Mystery
JF-Expert Member
- Mar 8, 2012
- 15,842
- 31,073
Wewe unasema wapiga kura walizidi huko Pemba.Na hili la Maalim Sefu kujipa nafasi ya ZEC na kujitangaza mshindi nalo mnalisemeaje. na ile idadi ya wapiga kura iliyozidi kule Pemba watu wakae kimya, hizo siyo dosari zisisemwe? unafki huo. uchaguzi urudiwe tu. CUF wajiamini. kama ushindi ni wao wataupata tu.
Sasa nikuulize swali moja tu jepesi, hivi si kila kituo kulikuwa na mawakala wa vyama vyote?
Sasa kama mawakala hao, pamoja na wa vyama vya CCM na CUF waliweka saini ya fomu za matokeo, ikiwa na maana walikuwa wamejiridhisha kuwa uchaguzi haukuwa na kasoro zozote.
Sasa huyo Jecha kukurupuka na kutangaza kuyafuta matokeo hayo tena bila kushirikisha makamishna wenzake wa ZEC, hivi huo bado
haujawa ushahidi wa kutosha wa mazingira kuwa Jecha 'aliamriwa' na CCM kutoa tamko hilo baada ya kugundua ya kuwa mgombea wao Dr Shein amebwagwa na Maalim Seif?
Kwa hali inayoendelea nchini mwetu ya CCM kutaka kung'ang'ania madarakani hata kwenye yale maeneo wanayojua dhahiri wameshindwa, kutakuja kuiletea maafa nchi hii.
Mfano halisi ni uchaguzi huo wa Zanzibar na hivi sasa umehamia kwenye uchaguzi wa mameya huku Bara.
Tumeshuhudia huko Tanga jana namna uchaguzi wa meya wa huko, namna msimamizi wa uchaguzi alivyoamua kumtangaza mgombea wa CCM ambaye alishindwa kuwa ndiye mshindi na mgombea wa CUF ambaye ndiye aliyeshinda akatangazwa kushindwa!
Hata hivyo kama lilivyotokea kwa Jecha baada ya kuyafuta matokeo ya Zanzibar 'akapelekwa' mafichoni, vivyo hivyo kwa msimamizi wa uchaguzi wa jijini Tanga, naye amesepa kwenda mafichoni mara tu baada ya kutangaza kuwa mgombea wa CCM kuwa ndiye aliyeshinda uchaguzi.
Hivi kama kweli msimamizi huyo angekuwa ametangaza kitu ambacho yeye aliamini ndicho sahihi, ni kitu gani kilichomtoa nduki baada ya kuyatangaza matokeo hayo??!!!!