Jaji Mkuu apinga mjadala mgombea binafsi

Ngongo

JF-Expert Member
Sep 20, 2008
18,923
31,166
Jaji Mkuu, Augustine Ramadhani, amesema uamuzi wa Mahakama Kuu kuruhusu kuwapo mgombea binafsi katika uchaguzi wa kisiasa nchini, haupaswi kujadiliwa hivi sasa.

Amesema haupaswi kujadiliwa kwa vile unasubiri uamuzi wa Mahakama ya Rufani kutokana na serikali kuwasilisha maombi kuomba ipewe kibali cha kutoa taarifa ya kusudio lake la kutaka kukata rufani kupinga uamuzi huo.

Amesema kujadili hivi sasa, kutazuia kusudio la serikali na vile vile kutaingilia uamuzi unaotarajiwa kutolewa na Mahakama ya Rufani kuhusiana na maombi ya serikali.

Jaji Ramadhani aliyasema hayo Ijumaa iliyopita alipotakiwa na Nipashe kutoa maoni yake kuhusu kauli ya Waziri wa Sheria na Katiba, Mathias Chikawe, kwamba, serikali haikubaliani na uamuzi huo wa Mahakama Kuu kwa vile umefuta baadhi ya vifungu vya Katiba ya nchi, kinyume na taratibu.

Hata alipotakiwa kueleza kama Mahakama inao uwezo kisheria wa kufuta kifungu chochote cha Katiba ya nchi, Jaji Ramadhani alisema ``siwezi kutoa maoni yangu kwa hilo, nitazuia rufani, tungojee uamuzi. Kwa hiyo, we tusubiri.``

Chikawe alikaririwa na Nipashe akisema kwamba, msimamo wa serikali wa kupinga uamuzi wa Mahakama Kuu kuruhusu kuwapo mgombea binafsi katika uchaguzi wa kisiasa nchini, bado uko pale pale kwa vile suala hilo limehusisha kufutwa kwa vifungu vya Katiba ya nchi, kinyume na taratibu.

Awali, katika hukumu ya Mahakama Kuu iliamriwa Ofisi ya Mwanasheria Mkuu kufanya marekebisho ya Sheria Namba 34 ya 1994 ambayo inapingana na kifungu cha 21 (1) cha Katiba ambacho kinampa haki ya kugombea na kupiga kura.

Mahakama Kuu ilimpa Mwanasheria Mkuu kati ya Mei 5, 2006 hadi uchaguzi ujao awe amewasilisha bungeni sheria inayotoa fursa ya kuwapo mgombea binafsi katika uchaguzi bila kutegemea chama chochote.

Kutokana na uamuzi huo wa Mahakama Kuu uliotolewa na majaji Amir Manento, Salum Massati na Thomas Mihayo, serikali ilikata rufaa ambapo inadai Mahakama Kuu ilikosea kisheria katika kutafsiri Ibara ya 21 (1) ( c ), 39 (1) (c ) (b) na 69 (1) (b) ya Katiba ya Jamhuri ya Muungano wa Tanzania kinachompa haki mtu ya kugombea na kupiga kura.

Majaji watatu wa Mahakama ya Rufaa walitoa hukumu ya kutupilia mbali rufaa ya serikali, hali iliyompa ushindi tena Mwenyekiti wa Democratic Party, (DP), Christopher Mtikila, ambaye amekuwa anahangaikia kuruhusiwa mgombea binafsi tangu mwaka 1993.

Mtikila baada ya kubaini kuwa kuna kasoro katika rufani ya serikali, aliwasilisha pingamizi mahakamani hapo akidai kuwa ina kasoro kutokana na tarehe iliyoko kwenye amri ya hukumu kuwa tofauti na tarehe iliyoko kwenye hukumu ya Mahakama Kuu.

Katika pingamizi hilo, Mtikila kupitia kwa mawakili wake, Richard Rweyongeza na Mpale Mpoki, waliliambia jopo la majaji hao kuwa rufaa hiyo haikuwa na rutuba ya kisheria kutokana na dosari hizo za tarehe tofauti kwenye amri na kwenye hukumu ya mahakama hivyo wakaiomba mahakama kukataa kusikiliza rufani hiyo.

Majaji walikubaliana na hoja za mawakili wa Mtikila wakisema kuwa amri hiyo (kikaza hukumu) ilikuwa hairekebishiki kwa kuwa ilitengenezwa Februari mosi mwaka juzi wakati hukumu ya Mahakama Kuu juu ya suala hilo ilitolewa Mei 5, 2006.

Wanasheria Waandamizi, Joseph Ndunguru na Mathew Mwaimu waliokuwa wanaiwakilisha Ofisi ya Mwanasheria Mkuu, waliiomba mahakama kukataa pingamizi hilo la Mtikila kwa vile suala hilo liliwasilishwa Mahakama Kuu chini ya sheria za haki za binadamu ambayo haihitaji kuwasilisha amri ya hukumu.

Kwa mujibu wa wanasheria hao, kilichokuwa kinabishaniwa siyo agizo la hukumu, bali maamuzi ya mahakama nyingine kwa hiyo hapakuwapo na sheria inayotaka tarehe iliyoko katika amri ya hukumu iwe sawasawa na ile iliyoko katika hukumu kama sheria inavyoelekeza kwenye agizo la hukumu.

