Jaja, Countinho & Maximo

Jaja, Countinho & Maximo

Mnyampaa msingida

Senior Member
Joined
Aug 5, 2013
Posts
180
Reaction score
55
Nikiwaangalia wachezaji hawa wawili wabrazil kwa kweli sioni utofauti wao na wachezaji wa kitanzania. Maximo hapo anachezea ajira kwa wachezaji hao.
 
Tatizo la wachezaji wa kibongo wanabweteka sana, wakipewa nafasi hawazitumii Yanga kuna Bahanuzi,Javu na Tegete hawa kama wangeonyesha viwango sidhani kama Yanga wangehitaji kuwa na mshambuliaji kutoka nje
 
Jaja amecheza mechi tano amefunga goli moja, Tegete amecheza mechi moja isiyozidi dk 30 amefunga goal mbili. Je nani mkali.
 
1. Amisi Tambwe, mfungaji bora wa Ligi iliyopita, ameshafunga magoli mangapi? Ndio tuseme si fowadi/mfungaji mzuri?
2. Kipre Tchetche, mfungaji bora kabla ya msimu wa Tambwe, amefunga magoli mangapi? Ndio tuseme si fowadi/mfungaji mzuri?
3. Unamkumbuka Boniface Ambani? Msimu wake wa pili baada ya kuwa mfungaji bora wa Ligi Kuu, alifunga magoli mangapi? Ndio tuseme hakuwa fowadi/mfungaji mzuri?
4. Tegete kabla ya leo, alikwishafunga magoli mangapi ya Ligi Kuu kwenye misimu miwili iliyopita? Ndiyo tuseme kabla ya hapo hakupata kuwa fowadi/mfungaji mzuri?
4. Ballotelli tangu aende Lverpool ameshinda magoli mangapi? Ndio tuseme sio fowadi/mfungaji mzuri?
5. Van Parse mwaka huu ameshafunga magoli mangapi? Ndio tuseme sio fowadi/mfungaji mzuri?
6. Unamkumbuka Ballack wa Ujerumani/Bayern Munich? Alifanya vizuri alipohamia Chelsea? Ndio tuseme hakuwa mchezaji mzuri kabla ya hapo? Veron je? Decco?
7. Unamkumbuka shevchenko akiwa A C Milan? Aliendelea na wimbi hilohilo la ufungaji alipohamia Chelsea? Ndio tuseme hakuwa fowadi/mfungaji mzuri kabla ya hapo?
Kuna visababishi (factors) vingi vinavyomfanya mchezaji mzuri kutoonekana mzuri, (ingawa binafsi bado naamini Jaja na Coutinho ni wazuri licha ya kuwa wamefunga goli moja moja tu hadi sasa - mbona Niyonzima, Salim Abubakar, hamis Mcha nk hawajafunga hadi sasa na hatuwasemi kuwa sio wazuri?): ugeni, ushikaji mafunzo ya mwalimu mpya kwake, imani yake kwa uchezeshaji anaouona, mazingira ya nje ya uwanja/timu/kambi, kuogopwa kunakolazimisha kuchungwa kupita kiasi hata kama kwa mbinu haramu, kite (tension) bahati, ushirikiano na wachezaji wengine, n.k.
 
Unaweza kufananisha lakini watu wanahitaji kupiga hatua. Ukianza kusema ugeni, mafunzo ya Mwalim mpya, mpaka wajekushika hayo mafunzo ligi imeisha.
 
Hoja yangu kuu ni kwamba mchezaji kuchemsha kwenye ligi au msimu mpya haimaanishi kwamba mchezaji huyo hakuwa mzuri kwenye ligi au msimu uliotangulia. Na kwahivyo mwalimu, mchezaji au timu hiyo hawapaswi kulaumiwa moja kwa moja kwa bahati hiyo mbaya. Na kwamba si kweli kuwa Jaja na Coutinho ni mizigo kama baadhi ya wakengeza wa soka wanavyoona. Na kwamba rekodi ya mabao 3 ndani ya mechi 6 (aliyofunga Jaja ukihesabu na ya Ngao ya Hisani) au ya goli moja na 'assists' 4 kwenye 6 (takwimu za harakaharaka za Coutinho tangu Ngao ya Hisani) si rekodi mbaya kama mwanzisha mada anavypojaribu kuonesha.
 
