Jaji awashauri waliomshtaki Askofu Kakobe kuondoa kesi | JamiiForums | The Home of Great Thinkers

Dismiss Notice
You are browsing this site as a guest. It takes 2 minutes to CREATE AN ACCOUNT and less than 1 minute to LOGIN

Jaji awashauri waliomshtaki Askofu Kakobe kuondoa kesi

Discussion in 'Jukwaa la Sheria (The Law Forum)' started by Rutashubanyuma, Aug 3, 2011.

 1. Rutashubanyuma

  Rutashubanyuma JF-Expert Member

  #1
  Aug 3, 2011
  Joined: Sep 24, 2010
  Messages: 158,806
  Likes Received: 419,846
  Trophy Points: 280
  [TABLE="class: contentpaneopen"]
  [TR]
  [TD="class: contentheading, width: 100%"]Jaji awashauri waliomshtaki Askofu Kakobe kuondoa kesi
  [/TD]
  [TD="class: buttonheading, width: 100%, align: right"] Send to a friend [/TD]
  [/TR]
  [/TABLE]
  [TABLE="class: contentpaneopen"]
  [TR]
  [TD="class: createdate"] Tuesday, 02 August 2011 20:13 [/TD]
  [/TR]
  [TR]
  [TD]

  James Magai
  JAJI wa Mahakama Kuu, Augustine Shangwa, amewashauri wachungaji wanaomshtaki Askofu Mkuu wa Kanisa la Full Gospel Bible Fellowship (FGBF), Zacharia Kakobe, wakatafari upya juu ya madai yao kuona kama yana msingi na wanapaswa kuendelea nayo.Wachungaji hao wanaodai kuwa ni wa kanisa hilo, ni Dezedelius Patrick, Angelo Mutasingwa na Benedict Kaduma, wamemfunguliwa Askofu Kakobe kesi wakimtuhumu kwa matumizi mabaya ya fedha za kanisa yanayokadiriwa kufikia Sh14 bilioni.

  Kesi hiyo ilipotajwa mahakamani hapo jana, Jaji Shangwa aliwashauri walalamikaji hao kutafakari madai yao na ikiwezekana wayaondoe mahakamani.Pia, Jaji Shangwa aliwatahadharisha kuwa iwapo wataamua kuendelea nayo na katika uamuzi wa mahakama, wakishindwa watajuta kwa sababu watatakiwa kumlipa Askofu Kakobe fidia kubwa na gharama za uendeshaji kesi, ambazo hana hakika kama watamudu.

  Kabla ya kuwashauri walalamikaji hao, Jaji Shangwa alianza kwa kuonyesha wasiwasi wake juu ya msingi wa madai ya walalamikaji kuhoji matumizi ya fedha za kanisa hilo.Alisema kwa mfumo wa FGBF, Kakobe ndiyo kanisa na kwamba mapato ya kanisa hilo ni mali ya Kakobe kwa sababu, kanisa hilo alilianzisha mwenyewe na kuhoji iweje wamhoji mtu anayetumia mali yake.

  “Kwani ni nani alimpa Kakobe uaskofu? Kakobe alijifanya mwenyewe, ni tofauti na maaskofu wa Katoliki ambao mpaka waende wakasomee;
  Msiniambie nina-prejudge (nihukumu kabla), maana huwa mnatulaumu kesi kurundikana mahakamani. Mimi hapa natafuta suluhu na suluhu ni pamoja na kuondoa kesi mahakamani,” alisema Jaji Shangwa.

  Jaji Shangwa alihoji kosa la Kakobe kukusanya michango kutoka kwa wanajumuia na kwenye mikutano ya mahubiri anayofanya nchi mbalimbali, kujengea nyumba yake kama walalamikaji wanavyodai.
  “Lakini si anatumia fedha zake? Mimi najiuliza maana ndiyo alianzisha kanisa, kama kulikuwa na wafadhili ndiyo akawafundisha nanyie mkawa wachungaji;

  Hizi fedha hapewi na serikali ni za wale anaowatibu na wanaokuja kuombewa mapepo. Kwa hiyo anazikusanya kwa huduma, sasa mtamuulizaje na chake?;
  Labda mngesema kuwa hawapi au anawapunja mshahara wakati mnashinda kanisani mnaombea mapepo, maana hii ni kazi kubwa,” alihoji Jaji Shangwa.

  Hata hivyo, Jaji Shangwa aliwataka walamikaji hao kujibu pingamizi lililowekwa na Kakobe dhidi yao, Septemba 5, mwaka huu kesi hiyo itakapoendelea.
  Kakobe kupitia kwa Wakili wake, Miriam Majamba, anapinga walalamikaji hao hawana hadhi ya kisheria kumshtaki kwa kuwa siyo wachungaji wa kanisa hilo, kwani walishafukuzwa uchungaji hivyo hawana mamlaka ya kuhoji jambo lolote linalohusiana na kanisa hilo.

