughwai anayewawakilisha wanachama watatu wa Chama cha Mapinduzi (CCM), Mussa Mkanga, Agness Mollel, na Happy Kivuyo, waliofungua shauri lililopelekea kutenguliwa kwa ubunge wa Lema wakidai kuwa wakati wa kampeni mbunge huyo alimdhalilisha mgombea wa CCM, Dk. Batilda Burian, kwa kutumia lugha ya matusi.


Awali Lema kupitia wakili wake, Kimomogoro, aliwasilisha kwenye mahakama hiyo hoja 18 za madai akipinga kutenguliwa kwa ubunge wake na Mahakama Kuu Kanda ya Arusha Aprili 5, mwaka huu.


Kwenye baadhi ya madai hayo, Lema aliiomba Mahakama ya Rufaa kutengua uamuzi wa Mahakama Kuu, uliotengua ubunge wake, huku akiitaka imtangaze kuwa mbunge halali wa Jimbo la Arusha Mjini.


Aidha, aliitaka mahakama hiyo ya juu, iwaamuru walalamikiwa katika shauri hilo walipe gharama za rufaa hiyo pamoja na zile za kesi iliyomalizika kwenye Mahakama Kuu Kanda ya Arusha.


Katika madai mengine, Lema anamlalamikia, Jaji Gabriel Rwakibarila, aliyesikiliza kesi hiyo kuwa alitoa uamuzi wake kwa kuzingatia maneno ya uvumi, huku akipuuza ushahidi uliotolewa mahakamani hapo.


Lema anadai kuwa jaji alikosea wakati alipoamua kuwa mpiga kura yeyote anaruhusiwa kupinga matokeo ya uchaguzi hata kama haki zake za msingi hazijaguswa.


 
Jaji aliyetajwa na Mh. Tindu Lissu kuwa hana shahada ya kwanza na amepewa ujaji kiongozi, ameondolewa kwenye kesi ya rufaa ya mbunge wa Arusha mh. Lema na nafasi yake itachukuliwa na jaji mkuu.
Source: magazeti ya leo.
 
Jaji Mkuu Wa Tanzania, Othman Chande atakuwa mmojawapo katika jopo la majaji watakaoshiriki kupitia na kisha kutoa maamuzi katika rufani ya kesi Na 47/2012 ya aliyekuwa Mbunge wa Arusha Mjini, God bless Lema.
Binafsi sifahamu kushirikishwa kwa Mh.Jaji Mkuu huwa ni hiari yake au inategemeana na uzito wa kesi, au na yeye huwa yumo kwenye roster, lakini huenda kwa shauri hili la Lema ikawa na maana yake maalum!
Lets wait.
 
wadau wa JF,
Ninasikiliza kipindi cha magazeti cha RFA nimesikia kuwa jaji chande atasikiliza kesi ya lema akishirikiana na jaji kimaro na jaji masati. kwa hiyo yule mwanafunzi wa open university ndg mbarouk mbarouk kapigwa chini. kumbe tundu lisu alisema kweli. viva cdm!

CDM huwa hatuongei hoja kwa kukurupuka.Hivyo Tundu Lissu aliongea Kweli ndio maana umeona Serikali imetii hoja ya Lissu.Big up kamanda Lissu kwa Umahiri wa kisheria ulionao.
 
Huyu chizi alishafukuzwa na makopo yake sioni sababu ya kuendelea kumzungumzia.Hata baraza la kata linaweza kusikiliza rufani ya Lema.
 
Kama jaji mkuu yumo, wajitahidi watende haki maana itakuwa aibu ya mwaka kama naye ataingia katika kurudia makosa ya aliyetengua ubunge wa lema!
 
CDM huwa hatuongei hoja kwa kukurupuka.Hivyo Tundu Lissu aliongea Kweli ndio maana umeona Serikali imetii hoja ya Lissu.Big up kamanda Lissu kwa Umahiri wa kisheria ulionao.
Chama Dhaifu kinachagua Viongozi Dhaifu,wanapeana vyeo kama njugu bila kujali uzoefu na shule...wameigeuza Tanzania kuwa na utawala wa kisurtani
 
Huyu chizi alishafukuzwa na makopo yake sioni sababu ya kuendelea kumzungumzia.Hata baraza la kata linaweza kusikiliza rufani ya Lema.

hata ukimwita chizi mapambano yanaendelea chama pinduzi hamna lenu Arusha.m4c ndo habari ya mujini.
 
Jaji Mkuu Augustino Ramadhan? yule aliyepindisha hukumu ya mgombea binafsi kutaka fadhila baada ya kustaafu(makamu mwenyekiti tume ya katiba)
Mh JM Chande hawezi kumuuzi boss wake, Yangu macho
 
Why Jaji mkuu kwenye rufaa ya LEMA? Kesi yake ilikuwa ngumu sana majaji wengine kushindwa?, au kutakuwa na utashi wa siasa ndani yake?
 
Maybe there's something cooking on. Let's wait and see. Frankly writing tundu lissu is the man to watch... I mean he's man of the match.
 
Tundu Lissu ni kiboko ni kati ya wanasheria wachache sana duniani ambao sio waoga aliwachana live kitu ambacho kwa upande wa ccm hawakiwezi kabisa
 
Ikitokea yule Jaji anayetokea pande za Pinda alitoa hukumu kishabiki Jaji Mkuu atapendekeza awajibishwe, ama atatoa maamuzi mwenyewe?
Bonga bana!
 
Chama Dhaifu kinachagua Viongozi Dhaifu,wanapeana vyeo kama njugu bila kujali uzoefu na shule...wameigeuza Tanzania kuwa na utawala wa kisurtani


Naye akichemka kwa kuelemea kwenye ukada badala ya weledi basi ajiandae kuingia katika historia ya majaji wabovu kuwahi kujiri!!!!!!!
 
hili swala lipo mahakamani lisijadiliwe- ha! ha! ha!ha! ha! ha!ha! ha! ha!
 
Huyu chizi alishafukuzwa na makopo yake sioni sababu ya kuendelea kumzungumzia.Hata baraza la kata linaweza kusikiliza rufani ya Lema.

Umetumia jazba zaidi matokeo yake hujaeleweka unamzungumzia nani ni chizi, Mbarouk, jaji kiongozi, Lisu, au Lema?
 
Turejeshee mbunge wetu wa arusha province..huyu chande c ndo kapenyeza jina The Hague akapigwa chini na Mbeijing wa Gabon? Kuna kazi hapa,ila mungu anatuambia kuwa We will never walk alone.
 
Sorry wanabodi hivi hukumu yenyewe itasomwa lini wish u allthe best bro Lema
 
Back
Top Bottom