GHIBUU
JF-Expert Member
- Jan 13, 2011
- 4,432
- 3,016
Na Gwamaka Alipipi
18th December 2015
Aliyewahi kuwa Mwanasheria Mkuu na Jaji mstaafu, Mark Bomani ameshauri liundwe jopo la wataalam wa masuala ya uchaguzi kubaini na kuzifanyia kazi dosari zilitokea katika mgogoro wa uchaguzi Zanzibar.
Jaji Bomani amesema jopo hilo lijumuishe wajumbe kutoka Tume ya Taifa ya Uchaguzi (NEC), Idara ya Uchaguzi ya Umoja wa Madola (Commonwealth), Umoja wa Afrika (AU) na liongozwe na Jaji Mkuu.
Aidha, amesema baada ya kuundwa kwa jopo hilo, daftari la wapiga kura lipitiwe kwa umakini kubaini dosari hizo kisha uchaguzi urudiwe haraka hata ikiwezekana ndani ya siku 30 tangu kuundwa kwa jopo hilo.
Alisema kama mgogoro wa Zanzibar hautapatiwa ufumbuzi haraka, madhara yake ni makubwa kwa taifa kwa kuwa hakutakuwa na serikali halali iliyochaguliwa na wananchi.
Jaji Bomani ametoa kauli hiyo tayari zimepita siku 73 tangu matokeo ya uchaguzi mkuu kufutwa na Mwenyekiti wa Tume ya Uchaguzi Zanzibar (ZEC), Jecha Salim Jecha kwa kile kilichoelezwa kuwapo kwa kasoro kadhaa zilizojitokeza wakati wa kupiga na kuhesabu kura.
Kufutwa kwa matokeo hayo, hadi sasa muafaka wa kutatua mgogoro huo visiwani Zanzibar haujapatikana, huku mgombea urais kupitia Chama cha Wananchi (CUF), Maalim Seif Sharif Hamad akidai kuwa yeye ndiye mshindi wa uchaguzi huo.
Maalim Seif anadai kuwa alipata kura 200,007 sawa na asilimia 52.87 baada ya chama chake kukusanya fomu za matokeo vituoni na kufanya majumuisho.
Akizungumza na waandishi wa habari Dar es Salaam jana, Jaji Bomani alisema baada kurudiwa kwa uchaguzi huo, jopo hilo litatakiwa liendelee kuwapo wakati wa kurudia uchaguzi, ili lishuhudie mwenendo wote wa uchaguzi.
Alisema kabla ya uchaguzi huo kurudiwa, wagombea wote pamoja na vyama vyao wale kiapo kwa kuahidi kukubali matokeo ya uchaguzi wa marudio.
Jaji Bomani alisema mgogoro uliopo sasa Zanzibar, hauwezi kupatiwa ufumbuzi bila kufuata sheria na katiba.
?Njia pekee ambayo inaweza kumaliza mgogoro huu wa Zanzibar ni kwa uchaguzi kurudiwa bila ya kuchelewa, lakini chini ya masharti ya haki, uwazi na yanayoridhisha,? alisema Jaji Bomani.
Aliongeza kuwa Maalim Seif asiendelee kujitangaza kuwa mshindi na wala asiogope uchaguzi kurudiwa kwani wananchi waliompigia kura hapo awali watarudia kufanya hivyo katika uchaguzi wa marudio na pengine kuongezeka.
Alisema kujitangaza kuwa mshindi, haileti maana yoyote kwa kuwa ZEC, ndiyo inayomtangaza mshindi kisha kuapishwa na Jaji Mkuu.
AKERWA NA RUSHWA
Jaji Bomani alisema anasikitishwa na vitendo vya rushwa au matumizi ya fedha chafu vilivyokuwa vinatokea wakati wa uchaguzi mkuu uliopita.
Alisema baadhi ya wagombea kwa kiasi kikubwa walikuwa wanatumia fedha chafu kama hongo na kushinda uchaguzi na kueleza kuwa: ?Hilo jambo linastahili kukemewa na kulaaniwa.?
KATIBA MPYA
Jaji Bobani alisema mchakato wa kupata Katiba mpya uendelee, lakini mpaka mgogoro wa Zanzibar utakapotatuliwa na kupatikana kwa serikali mpya ya Zanzibar.
Kuhusu migogoro ya ardhi na ile ya wafugaji na wakulima, Jaji Bomani alisema: ?Serikali inapaswa kuweka kipaumbele cha hali ya juu kwa sekta ya ufugaji kutambuliwa.?
CHANZO: NIPASHE
Bonge 19/12/2015 kwa 10:01 mu ? Jibu
Aibu kwa Mark Bomani, bora angenyamaza kimya kulinda hadhi yake, Bila shaka amekurupuka pasi na kufanya uchambuzi wa kina katika jambo hili.
Hebu tuzichambue hoja zake za kipuuzi:
Amesema: ?liundwe jopo la wataalam wa masuala ya uchaguzi kubaini na kuzifanyia kazi dosari zilitokea katika mgogoro wa uchaguzi Zanzibar?
