Jaji Augustino Ramadhani achukua Fomu kugombea Urais wa JMT

Mkandara,

..Jaji Ramadhani ni mchungaji wa kanisa la Anglican.

..ni kanisa hilo ambalo tawi lake la Uingereza na Marekani wameruhusu ushoga na kusimika ukasisi wanawake.

..sasa kuna wakati tuliambiwa nchi hii haiwezi kuongozwa na Padri. Ili kumkatisha tamaa Dr.Slaa.

..Wengine wakasema haiwezi kuongozwa na Padri na Shekhe pia.

..hivi mimi najiuliza: hatuwezi kuongozwa na Padre, lakini ruksa kuongozwa na Mchungaji?

..pia kulikuwepo na propaganda za kuwakataa wazee, wenyewe wanasema hatuwezi kuongozwa na watu wenye "jana nyingi na kesho kidogo." Kiumri Jaji Ramadhani siyo rika moja au hajamzidi Dr.Slaa ambaye kina Nape wanamkashifu kwa kumuita "babu"?

cc ZeMarcopolo, Ritz, Nape Nnauye, Mag3, Molemo, Kimbunga
Unajambo lingine bado hujasema? Sema yote hasira zikuishe kwanza.
 
Sio kosa wala dhambi kwa watu wanaotoka kwenye nafasi za utumishi kama ulivozitaja kushiriki siasa.
Ukifuatilia nchi nyingi duniani wanafanya ivo mfano marekani Leon Panneta na Roberts Gates walishawai kuwa directors wa CIA kabla ya kuwa mawaziri wa ulinzi, same kwa Gen Collins Powell aliyekuwa mkuu wa majeshi ya marekani na baadae waziri wa mambo ya nje. Hata Israel mawaziri wakuu wao wengi wanatokaga kuwa majenerali wa jeshi kama Ariel Sharon hata huyu wa sasa Ehud Mubarak.
Kikubwa cha kuangalia ni je wanafaa kwa changamoto tulizo nazo?????

..hapa Mkandara anazungumzia Jaji Mkuu wa Mahakama ya Rufani.

..hiyo mifano ya US inahusu watu waliokuwa jeshini wakaingia kwenye siasa, siyo waliokuwa majaji wakaingia kwenye siasa.

..Upande wa Majaji nafasi zao ni tofauti kidogo. Hata miiko ya kazi zao ni tofauti na miiko ya kazi nyingine. Hawa tunawategemea hawatakua na matamanio yoyote yale ya kujihusisha na siasa kutokana na wao kuwa ndiyo watoa haki.

..Mimi nadhani sheria yetu ingeweka gap ya kipindi fulani, toka wakati mtu ana-serve ktk bench mpaka anaporuhusiwa kugombea nafasi za kisiasa.

..Sasa hivi hata hatujui Jaji Ramadhani alijiunga lini na CCM. Je, alikuwa mwanachama hai wa CCM huku akitumikia kama Jaji Mkuu wa mahakama ya rufani?

cc Mkandara
 
Miezi kadhaa iliyopita niliwahi kuweka bandiko humu likidokeza kuwa JK alikuwa akimnong'oneza jaji Othamn Chande, jaji mkuu wa Tanzania kuwa mpeperusha bendera wa urais CCM anaweza kutoka katika kitengo chao.

Katika bandiko hilo niliweka kwa makusudi jina moja tu la jaji Augustino Ramadhan na kuelezea wasifu wake.Bahati mbaya mods wameshalifuta bandiko hilo na sijui sababu ni nini.

Aidha naomba niwaombe radhi kuwa jumapili nilishindwa kupata taarifa sahihi za mwana CCM atakayechukua fomu leo jumatano (Katika bandiko langu la "Majina saba yaipa kamati kuu ya CCM wakati mgumu") Katika bandiko hili nilimuweka Dr. Salim A Salim kama kinara wao
na ambaye angechukua fomu leo. Kimsingi niliambiwa kuwa yupo kinara atakayechukua fomu leo na nilipewa jina la uongo ambaye ni Dr. Salim.

Aidha aliyetakiwa kuchukua fomu leo kulingana na lile bandiko ni Jaji A. Ramadhan hivyo jina nililopewa kutoka vyanzo vyangu vya ndani nilipotoshwa (kumradhi wana JF)

Kwa maana hiyo basi 'mtarajiwa' kashachukua fomu!