  Wakati Kakobe akiwawekea pingamizi hilo, walalamikaji nao juzi waliwasilisha maombi mahakamani wakiomba mahakama isipokee maelezo ya utetezi wa maandishi ya Kakobe kwa kuwa yamewasilishwa nje ya muda wa siku 21 kisheria.

  Katika kesi hiyo namba 79 ya mwaka 2011, ilifunguliwa na wachungaji hao Juni 21, wakiorodhesha tuhuma mbalimbali za matumizi mabaya ya fedha za kanisa hilo yanayofanywa na Kakobe na kwamba, amekuwa akikiuka Katiba ya kanisa hilo.

  Wanadai Sh10 bilioni zinazodaiwa kutumika kwa ujenzi wa eneo la kanisa na Sh800 milioni zinazodaiwa kutumika kuanzisha kituo cha televisheni. Pia, wachungaji hao wanamshutumu Askofu Kakobe kwa kutoitisha mkutano mkuu wa kanisa hilo tangu mwaka 1989.
  [/TD]
  [/TR]
  [/TABLE]
   
 2. Rutashubanyuma

  Rutashubanyuma JF-Expert Member

  #2
  Aug 3, 2011
  Joined: Sep 24, 2010
  Messages: 158,806
  Likes Received: 419,846
  Trophy Points: 280
  tatizo kwa jaji shangwa ni ukiukaji wa maadili..........................yeye anazungumzia gharama za kesi na msingi wa madai husika wakati yeye ndiye jaji wa kuchunguza..........................kauli yake hii yaonyesha upendeleo hasa ukizingatia ya kuwa akiwa jaji wa kesi hiyo hapaswi kutoa maoni hata kama ya kiusuluhishi bali alipaswa kulipeleka jarida tajwa kwa jaji mwingine ili awasuluhishe ....................kesi hii inahusu katiba ya kanisa ambayo hata hivyo jaji shangwa hakuidadisi uhalali wake na inasemaje hivyo hayupo kwenye nafasi ya kuoni kama alivyoni.........................ushauri wangu ni waddawa wamkatae jaji tajwa kwa sababu kauli zake zaonyesha upendeleo mkubwa.
   
 3. Rutashubanyuma

  Rutashubanyuma JF-Expert Member

  #3
  Aug 3, 2011
  Joined: Sep 24, 2010
  Messages: 158,806
  Likes Received: 419,846
  Trophy Points: 280
  [h=4]Comments [/h]


  0 #2 ahmed00 2011-08-03 02:41 Mh Judge nakubaliana nawe, hilo ni jambo la pande zote kukaa chini na kujadiliana.
  I wish Mh WEREMA angekuwa na busara kama zako
  Quote

  0 #1 Mugariga 2011-08-03 02:25 Jaji busara zipo hii kesi ni hewa tupu tu na kupotezeana muda.
  Quote
   
 4. Mzee Wa Rubisi

  Mzee Wa Rubisi JF-Expert Member

  #4
  Aug 3, 2011
  Joined: Nov 6, 2010
  Messages: 1,754
  Likes Received: 71
  Trophy Points: 145
  Wakina Yuda,tamaa ya fedha
   
 5. G

  Gad ONEYA JF-Expert Member

  #5
  Aug 3, 2011
  Joined: Oct 26, 2010
  Messages: 2,641
  Likes Received: 4
  Trophy Points: 135
  Mambo ya kanisa huwa hayaamuliwi kwenye mahakama za kawaida, hawa wachungaji(?) kama wanamwamini Mungu wao kwa nini wasimshitakie? Ukiona hivyo jua hapa hakuna Mungu wa kweli ila biashara tu!
   
 6. Kiranga

  Kiranga JF-Expert Member

  #6
  Aug 3, 2011
  Joined: Jan 29, 2009
  Messages: 34,607
  Likes Received: 6,197
  Trophy Points: 280
  Duh, jaji gangstar kwanza kashajihukumu mwenyewe kwa ku pre-judge.

  The interesting take here ni assertion ya kamba kisheria kanisa ni mali ya Kakobe ( which tells me the judge went through the structure of that church).

  The folly of evangelical churches, watu mnatoa sadaka miaka nenda rudi kumbe mnamchangia mtu.

  Kumbe ndiyo maana Kakobe alikazania sana ukija na mkufu wa dhahabu shingoni kanisani uutoe sadaka.