Kwanza, mgogoro wa Zanzibar ni wakutengeza baada ya CCM kushindwa kwa lugha nyengine ?hakuna mgogoro? ni ujanja wa kung?ang?ania madaraka tu!
Pili, dosari zipi anazozizungumza hali ya kuwa hakuna fomu za malalamiko kutoka kwa mawakala wa vyama? Bora angependekeza jopo liundwe kuchunguza Dosari nyingi za wazi zilizotokea katika uchaguzi wa Tanganyika lakini amefumbia macho kwa kuwa CCM imelazimisha ushindi.
Amesema: ?jopo hilo lijumuishe wajumbe kutoka Tume ya Taifa ya Uchaguzi (NEC), Idara ya Uchaguzi ya Umoja wa Madola (Commonwealth), Umoja wa Afrika (AU) na liongozwe na Jaji Mkuu?
Huyu mzee alikuwepo wapi wakati Jumuiya ya Madola, Jumuiya ya Ulaya, Umoja wa Africa, Jumuiya ya Afrika Mashariki na SADC walipotoa ripoti yao kuwa uchaguzi hususan wa Zanzibar ulikua huru, haki na uwazi na wamesikitishwa kufutwa kwa uchaguzi. Anadhani hawa jamaa ni wapumbavu kama yeye, eti leo uwaite tena wachunguze upuuzi wa CCM?
Amesema: ? baada ya kuundwa kwa jopo hilo, daftari la wapiga kura lipitiwe kwa umakini kubaini dosari hizo kisha uchaguzi urudiwe?
Kabla ya uchaguzi wapinzani walipiga kelele nyingi kuhusu daftari la wapiga kura, Yeye alikuwepo wapi wakati huo ili kupendekeza kuwa liundwe jopo la kupitia daftari hilo? Huyu mzee punguwani! Leo baada ya CCM kushindwa anakuja na hoja za kipuuzi za kuchunguza daftari.
Eti ?uchaguzi urudiwe haraka? Swali, kipengele kipi cha katiba au sheria ya uchaguzi kinachompa mamlaka Jecha kufuta uchaguzi? Je uchaguzi ulioharibika ni wa raisi tu? Wawakilishi wote walishakabidhiwa vyeti vya uthibitisho wa ushindi na uchaguzi ulishamalizika tokea 25 Oktoba. Jamani huyu ni mwanasheri gani? Au alikuwa ameshalewa? Je, sababu zipi za msingi zinazopelekea kurudiwa kwa uchaguzi? Kura 5 zilipigwa katika kituo kimoja, wasimamizi walewale, wapigakura haohao, kura 4 zilienda sawa lakini ya uraisi wa Zanzibar zimeharibika!
Huyu Mzee ni kibaraka wa CCM na usomi wake tanautilia mashaka, ameshindwa kutaja hoja za walio wengi wanaodai kuwa uchaguzi ulikuwa huru, haki na wazi hivyo hakuna haja ya kurudia uchaguzi bali mshindi wa uchaguzi atangazwe. Yeye amekariri hoja za CCM eti ?Njia pekee ambayo inaweza kumaliza mgogoro huu wa Zanzibar ni kwa uchaguzi kurudiwa bila ya kuchelewa?. Wazanzibari tunakwambia, uchaguzi haurejewi na mara hii Tanganyika mtaonja joto ya jiwe kwa hili mpaka mtakapoitema Zanzibar.
Jaji Bomani alisema mgogoro uliopo sasa Zanzibar, hauwezi kupatiwa ufumbuzi bila kufuata sheria na katiba. Shabash! Katiba na sheria zipo wazi kuwa, uchaguzi ulishamaliza tokea tarehe 25, Mwenyekiti wa tume hana mamlaka ya kufuta uchaguzi, hakuna chama kilichowasilisha fomu za malalamiko, wawakilishi walishapewa vyeti vya ushindi, wabunge na Raisi wa Jamhuri walishaapishwa, majimbo 31 yalishatangazwa, kilichobaki ni kumtangaza mshindi wa uraisi wa Zanzibar.
Hivi Bomani na CCM wenzio mnaogopa nini kuachia madaraka hali ya kuwa wananchi walishaamua kuwaondoa madarakani?
Mnachoweza kufanya ni kuchelewesha kutenda haki lakini hamuwezi kuepuka wimbi la mabadiliko, mkijaribu kuforce mtaiyona people?s power, na Tanzania haitatawalika tena!
rasmi 18/12/2015 kwa 8:41 um ? Jibu
?
Khasara za Nyerere
In June, The Economist of London had declared, in an article entitled ?The Perils of Nyerere,? that the President had ?managed half the work of a python.? It continued: ?He swallowed Zanzibar all right but he did not crush its fighting force first. The live animal is a long time digesting, and its kicks are being felt hurtfully, and possibly even fatally, deep inside Tanganyika?s body politic.? Kutoka kitabu cha William Edgett Smith in We Must Run While They Walk: A Portait of Africa?s JULIUS NYERERE. p. 179.
