Jaji Bomani azilipua Kampuni za madini | JamiiForums | The Home of Great Thinkers

Dismiss Notice
You are browsing this site as a guest. It takes 2 minutes to CREATE AN ACCOUNT and less than 1 minute to LOGIN

Jaji Bomani azilipua Kampuni za madini

Discussion in 'Jukwaa la Sheria (The Law Forum)' started by BAK, Apr 20, 2011.

 1. BAK

  BAK JF-Expert Member

  #1
  Apr 20, 2011
  Joined: Feb 11, 2007
  Messages: 70,418
  Likes Received: 81,463
  Trophy Points: 280
  Jaji Bomani azilipua Kampuni za madini Tuesday, 19 April 2011 09:31

  Ramadhan Semtawa
  Mwananchi

  MWANASHERIA Mkuu Mstaafu Jaji Mark Bomani, amezitaka kampuni za madini nchini kuwekeza asilimia 50 ya mapato yao ya fedha za kigeni kwenye benki za ndani ili kunusuru shilingi.

  Kauli hiyo ya Jaji Bomani ambaye aliwahi kuongoza Kamati ya Rais ya Kudurusu mikataba ya madini, inakuja kipindi ambacho maliasili hiyo imetajwa kutonufaisha nchi kichumi kutokana na Sheria ya Madini ya 1998 inayotoza mrahaba wa asilimia tatu.

  Akizungumza katika mahojiano maalumu ofisini kwake wiki iliyopita, Jaji Bomani alisema tayari amefikisha hoja hiyo kwa wadau husika baada ya kuona utajiri wa madini haunufaishi nchi kwa kiasi kikubwa.

  Bomani alisema thamani ya shilingi dhidi ya fedha za kigeni inazidi kushuka na kuongeza, "sasa hivi thamani ya dola moja ya Marekani ni sawa na takribani Sh1,500."

  Alisisitiza kwamba fedha za kigeni zinazoingia nchini hazitoshi ikilinganishwa na mahitaji ya nchi na wananchi wake na kuweka bayana, hiyo inatokana na kuwepo kwa mianya mingi.

  Mikataba ya madini
  "Mojawapo ya mianya hiyo ni ruhusa iliyotolewa na serikali kwa Kampuni za madini ya dhahabu kutorejesha nchini fedha zinazotokana na mauzo ya dhahabu nje. Miaka ya 1990 serikali ilitiliana saini na kampuni kadhaa za madini, mikataba ambayo ilizipa ruksa kampuni hizo ya kutorejesha nchini fedha zao za mauzo ya kigeni," alifafanua.

  Kwa mujibu wa mzee Bomani, wakati mikataba hiyo ikitiwa saini bei ya dhahabu ilikuwa chini ambayo ni dola za Marekani 260 kwa wakia lakini, leo hii bei ya dhahabu ni
  dola za Marekani 1,500 kwa kila wakia.

  Akikazia katika eneo hilo, Jaji Bomani alisema, "Maana yake ni kwamba kampuni za madini zinapata mapato ya juu kweli kweli." (Na Tanzania inaambulia vijisenti tu!)

  Mwanasheria huyo nguli, alisema sababu za masahama huo kwa kipindi hicho ilikuwa kuwahakikishia wawakezaji kwamba wakati wote wangekuwa na akiba ya fedha zao nje kwa ajili ya manunuzi kwani walikuwa na matumizi makubwa.

  Bomani alihoji, "Je, msamaha huo bado unahitajika kweli katika hali ya bei ya sasa ya dhahabu ambayo ni karibu mara tano ya bei ya wakati huo, ikizingatiwa matumizi makubwa makubwa yamepungua?"

  Aliongeza, "hivi karibuni kampuni ya African Barrick Gold ilitoa taarifa yake ya mwaka 2010, ikitamba mambo yalikuwa mazuri kweli kweli! Hata kama kampuni hizi bado zina msamaha huo uliotolewa zaidi ya miaka kumi iliyopita, haziwezi zenyewe kwa kuzingatia mahitaji ya nchi, zikarejesha nchini angalau sehemu ya mapato hayo, hata kama serikali inazionea huruma au haya?" (Mhhhh! Wachukuaji hawa wanachota tu!)

  Mauzo ya madini mwaka 2010

  Jaji Bomani alisema mwaka jana thamani ya dhahabu iliyouzwa nje ya nchi ilikuwa zaidi ya dola 1.4 bilioni za Marekani na kwamba, "kampuni hizi zingekuwa zimerejesha asilimia 50 tu ya mapato yake zingekuwa zimerejesha nchini zaidi ya dola 700. milioni za Marekani (takriban sh 1.2trilioni).

  Alisema ukiongeza mapato yanayotokana na na vyanzo vingine kama utalii, uuzaji wa bidhaa mbalimbali, ikiwa ni pamoja na uuzaji mazao ya kilimo na misaada mbalimbali nchi ingekuwa imejipatia dola nyingi na shilingi ingeendelea kubaki imara.
   
 2. Mufiyakicheko

  Mufiyakicheko JF-Expert Member

  #2
  Apr 20, 2011
  Joined: Mar 24, 2011
  Messages: 893
  Likes Received: 2
  Trophy Points: 0
  wasomi wetu hawajanawa uso hawayaoni hayo wala kusikia ata huluma hawana kwa wadanganyika
   
 3. Niko

  Niko Member

  #3
  Apr 20, 2011
  Joined: Mar 12, 2011
  Messages: 99
  Likes Received: 2
  Trophy Points: 0
  Angeanza kwa kusema "samahani, nilisahau kulijumuisha hili kwenye ripoti yangu," ningemwona wa maana sana.
   
 4. BONGOLALA

  BONGOLALA JF-Expert Member

  #4
  Apr 20, 2011
  Joined: Sep 14, 2009
  Messages: 13,782
  Likes Received: 2,391
  Trophy Points: 280
  kuthubutu ni kitu muhimu sana ktk maendeleo!tatizo la serikali yetu haina uthubutu hata chembe!mtu anadanganywa kusomeshewa watoto huku anaachia trilions!wananchi geita wakati wowote watapambana na GEITA GOLD MINE kwani wanachoambulia ni sumu kali toka machimboni
   
 5. King'asti

  King'asti JF-Expert Member

  #5
  Apr 20, 2011
  Joined: Nov 26, 2009
  Messages: 27,506
  Likes Received: 2,248
  Trophy Points: 280
  <p>
  </p>
  <p>&nbsp;</p>
  wasomi wanajua yote haya na wanashauri.maamuzi yanafanywa na wanasiasa!kulikuwa na sheria mpya ambayo ilikuwa ianze mwaka jana mwishoni (sina hakika kama ilishasainiwa na rais) ya kuongeza mrahaba to a shamefull 10% (wakati makato ya kodi ya mfanyakazi ni around 30%).
   
 6. Mufiyakicheko

  Mufiyakicheko JF-Expert Member

  #6
  Apr 21, 2011
  Joined: Mar 24, 2011
  Messages: 893
  Likes Received: 2
  Trophy Points: 0
  wasomi wetu ndo wanao shilikiana na wanasiasa kusaini mikataba fek ufisadi na hao wasomi wamesoma kwa kodi zetu ninaimani wanasiasa hawana ubavu kama wasomi wakawa na msimamo juu ya vitengo wanavyo simamia narudia wasomi wetu hawajanawa uso hawaoni wara hawasikii kujuwa si tatizo jee? wanatenda wayajuwayo au wanatenda yao ata shetani anazijuwa sana sheliya za mngu jee anaendana nahizo sheliya bora usijuwe kabisa
   
Loading...