Imekuwa kama ni mtindo wa aina fulani kwa Polisi kuwakamata watuhumiwa, kwa kificho bila kutoa vitambulisho na kueleza madhumuni ya kumkamata mtuhumiwa
Inajulikana wazi kuwa kanuni za Jeshi la Polisi, zinawataka wao kabla ya kumkamata mtuhumiwa yeyote kwa kosa lolote la jinai, lazima wafuate kanuni zifuatazo:-
1. Kujitambulisha na watoe vitambulisho vya kazi vinavyoonyesha majina halisi ya maaskari hao
2. Kutoa fursa kwa mtuhumiwa kuwa na wakili wake, wakati wa mahojiano na Polisi hao
3. Kueleza ni kosa gani wanalomkamata nalo mtuhumiwa huyo
4. Kueleza,kuwa ni kituo gani cha Polisi wanampeleka mtuhumiwa huyo
Kwa Bahati mbaya sana hizo kanuni zote za Jeshi la Polisi hazikifuatwa wakati wa kuwakamata watuhumiwa Eric Kabendera na Tito Magoti
Mbaya zaidi wakati wa kumkamata Eric Kabendera askari hao walieleza kuwa wamemkamata kwa ajili ya kutaka kumuhoji utata wa uraia wake.
Lakini cha kushangaza sana ni kuwa wakati wanamfikisha mahakamani "walimgeuzia" kibao na kuyapindia mashitaka hayo na kuyaweka mashitaka "mapya" ya utakatishaji pesa na uhujumu uchumi
Kitu ambacho askari hao wanafanya "ukatili" wa hali ya juu, ni kwa kuwa mashitaka hayo hayana dhamana, basi hao askari ni kupiga "danadana" na kudai kuwa ushahidi haujakamilika kwa zaidi ya miezi sifa sasa!
Imaeleweka pia.ndani ya sheria kuwa mtuhumiwa bado anakuwa ni "innocent person" hadi pale mahakama imtie hatiani, kwa maana hiyo hiki kinachoendelea sasa naeeza kukiita kuwa ni "justice delayed is justice denied"
Kutokana na mazingira hayo ningependa kuuliza swali lifiatalo kwa mhimili wa mahakama, ni kwanini hawazitipilii mbali kesi zote zinazoletwa mahakamani zikiwa hazijakamika ushahidi wake na askari wanaendekea kuziahirisha kila inapofika mahakamani kwa kudai kuwa ushahidi haujakamilika?