Jarida la The Economist la London lilitangaza katika makala iitwayo ?Khasara za Nyerere.? Kuwa Rais [Nyerere] ?ameifanya nusu ya kazi ya chatu.? Makala inaendelea: ?Ameimeza Zanzibar, sawa, lakini hakuzizuwa nguvu zake za kujitetea kwanza. Mnyama [Zanzibar] yuhai na kwa muda mrefu amekuwa anaendelea kula, na mateke yake yenye kuumiza na yenye uwezo wa kuuwa yanapiga ndani ya tumbo la utawala wa Tanganyika.? From William Edgett Smith in We Must Run While They Walk: A Portait of Africa?s JULIUS NYERERE. Ukurasa wa 179
Quote kutoka facebook page ya Jamhuri Ya Watu Wa Zanzibar.
Huyo Jaji ni mmoja wa waendelezaji wa kazi ya Nyerere, kwa Zanzibar amenoa?
Jibu: Moyo
Huyu bomani anakuja na maneno ya kilevi! Mimi nilivyosikia anataka kuzungumza na waandishi wa khabari nilidhani anataka kuwaambia kweli ccm kumbe kaja na upuuzi huu.
Uchaguzi urudiwe kwa sababu gani! Uchaguzi ulikuwa huru na usio na mizengwe ukilinganisha na chaguzi zote zilizopita huko nyuma, hapakuwa na malalamiko wakati wa uchaguzi kutoka katika vyama vyote, matokeo yameshatangazwa zaidi ya asilimia 50, kwa kuwa ccm wameshindwa ndio uchaguzi urudiwe! Au hamjaridhika mpaka mwataka wazanzibari tuuwane ndio muone raha?
Nataka nimrudi bomani kwa baadhi ya vipengele alivyovitaja:
1) Anasema paundwe tume itakayoshirikisha hao watu aliowataja na iongozwe na jaji mkuu.
Raddi: Hata muunde tume ya malaika hakutakuwa na maana yoyote wakati mshindi anajuulikana na kwamba ameshinda kihaki. Bali ni khasara ya kupoteza pesa na wakati na kusababisha machafuko ambayo yanaweza kupoteza roho za wazanzibari.
Eti tume hio iongozwe na jaji mkuu! Kwani ukisikia jaji mkuu ndio hafanyi makosa na ni muadilifu? Kama huyo jaji hana kazi na anatafuta la kufanya na aende akaishughulikie kesi ya mashekhe wa uamsho na waislaamu wengi wa tanganyika wanateseka gerezani kwa dhulma, kama ni muadilifu kweli aende huko akafanye huo uadilifu.
2) Anasema maalim asiogope kurudia uchaguzi?
Raddi: Kwani maalim ndie mwenye haki ya kura za wazanzibari? Maalim hana kura ya veto, kura yake ni moja sawa na kura ya mzanzibari yoyote , hivyo hio ni haki ya wazanzibari na hatutaki zaidi ya kupewa haki yetu sio vyenginevyo.
3) Anasema wagombea urais wale kiapo cha kukubali matokeo.
Raddi: Kwani alieshindwa kutamka kukubali kushindwa ni nani? Si sheni! wacha kula kiapo, kwani hivyo viapo vya kujiapiza si munakula kila siku kulinda katiba na sheria! Mbona nyinyi mnaokula viapo hinyo si ndio wa mwanzo mnaovivunja? Sasa hicho kiapo ukisemacho wewe kina utofauti gani na hivyo mnavyo vila kila siku? Au hiki cha mara hii watakuja mitume kukisimamia?
4) Anasema eti anasikitishwa na baadhi ya wagombea kutoa rushwa!
Raddi: Wacha uongo wako nyinyi majaji ndio wala rushwa nambari moja leo wajitia kusikitishwa na hilo!
Nakhitimisha kwa kusema kama wewe umetumwa umuingize maalim katika mtego huo basi tambua umechelewa na jua kuwa wazanzibari si wajinga ni watu wenye akili kuwapita nyinyi waTanganyika na ndio maana mpaka leo mwateseka na zanzibar hamli vikawashuka wala hamlali mukapumzika mpaka pale mtakapoitema zanzibar.
Hapa hakuna atakaerudia uchaguzi, kama nyinyi ni wababe na madikteta twendeni hivi hivi na kama munaweza mtawazeni sheni kuwa ni mfalme wa zanzibar.
Eti jaji mkuu! Mtu mzima ovyooooo kama uchaguzi uliharibika zanzibar basi na tanganyika pia ume haribika maana kura za ushindi wa magufuli nyengine zimetokea zanzibar na kama kurejea uchaguzi basi urejewe wa tanzania nzima maana huko tanganyika zimekamatwa kura malori kwa malori na nyengine kuonekana misituni zimetupwa na wapo watu waliopigwa mpaka kuchiririka damu kwa kukamatwa na kura feki na hayo yote yalizagaa katika mitandao ya kijamii lakini hilo hamkuliona kuwa ni tatizo, na huku zanzibar hatukuona hizo dosari mlizosema bali ni porojo tupu.