Jaji Mkuu achukizwa na wapelelezi wanaokamata mtuhumiwa kabla ya kukamilisha upelelezi

Lakini pia nadhani sio lazima kila hoja inayo wasilishwa mahakamani na wapelelezi hakimu akubliane nayo... Hivi mtu umetuhumiwa kwa kosa la kutoa mimba lakini charge sheet ina wekwa uhujumu uchumi na utkatishaji pesa bado hakimu ana funga dhamana?? Is this fair??
Maoni binafsi usiyashabihishe na uraia wa mtu. Gharama za kumtunza 'mtuhumiwa' huko mahabusu nani anazibeba? Niko pale pale...haraka ya nini kama upepelezi haujakamilika?

Sent using Jamii Forums mobile app
 
Mwanasheria mkuu,DPP,Jaji Mkuu wanayo nafasi kubwa Sana kama wataamua kwa nia ya dhati kupunguza idadi ya mahabusu magerezani waagize tu watendaji wao kama ushahidi haujakamilika watuhumiwa wote wapewe dhamana na kurudishwa mahakamani ni hadi ushahidi ukamilike kwanza na mtu akipelekwa mahakamani ni kwa ajili ya hukumu tu na sio vingine,haya mambo ya kila siku watu wanapelekwa mahakamani kisha wanasomewa tu na kurudishwa tena mahabusu eti ushahidi aujakamilika sasa kama aujakamilika mnawapelekea nn mahakamani kuuza sura au.Twende kisomi zaidi.
 
Upelelezi haujakamilika ni uvunjifu mkubwa na ukatili Wa hali ya juu dhidi ya binadamu.Mahabusu kuna kesi uchwara nyingi Sana ambazo kama tungeacha uzamani tungepunguza idadi isiyo ya lazima ya mahabusu wanaokula kodi zetu bure ambayo ingewezasaidia kwenye ujenzi wa vyoo vya shule zetu.
 
Upelelezi haujakamilika ni uvunjifu mkubwa na ukatili Wa hali ya juu dhidi ya binadamu.Mahabusu kuna kesi uchwara nyingi Sana ambazo kama tungeacha uzamani tungepunguza idadi isiyo ya lazima ya mahabusu wanaokula kodi zetu bure ambayo ingewezasaidia kwenye ujenzi wa vyoo vya shule zetu.
Tuna Jaji Mkuu wa nchi ya Tanzania ambaye ni kituko. Itakuwaje uwe na nafasi hiyo usijue nguvu ulizo nazo. Analalamika tu kama mwananchi wa kawaida
 
Kwa nn wapo wanawapokea watuhumiwa kama upelelezi haujakamilika,tatizo liko mahakamani siku mahakama ikiamua kutowapokea watu ambao upelelezi haujakamilika na kuwaachia huru basi polisi wataacha huo mchezo

Sent using Jamii Forums mobile app
 
Imekuwa kama ni mtindo wa aina fulani kwa Polisi kuwakamata watuhumiwa, kwa kificho bila kutoa vitambulisho na kueleza madhumuni ya kumkamata mtuhumiwa

Inajulikana wazi kuwa kanuni za Jeshi la Polisi, zinawataka wao kabla ya kumkamata mtuhumiwa yeyote kwa kosa lolote la jinai, lazima wafuate kanuni zifuatazo:-

1. Kujitambulisha na watoe vitambulisho vya kazi vinavyoonyesha majina halisi ya maaskari hao

2. Kutoa fursa kwa mtuhumiwa kuwa na wakili wake, wakati wa mahojiano na Polisi hao

3. Kueleza ni kosa gani wanalomkamata nalo mtuhumiwa huyo

4. Kueleza,kuwa ni kituo gani cha Polisi wanampeleka mtuhumiwa huyo

Kwa Bahati mbaya sana hizo kanuni zote za Jeshi la Polisi hazikifuatwa wakati wa kuwakamata watuhumiwa Eric Kabendera na Tito Magoti

Mbaya zaidi wakati wa kumkamata Eric Kabendera askari hao walieleza kuwa wamemkamata kwa ajili ya kutaka kumuhoji utata wa uraia wake.

Lakini cha kushangaza sana ni kuwa wakati wanamfikisha mahakamani "walimgeuzia" kibao na kuyapindia mashitaka hayo na kuyaweka mashitaka "mapya" ya utakatishaji pesa na uhujumu uchumi

Kitu ambacho askari hao wanafanya "ukatili" wa hali ya juu, ni kwa kuwa mashitaka hayo hayana dhamana, basi hao askari ni kupiga "danadana" na kudai kuwa ushahidi haujakamilika kwa zaidi ya miezi sifa sasa!

Imaeleweka pia.ndani ya sheria kuwa mtuhumiwa bado anakuwa ni "innocent person" hadi pale mahakama imtie hatiani, kwa maana hiyo hiki kinachoendelea sasa naeeza kukiita kuwa ni "justice delayed is justice denied"

Kutokana na mazingira hayo ningependa kuuliza swali lifiatalo kwa mhimili wa mahakama, ni kwanini hawazitipilii mbali kesi zote zinazoletwa mahakamani zikiwa hazijakamika ushahidi wake na askari wanaendekea kuziahirisha kila inapofika mahakamani kwa kudai kuwa ushahidi haujakamilika?
 
Bahati hili siala ameliongelea Jaji Mkuu, Profesa Ibrahim Juma na kutoa onyo kwa askari kutopeleka kesi ambazo upelelezi wake haujakamilika

Ninashangaa ni kwa vipi kesi ya Eric Kabendera iendelee huku maaskari hao wakidai kuwa upelelezi bado haujakamilika, huku wakimpuuza Jaji Mkuu kutokana na kauli yake!
 
14 Reactions
Reply
Back
Top Bottom