Majaji kwa upande wao walisema maamuzi kama hayo yanaendana na sheria za mwenendo wa kesi za madai zinazohitaji amri ya hukumu yoyote ionyeshe tarehe inayofanana na ile iliyoko kwenye hukumu.

Mtikila alifungua kesi hiyo Februari 17, 2005 akiiomba mahakama kutamka kuwa ni kinyume cha Katiba ya nchi kupinga kuwapo kwa mgombea binafsi katika nafasi za kisiasa.

Katika uamuzi wa Mahakama Kuu, jopo la majaji watatu liliruhusu kuwapo kwa mgombea binafsi katika uchaguzi, kwa sababu katiba ya nchi inatoa haki hiyo.

Majaji hao walibainisha kuwa katiba inatamka wazi kuwa kila mwananchi anayo haki ya kuchagua au kuchaguliwa kuwa kiongozi na haiweki masharti kuwa hilo lifanyike kwa mtu kujiunga na chama fulani.

Mwaka 1993, Mtikila alishinda kesi kama hiyo katika Mahakama Kuu Kanda ya Dodoma, lakini licha ya uamuzi huo wa mahakama, Bunge lilishindwa kutunga sheria ya kuruhusu mgombea binafsi na ndipo Mtikila alifungua kesi hiyo ya kikatiba Mahakama Kuu Kanda ya Dar es Salaam na kushinda tena.


SOURCE: Nipashe
 
Je tuna anza kuona fadhila zinalipwa kidogo kidogo baada ya teuzi hizi ama aliyo yasema yana ukweli wowote ?Wacha tuone kama kweli teuzi zinazo lalamikiwa basi wanao lalama wana makosa .
 
Naweza kuona kwa nini Serkali inapinga. Kwa sababu hoja imetolewa na Mtikila. Huyu Mtikila ni troublemaker,mvunja sheria,ambaye amefungwa mara nyingi. Hastahili kabisa kuuteka nyara mjadala huu wa mgombea binafsi. Ili hili swala hili lipate hearing inabidi lipendekezwe na mtu wa heshima,siyo Mtikila,mtu ambaye hata hivi sasa anazo kesi nyingi Mahakamani. Kwa ajili wanayo tabia Mahakamani kwamba mtu akienda kule na complaints,hawamfukuzi. Ndiyo maana watu kama Mtikila wanalisumbua Taifa. Kwa kifupi,Mtikila ajitoe katika hiyo kesi,ili hilo swala lichukuliwe na mtu mwingine,mtu ambaye anaheshimiwa na wananchi,siyo mtu ambaye anakwenda kugombea Ubunge,halafu haambulii chochote,isipokuwa kupopolewa na mawe.
 
Naweza kuona kwa nini Serkali inapinga. Kwa sababu hoja imetolewa na Mtikila. Huyu Mtikila ni troublemaker,mvunja sheria,ambaye amefungwa mara nyingi. Hastahili kabisa kuuteka nyara mjadala huu wa mgombea binafsi. Ili hili swala hili lipate hearing inabidi lipendekezwe na mtu wa heshima,siyo Mtikila,mtu ambaye hata hivi sasa anazo kesi nyingi Mahakamani. Kwa ajili wanayo tabia Mahakamani kwamba mtu akienda kule na complaints,hawamfukuzi. Ndiyo maana watu kama Mtikila wanalisumbua Taifa. Kwa kifupi,Mtikila ajitoe katika hiyo kesi,ili hilo swala lichukuliwe na mtu mwingine,mtu ambaye anaheshimiwa na wananchi,siyo mtu ambaye anakwenda kugombea Ubunge,halafu haambulii chochote,isipokuwa kupopolewa na mawe.

Mkuu Ganesh, sijakuelewa kabisa. Naomba unieleweshe. Ina maana Mtikila hana haki ya kufungua mashitaka kama hayo ama vipi? Najaribu kutafakari unachotaka kukisema tu Mkuu. Nadhani sheria na Katiba zinatoa haki kwa mtu yeyote kufungua mashitaka kama hayo.

Kuhusu usumbufu wa Mtikila, sijui kama nimeuona katika maelezo yaliyotangulia. Nilichokiona/kushuhudia ni uhodari, ushupavu wake kuamua kutetea haki ya kila Mtanzania kuchagua au kuchaguliwa bila kuwekewa pingamizi kutokana na kuwa au kutokuwa na uwakilishi wa chama cha siasa.

Inaweza ukafika wakati waTanzania wote wenye kutaka kupiga kura kuwa kwanza wanachama wa vyama vya siasa. Sijui kama hiyo itakuwa Demokrasia sahihi. Maana kama kuchaguliwa ni lazima uwe na chama, kwanini kuchagua pia usiwe na chama?
 
Ganesh mkuu heshima mbele. Naona tatizo lako katika hoja hii ni " Nani "amefungua kesi na si" Kesi " iliyofunguliwa inahusu nini? Kwa mtazamo
 
Last edited:
Back
Top Bottom