  Alijua kiendacho kwa mganga wa kienyeji hakirudi, na yeye hana lolote zaidi ya mpiga ramli tu.

  Katika jina la Yesu.... Shindwa...
   
 7. Tutafika

  Tutafika JF-Expert Member

  #7
  Aug 3, 2011
  Joined: Nov 4, 2009
  Messages: 1,395
  Likes Received: 96
  Trophy Points: 160
  naunga mkono hoja. maslahi tuu yanawasumbua. makanisa siku hizi yamekuwa sehemu ya biashara kutafutia fedha. hakuna imani wala hofu kwa Mungu tena
   
 8. d

  damn JF-Expert Member

  #8
  Aug 3, 2011
  Joined: Feb 22, 2010
  Messages: 585
  Likes Received: 4
  Trophy Points: 35
  you are right Kiranga, na watu wanatoa on their own free will, na wanaoshtuka kama wewe hawatoi na wale kakobe hawezi kwenda kwa kiranga kumuuliza kwa nini hujaja kunitolea sadaka. So is those wachungaji kakobe never forced them to join his course, they joined him on their own free will, they have to leave on their own free will.

  Sikiliza hapo uone how some of these so called wachungaji walivyo: Bomu la Kakobe Part1 na Bomu la Kakobe part 2
   
 9. SMU

  SMU JF-Expert Member

  #9
  Aug 3, 2011
  Joined: Feb 14, 2008
  Messages: 7,933
  Likes Received: 2,085
  Trophy Points: 280
  Kwa kusema FGBF ni mali binafsi ya Kakobe, nadhani Judge Shangwa amepotoka.....na kwa kweli kama alivyosema mwenyewe ame pre judge.

  'Makanisa' yote (likiwemo FGBF) yanasajiliwa kama taasisi (jumuiya za watu) zisizo za kiserikali (za kidini) na kimsingi kunakuwapo na masharti mbalimbali likiwemo 'katiba' na taratibu ambazo ni za kitaasisi na sio kama mali binafsi ya muanzilishi. Hivyo sio kweli kwamba haiwezekani kumshitaki Kakobe kwa matumizi mabaya ya fedha (kama yapo).
   
 10. g

  great vision Senior Member

  #10
  Aug 3, 2011
  Joined: Jul 1, 2011
  Messages: 111
  Likes Received: 55
  Trophy Points: 45
  kimsingi mkuu,jaji anapopitia utetezi wa mtu, anaangalia kama kuna kesi ya kujibu au la ! mimi ninadhani baada ya kufanya hivyo aliona fika hapa hakuna kesi ya kujibu. wewe umesikiliza zile CD za mpango wa kimafia waliokuwa wanapanga hawa wanaomshitaki? pili je wewe unajua utetezi aliouwakilisha Askofu kakobe mahakamani? ki-msingi kwa mtu aliyekuwa anafuatia kwa makini alijua fika hawa waliomshitaki hawawezi kufika mbali, kwa sababu ni majungu matupu hakuna kesi hapo. kwanza si wachungaji wa FGBF-CHURCH, Pili kakobe hashiki pesa za kanisa hilo.kwa maelezo ya Katibu Mkuu wa FGBF, Askofu Nathan Meshack .MTUNZA HAZINA MKUU WA KANISA HILO ni Askofu JIMMY SAKUYE .na Maaskofu 19 na Wachungaji zaidi ya 400 waliokuja Dar toka ktk Mkutano mkuu walithibitisha hilo mbele ya waandishi wa habari,pia Katibu Mkuu alionyesha saini za wachungaji wapatao 447 ambao ndiyo wajumbe wa Mkutano mkuu kisheria kulingana na Katiba ya Full Gospel , waliomchagua kakobe kuwa Askofu MKUU,TENA WA MILELE yaani hadi kifo chake. Huyo DEzy alikuwa haendi ktk Mkutano Mkuu hata akichangiwa pesa na kanisa alilokuwa analiongoza huko mafinga kabla ya kufukuzwa kwa utapeli mwingi, anakwenda DAR kutanua nazo, hata michango ya waumini wake ya mfuko wa kitaifa ilikuwa haifiki,wenzake wapo DODOMA yeye hupo Dar kwenye Biashara zake na Matanuzi.jaji alijua fika wanapoteza muda tu> na siku ya siku itawabidi kumlipa Askofu kakobe >je wataweza? na mimi nasema kwa sababu wanafanya mchezo .Bishop wakiendelea na Kesi ukishinda wang'ang'anie walipe hadi senti ya mwisho ili na wengine wajifunze.mwisho wewe ndugu yangu Kakobe ameshasema mara chungu nzima yeyote anayedai nimemnyanganya mkufu wa dhahabu ajitokeze hadharani. na hatujawahi KUMWONA awaye yote. yote ni majungu fika kanisa kwake ndiyo utajua mbivu na mbichi. hata wanaotoa sadaka zao wanaridhika na kazi ya Mungu inayofanyika ndiyo maana wanaendelea kutoa, la sivyo wasingetoa.
   