Asanteni
 
Je, Jaji Mstaafu Augustino Ramadhani alikuwa kada wa CCM wakati wa utumishi wake katika Mahakama ya Tanzania?

Nyie teamel mnaonekana kuweweseka na kuuliza maswali yenye miguu lakini hayana kichwa. mtumishi ye yote wa serikali ana uhuru wa kuwa mwanachama wa chama cho chote. mbona Rais (head of state anakuwa mwanachama tena mwenyekiti).
 
Yaani hapa pa kutokea hakuna.Lalini huyu Jaji ametubana kweli huku Bara.Ngoja tuone.Lakini bado ukawa wapo.Na hawajambo kabisa.
 
mkuu hata mimi bado najiuliza. nimeamini ccm ni chama dola...

Vyama vya upinzani vinapambana na mfumo uliomo ndani ya Ikulu,Mahakama na Bunge,kwa hili nimeamini ndio maana ccm inakataa katiba,inafumbia wezi na wafujaji wa raslimali zetu na mtumishi wa serikali anaweza kujibu lolote kama alivyofanya Mnikulu kwa kuwa ikulu kote ni makada wa ccm,mahakamani,polisi,magereza,na ofisi nyingi za utumishi wa umma

Chadema hapa......
 
Rais ajae atakuwa na majina mawili la kiislam na kikristo - Utabili wa Hussein Yahya
 
Nyie teamel mnaonekana kuweweseka na kuuliza maswali yenye miguu lakini hayana kichwa. mtumishi ye yote wa serikali ana uhuru wa kuwa mwanachama wa chama cho chote. mbona Rais (head of state anakuwa mwanachama tena mwenyekiti).

Acha kutudanganya,ccm imewahi na inaendelea kuwanyanyasa watumishi wa serikali wanaoonesha wako wanachama wa vyama vya upinzani!

Mh.Pr.safari,Mh.pr. Ibrahimu Lipumba,Dr.Axervery Lwaitamba wamefukuzwa utumishi kisa,ni wapenzi wa vya vya upinzani!

Chama dola ndio imeua uwajibikaji,uwazi na uwajibifu kwa kuwa wahusika wakuu wa makosa haya ni makada wa ccm na

Ccm haitabadilika,this is ever!
 
Usikatae,kama alikuwa mwanachama mfu,mnawezaje kumpatia fomu ya kugombea Urais mtu ambaye hakijui chama na chama hakimjui?

Unajuwa hakuna kitu kigumu duniani kuwapa darsa mapunguani, soma:

1) Anaweza kuwa alikuwa mwanachama kabla hajateuliwa kuwa Jaji.
2) Akauwa uanachama wake alipoambiwa kuwa anataka kuteuliwa kuwa Jaji.
3) Alipostaafu ujaji akauhuisha uanachama wake.
4) Tatizo liko wapi?

Mbona ukawa mmeanza kuweweseka?
 
Miezi kadhaa iliyopita niliwahi kuweka bandiko humu likidokeza kuwa JK alikuwa akimnong'oneza jaji Othamn Chande, jaji mkuu wa Tanzania kuwa mpeperusha bendera wa urais CCM anaweza kutoka katika kitengo chao.

Katika bandiko hilo niliweka kwa makusudi jina moja tu la jaji Augustino Ramadhan na kuelezea wasifu wake.Bahati mbaya mods wameshalifuta bandiko hilo na sijui sababu ni nini.

Aidha naomba niwaombe radhi kuwa jumapili nilishindwa kupata taarifa sahihi za mwana CCM atakayechukua fomu leo jumatano (Katika bandiko langu la "Majina saba yaipa kamati kuu ya CCM wakati mgumu") Katika bandiko hili nilimuweka Dr. Salim A Salim kama kinara wao
na ambaye angechukua fomu leo. Kimsingi niliambiwa kuwa yupo kinara atakayechukua fomu leo na nilipewa jina la uongo ambaye ni Dr. Salim.

Aidha aliyetakiwa kuchukua fomu leo kulingana na lile bandiko ni Jaji A. Ramadhan hivyo jina nililopewa kutoka vyanzo vyangu vya ndani nilipotoshwa (kumradhi wana JF)

Kwa maana hiyo basi 'mtarajiwa' kashachukua fomu!

Asanteni

kwanini kuwasingizia mamod???

https://www.jamiiforums.com/jukwaa-...bendera-ya-urais-ccm-atatokea-kwa-majaji.html
 
Back
Top Bottom