Jaji mkuu hawaamini watendaji wake au ......? | JamiiForums | The Home of Great Thinkers

Dismiss Notice
You are browsing this site as a guest. It takes 2 minutes to CREATE AN ACCOUNT and less than 1 minute to LOGIN

Jaji mkuu hawaamini watendaji wake au ......?

Discussion in 'Jukwaa la Siasa' started by Nuru John, Nov 23, 2010.

 1. N

  Nuru John Member

  #1
  Nov 23, 2010
  Joined: Aug 26, 2009
  Messages: 15
  Likes Received: 0
  Trophy Points: 0
  Jaji Mkuu Augustino Ramadhani ameamua kuingilia kati kesi ya wastaafu wa iliyokuwa Jumuiya ya Africa Mashariki (EAC) kwa ajili ya kulifanyia mapitio ili kujiridhisha kuwa Mhe Jaji wa Mahakama Kuu aliyeisikiliza kesi hii,alizingatia mwenendo wa shauri na ushahidi wa kesi uliokuwa mbele yake na pia alizingatia sheria husika.

  Kasambaza barua sehemu kibao mpaka Ubalozi wa Marekani na Uingereza,sijui kazipeleka huko kufanya nini labda kuna maslahi.

  Mimi hapo napata maswali mengi sana yasiyokuwa na jibu sahihi kutoka kwangu mwenyewe na ndio maana nimeamua kuwauliza Great Thinkers of JF kunisaidia kuyajibu kama si kunielewesha ili nipate ufahamu.

  • Inamaana Jaji Mkuu hawaamini watendaji wake au..?
  • Kama jibu ni ndio,sisi wananchi wa kawaida anatuletea ujumbe gani kuhusu hao watendaji wake wa Mhimili mmoja wapo wa nchi?INATISHA SANA
  • Je huo ndio utaratibu yeye kuita faili na kulipitia kabla ya wahusika kufuata sheria ya kukata rufaa?
  • Nini hasa kilichomsukuma kuitisha faili la kesi ya wastaafu na kuacha mafaili mengine lukuki yanayoozea mahakamani bila kufanyiwa kazi kwa wakati?
  • Wakitokea watu wengine wenye kesi wakimuomba apitie hukumu za kesi zao atakuwa yuko tayari?
  Maswali mengine muyaongeze wenyewe kama mnayo.

  Hii nchi inakwenda wapi sasa?Jaji Mkuu amejiweka pabaya kama si kwenye mtego wa panya.
  Au siasa zimekwishaingia humo ndani....????

  Nisaidieni ndugu zangu kabla sijaanza kupoteza imani na mhimili huu.
   
Loading...