 11. n

  njija Senior Member

  #11
  Aug 4, 2011
  Joined: Jun 30, 2011
  Messages: 110
  Likes Received: 9
  Trophy Points: 35
  Ndugu yangu KIRANGA, wewe bado ni miongoni mwa watu wanaoendekeza majungu na maneno ya kijiweni bila kuyafanyia UCHUNGUZI,mimi siwezi kumtetea Askofu Kakobe kwani jambo bado liko mahakamani lakini naomba usahihishe kauli yako ya KUSEMA KUWA ASKOFU KAKOBE ALIKUWA ANAWAAMBIA WATU WAJE NA MIKUFU KISHA KUICHUKUA AU KUITOA SADAKA, KUMCHAFUA MTU KWA JAMBO LA UONGO NIKOSA KABISA TENA SIO UUNGWANA,WALIOFANYA UCHUNGUZI JUU YA JAMBO HILI WATAUNGANA NA MIMI KUWA BISHOP HAJAWAHI KUFUNDISHA WATU WALETE MIKUFU KUZITOA SADAKA, BADALA YAKE MAFUNDISHO AMBAYO YAMEKUWA YAKITOLEWA KANISANI HAPO YAMEKUWA YAKIPINGA MAPAMBO KWA WANAWAKE NA IMEWAPELEKEA WANAWAKE KATIKA KANISA HILO KUTOKUVAA MIKUFU, HELENI NA PETE. Hivyo kama wewe kweli utakuwa na uungwana ndani yako au kama wewe hupendi kusingiziwa jambo, tafuta ukweli wa jambo kisha kulisema ukiwa UNAUHAKIKA KULIKO KUMCHAFUA MTU BILA SABABU.NASEMA HAYA KWASABABU NIMEFANYA UTAFITI WA KINA KUHUSU JAMBO HILI TANGU MWAKA 1998 AMBAPO UVUMI HUU ULIANZA KUENEA KWA KASI KUBWA.
   
 12. l

  lumange Member

  #12
  Aug 5, 2011
  Joined: Jul 6, 2011
  Messages: 14
  Likes Received: 0
  Trophy Points: 0
  Bwana mkubwa tuambie Kakobe Uaskofu alipewa na nani?! ordaining ni mtu kutiwa ukuhani kwa kupakwa mafuta ili ukatangaze neno na kutenda kazi ya Bwana muumba ndivyo maandiko yanavyosema toka enzi ya akina Daudi. Sasa mtu kasajili NGO yake baada ya kushindwa venchurs nyingine kama vile Disco na kuuza kanda za mziki pale mwenge stand, baadae anashindwa kufuata masharti ya katiba iliyomsajili kwa kutumia udikteita kwamba kila atakaye mpinga anamfukuza katika kanisa ili amnyime mamlaka ya kulalamika!

  Hapana Bwana Jaji acha kesi iendelee kila upande u prove beyond reasonable doubt haki zake na si vinginevyo. Tena nashauri iwe open kwa kila msikilizaji kwani ina maslahi ya watu wengi.
   
 13. g

  great vision Senior Member

  #13
  Aug 7, 2011
  Joined: Jul 1, 2011
  Messages: 111
  Likes Received: 55
  Trophy Points: 45
  Na mimi nakuuliza MARTIN LUTHER ambaye ni mwanzilishi wa Kanisa la KKKT Duniani alitiwa mafuta na nani? au alipewa uaskofu na nani? Kuna mawazo Potofu kuwa watumishi wa Mungu wanawekwa ktk utumishi na wanadamu kitu ambacho ni kinyume na maandiko. YESU mwenyewe alisema "Roho wa Bwana yu juu yangu kwa maana amenitia mafuta kuwahubiri maskini habari njema" (LUKA 4:18-19) Anayewaita watu katika utumishi na kuwatia mafuta ni Roho Mtakatifu mwenyewe Bwana wa Mavuno.
   
 14. Mtazamaji

  Mtazamaji JF-Expert Member

  #14
  Aug 7, 2011
  Joined: Feb 29, 2008
  Messages: 5,972
  Likes Received: 33
  Trophy Points: 0

  Hahhahahaha Kiranga umenichekesha Ameeeeeeen
   
Loading...