Jaji Kiongozi:Askari Polisi wanabambika raia kesi

MziziMkavu

MziziMkavu

JF-Expert Member
Joined
Feb 3, 2009
Messages
40,028
Likes
5,492
Points
280
MziziMkavu

MziziMkavu

JF-Expert Member
Joined Feb 3, 2009
40,028 5,492 280

Inspekta Jenerali (IGP), Said Mwema.Jaji Kiongozi, Fakihi Jundu, amewashutumu polisi nchini kwa kuendelea na tabia ya kuwabambikizia kesi raia na kuchelewesha upelelezi wa kesi zao licha ya Inspekta Jenerali (IGP), Said Mwema, kukemea vitendo hivyo.
Aidha, amemshauri Mkurugenzi wa Mashitaka (DPP), kufuta kesi ambazo zinaonekana hazina haja ya kuendelea hata kama zinahusu tuhuma za unyang'anyi wa kutumia silaha.
Jaji Kiongozi alitoa kauli hiyo juzi wakati akizungumza na waandishi wa habari jijini Dar es Salaam mara baada ya kumaliza ziara yake ya kukagua baadhi ya mahakama zilizopo katika Wilaya ya Kibaha, mkoani Pwani.
Alikuwa akizungumzia msongamano wa mahabusu katika baadhi ya magereza nchini, hali aliyosema kuwa inachangiwa na Jeshi la Polisi pamoja na maamuzi ya mahakama ambayo wakati mwingine yamekuwa yakichangia kutokea kwa hali hiyo.
“Tatizo hilo la kubambikiziwa kesi lipo katika magereza mengi, kila nilipotembelea nimeongea na ma-RCO (Maofisa Upelelezi wa Makosa ya Jinai wa Mikoa). Mara nyingine kesi hizo haziendi miaka 4 hadi 5 makosa hayana dhamana, nakumbuka IGP alitoa mapendekezo kwa polisi lakini hawajayafanyia kazi,” alisema na kuongeza:
“Mimi sipendezewi ndo maana magereza zinafurika, kama mtu akifanya kosa kwa nini hapewi kosa lake lile lile, anabadilishwa. Hayo nimeyakuta magerezani nilipotembelea.”
Alisema tabia ya kutengeneza kesi inamnyima haki mshtakiwa na kujikuta akipewa hukumu isiyostahili. “Mfano, kukopeshana kwa akinamama polisi anatengeneza shtaka la jinai badala ya madai, nilitembelea gereza moja mama mjamzito aliwekwa ndani na kufungwa miaka mitano kwa deni la Sh. 60,000 hadi akajifungua akiwa gerezani,” alisema na kuongeza:
“Jamani ujauzito ulikuwa unajionyesha, lakini hakimu wa wilaya angeweza kufanya mapitio ya kumtoa yule mama, rabsharabsha zangu mimi kwa hakimu wa wilaya ndo zimemsaidia yule mama kutendewa haki.”
Jaji Jundu alisema watoto wadogo ambao wanastahili adhabu ya kuchapwa viboko wanapelekwa magerezani na kusababisha msongamano.
Alisema ni jambo la kawaida kuwepo na makosa hayo, lakini inashangaza upelelezi haukamiliki kila kukicha licha ya kufanyika kwa mazungumzo na wadau na polisi kutakiwa kuuharakisha.
“Kesi zisizo na ufumbuzi hazina haja ya kuendelea nazo, upelelezi wa kesi miaka mitano mtu yupo ndani miaka mitano upelekezi haujakamilika. Polisi waliangalie hilo hata kama ni uhalifu wa kutumia silaha,” alisema.
Jaji Kiongozi alisema kuwa polisi wangejipa muda wa mwisho wa kukamilisha upelelezi yote yasingetokea.
Hata hivyo, alisema mwenye mamlaka ya kuondoa mashtaka hayo ni DPP, lakini upelelezi unashikiliwa na polisi.
Alisifu baadhi ya mahakimu wenye msimamo kwenye maamuzi yao ya kimahakama kwa kuziondoa kesi zisizo za mwelekeo licha ya upande wa mashtaka kutoa visingizio kuwa upelekezi bado haujakamilika kwa muda mrefu.
Katika hatua nyingine alizitaka mahakama kutoa masharti nafuu kwa ajili ya dhamana ili kupunguza msongamano huo isipokuwa tu pale sheria inapobana katika kutoa maamuzi hayo.
“Adhabu zinachangia msongamano, sio kila siku kutoa vifungu, unao uhuru wa kutoa adhabu mbadala,” alisema.
Aidha, aliwataka mahakimu wa mahakama za mwanzo waache utata katika uendeshaji wa mashauri ya mirathi kwa kujipa majukumu ya ugawaji wa mali za marehemu na wao kujipa mafungu yao.
“Kazi yenu ni usimamizi, utakuta hakimu anajiingiza katika ugawaji wa mali za marehemu hivyo wenye haki yao wanaikosa wanapewa wasio na uhusiano na marehemu na yanatokea malalamiko makubwa. Tusiende nyuma ya sheria tufuatae taratibu za kisheria,”alisema Jaji Jundu.
Aliwataka mahakimu kila mwezi kuweka ratiba ya kutembelea magereza na kujua malalamiko ya wafungwa ili kamati za kusukuma kesi ziweze kuyafanyia kazi malalamiko hayo kwa kuhakikisha kuwa kila mwezi watu 15 kati ya 20 waliopo gerezani wanatoka ili msongamano uweze kupungua.
CHANZO: NIPASHE
 
TingTing

TingTing

Member
Joined
Dec 20, 2009
Messages
93
Likes
2
Points
0
TingTing

TingTing

Member
Joined Dec 20, 2009
93 2 0

Ni vyema kukapitishwa muda wa uchunguzi ili polisi wafanye kazi kwa kuzingatia muda. Kukomoana hakusaidii jamii wala yule mwenye nia ya kumkomoa mwenzake. Hizi ni ishara za uadui na kwa mtindo huu basi itafikia kipindi wananchi watakuwa hawana imani na polisi kabisa na badala yake kuchukua sheria mkononi. (Haya ni mawazo yangu tu)
 
Forum statistics

Threads 1,275,205
Members 490,931
Posts 30,535,694