1. Amisi Tambwe, mfungaji bora wa Ligi iliyopita, ameshafunga magoli mangapi? Ndio tuseme si fowadi/mfungaji mzuri?
2. Kipre Tchetche, mfungaji bora kabla ya msimu wa Tambwe, amefunga magoli mangapi? Ndio tuseme si fowadi/mfungaji mzuri?
3. Unamkumbuka Boniface Ambani? Msimu wake wa pili baada ya kuwa mfungaji bora wa Ligi Kuu, alifunga magoli mangapi? Ndio tuseme hakuwa fowadi/mfungaji mzuri?
4. Tegete kabla ya leo, alikwishafunga magoli mangapi ya Ligi Kuu kwenye misimu miwili iliyopita? Ndiyo tuseme kabla ya hapo hakupata kuwa fowadi/mfungaji mzuri?
4. Ballotelli tangu aende Lverpool ameshinda magoli mangapi? Ndio tuseme sio fowadi/mfungaji mzuri?
5. Van Parse mwaka huu ameshafunga magoli mangapi? Ndio tuseme sio fowadi/mfungaji mzuri?
6. Unamkumbuka Ballack wa Ujerumani/Bayern Munich? Alifanya vizuri alipohamia Chelsea? Ndio tuseme hakuwa mchezaji mzuri kabla ya hapo? Veron je? Decco?
7. Unamkumbuka shevchenko akiwa A C Milan? Aliendelea na wimbi hilohilo la ufungaji alipohamia Chelsea? Ndio tuseme hakuwa fowadi/mfungaji mzuri kabla ya hapo?
Kuna visababishi (factors) vingi vinavyomfanya mchezaji mzuri kutoonekana mzuri, (ingawa binafsi bado naamini Jaja na Coutinho ni wazuri licha ya kuwa wamefunga goli moja moja tu hadi sasa - mbona Niyonzima, Salim Abubakar, hamis Mcha nk hawajafunga hadi sasa na hatuwasemi kuwa sio wazuri?): ugeni, ushikaji mafunzo ya mwalimu mpya kwake, imani yake kwa uchezeshaji anaouona, mazingira ya nje ya uwanja/timu/kambi, kuogopwa kunakolazimisha kuchungwa kupita kiasi hata kama kwa mbinu haramu, kite (tension) bahati, ushirikiano na wachezaji wengine, n.k.

Asante sana kaka kwa ufafanuzi mzuri. Nchi hii ndio maana hatuendelei ktk hili eneo soka. Waulize wanaofikiri tunawachezaji wazuri zaidi ya jaja na cotiunho watuambia tangu uhuru ni mchezaji gani alishapata bahati ya kucheza ligi soka duniani kama epl, serial A, La liga nk? Sisi tumejaa fitina ktk mpira na tunapenda matokeo mazuri bila kutoa jasho. Kila kitu ni fasta fasta bila kutoa jasho. Mchezo wa mpira ni team work kama wachezaji Yanga hawajaweza kuchezesha inavyotakiwa jaja na cotiunho itakuwa vigumu kuonesha vipaji vyao. Think of Thierry Henry alivyohamia Arsenal akitokea Juventus, msimu mzima hakuweza kuonesha kipaji cha mpaka msimu wa pili, mpaka pale alipozoeana na wenzake na baada kuwa tishio kwa epl.
 
Kwa coutinho sawa, lakini kwa jaja tumefeli, hilo tukubali...ni mchezaji ambaye anakabwa kwa urahisi, hana madhara sana akiwa na mpira, ni nzito kupita kiasi, ni rahisi kanguka bila sababu..kwa fawad ya jaja mimi sina imani nae hata kidogo..
 
Jaja amecheza mechi tano amefunga goli moja, Tegete amecheza mechi moja isiyozidi dk 30 amefunga goal mbili. Je nani mkali.
Ni vema pia kutambua kuwa UWEPO wa Jaja ni faida kubwa sana. Ndio maana unaona Tegete anapopata nafasi ya kucheza atahakikisha anafanya vema ili kudhihirisha yeye ni bora kuliko Jaja, '' USHINDANI WA NAMBA'''. Tegete alikuwa ameshabweteka na hata kushuka kiwango sana. Hii ndio dawa ya mtu mvivu na asiyejituma, mletee mtu wakushindana naye vinginevyo asugue bench.
Halafu nadhani ndani ya wachezaji wa yanga kuna KAROHO ka kwanini na wivu. Inawezekana wanaopewa majukumu yakumlisha mipira wakafanya FITINA za kimpira dhidi yake ili aonekane hafai. Ikumbukwe ujio wa kina Jaja na Continho umewafunika sana kina Ngasa, Tegete na wenzao, hivyo kwa hulika zetu ngozi nyeusi ni wazi hawafurahii kuona majina yao yanafunikwa na kina Jaja. Kinachobaki ni kufanya FITINA za uwanjani ambazo sio rahisi kuzibaini. Mechi ya ngao ya hisani kati ya Yanga na Azam ukiangalia utaona jinsi jaja alivyokuwa anapewa ushirikiano mkubwa sana na baada tu ya ile mechi ndio ikawa habari ya mjini. Jaja, Jaja. Hakuna cha ngasa, Tegete wala nani.

NADHANI JAJA NA CONTINHO WANGEKUWA AZAM WANGEFANYA VIZURI SANA. Azam hakuna SIASA kama Simba na Yanga. Azam wapo ki Professional zaidi
 
mpira kuna kufunga au kuchezesha wenzako sasa jaja anamambo yote akibanwa sana mtoa pasi mzuri sana lakini wajuaji wasiojua mpira wanasema jaja si mchezaji.

nawauliza nyinyi kama jaja hajui kwa nini mabeki pinzani wanamkaba watatux2?
 
Back
Top Bottom