Jaji Makame aahidi uchaguzi huru - KUNA JIPYA? | JamiiForums | The Home of Great Thinkers

Dismiss Notice
You are browsing this site as a guest. It takes 2 minutes to CREATE AN ACCOUNT and less than 1 minute to LOGIN

Jaji Makame aahidi uchaguzi huru - KUNA JIPYA?

Discussion in 'Habari na Hoja mchanganyiko' started by Kidudu Mtu, Dec 15, 2009.

 1. Kidudu Mtu

  Kidudu Mtu Member

  #1
  Dec 15, 2009
  Joined: Nov 7, 2009
  Messages: 66
  Likes Received: 0
  Trophy Points: 0
  Mwenyekiti wa Tume ya Taifa ya Uchaguzi, Jaji mstaafu, Lewis Makame (pichani), amesema hivi sasa inajadili majukumu ya kuandaa uchaguzi mkuu wa mwakani, uweze kufanyika kwa uwazi, uhuru na haki kwenye mazingira ya usalama na utulivu zaidi.
  Jaji Makame alisema miongoni mwa wadau katika zoezi la uchaguzi ni vyombo vya ulinzi na usalama ambavyo vitahakikisha utulivu unakuwepo.
  Pia, alitaka polisi kutokuwa la itikadi kwenye utendaji wake na kutokuwa mashabiki wa kisiasa.
  "Kama mnavyojua kwa mujibu wa ibara ya 147(3) na (4) ya Katiba ya Jamhuri ya Muungano wa Tanzania ya Mwaka 1977 ni marufuku kwa mwanajeshi yeyote kujiunga na chama cha siasa,” alisisitiza
  Alisema kuendesha uchaguzi wa kidemokrasia ni lazima pawepo sheria, kanuni na taratibu zinazoelezwa na kuwekwa wazi ili wadau wote wanaoshiriki waweze kuzifahamu na kushiriki kikamilifu.
  CHANZO: NIPASHE
  ............................................................................

  Huwa nashindwa kuelewa hawa wasomi na wazoefu inakuwaje wasiwe na uwezo wa kutafakari na kusaidia katika masuala muhimu kwa mustakabali wa taifa, au ili mradi wao wanapata mlo wao wa kila siku inatosha! Inawezekana kwa kuwa wanapewa nyadhifa baada ya "kustaafu", kwao vyeo hivi vinakuwa ni fadhila na si dhamana.

  Inawezekana vipi kuwepo na uchaguzi huru wakati:


  • Hakuna tume huru ya uchaguzi
  • Hakuna mazingira sawa ya ushindani kati ya wagombea na vyama
  • Katiba inaipa mamlaka ya juu zaidi tume ya uchaguzi kuweza kuamua nani awe Rais
  • .....
  • ....nk...nk
   
 2. J

  Jasusi JF-Expert Member

  #2
  Dec 15, 2009
  Joined: May 5, 2006
  Messages: 11,484
  Likes Received: 165
  Trophy Points: 160
  Tunahitaji tume mpya ya uchaguzi chini ya uongozi mpya. Wenzetu Wakenya walishalitambua hilo na wameshalifanyia kazi.
   
 3. Bluray

  Bluray JF-Expert Member

  #3
  Dec 15, 2009
  Joined: Mar 25, 2008
  Messages: 3,446
  Likes Received: 31
  Trophy Points: 135
  Jaji Makame hivi after Zanzibar 95 wewe una haiba hata robo ratili ya kujishaua mbele ya watu wajuao kilichoendelea kwamba unaweza hata kutamka maneno "uchaguzi huru" kwa roho nyeupe ?
   
 4. Mag3

  Mag3 JF-Expert Member

  #4
  Dec 15, 2009
  Joined: May 31, 2008
  Messages: 9,094
  Likes Received: 6,188
  Trophy Points: 280
  Atalitakaje jeshi la polisi kutokuwa la itikadi kwenye utendaji wake na kutokuwa mashabiki wa kisiasa wakati yeye mwenyewe utendaji wake umegubikwa na itikadi na ushabiki wa kisiasa ? Mikono ya Jaji Makame ina damu ya wananchi waliopoteza maisha wakipinga utendaji wake na kudai uchaguzi huru na wa haki.
   
 5. Jethro

  Jethro JF-Expert Member

  #5
  Dec 15, 2009
  Joined: Mar 23, 2009
  Messages: 2,223
  Likes Received: 98
  Trophy Points: 145
  Teh teh amakweli sie ni wadanganyika duh ni mara ngapi hawa askali wanakuwa mstari wa mbele kulinda maslahi ya Chama kilichoko madarakani kwa kujidanganya ati CCM ikitoka wakija wengine hampati kitu ni fikra mbovu na ufinyo mdogo wa viongozi wa kitanzania.

  Viongozi wakubwa ndani ya police ndio wao wa kwanza kuwasisitiza police wenye vyeo vidogo kuahaikisha CCM inashinda na kuilinda mambo yao yafanyike.

  Yani siku inchi hii ika gombolewa upya na vizazi vijavyo watatuhukumu vibaya kwa wale watakao kuwepo hawato tizama makunyanzi oooh wewe ulileta mambo fulani kumbe huku nyuma yake ulivurunda na tutapigwa ndani mbaya subilini au tuombe tufe mapema hayo yasitukute. eg mfano mzuri ni Chile Augustino Pinoche at the Age of 80's aliwekwa chini ya ulizi pale alipo toka chile kwenda Uk kutibiwa tu mahakamani kwa mapinduzi aliyo yafanya kule Chile na pamoja alikuza uchumi wa nchi ile na iko vyema kimaendeleo na kiuchumi.

   
 6. Ustaadh

  Ustaadh JF-Expert Member

  #6
  Dec 16, 2009
  Joined: Oct 25, 2009
  Messages: 413
  Likes Received: 7
  Trophy Points: 0
  Debe tupu.................
   
Loading...