Jaja, Countinho & Maximo

Jaja, Countinho & Maximo

Ni vema pia kutambua kuwa UWEPO wa Jaja ni faida kubwa sana. Ndio maana unaona Tegete anapopata nafasi ya kucheza atahakikisha anafanya vema ili kudhihirisha yeye ni bora kuliko Jaja, '' USHINDANI WA NAMBA'''. Tegete alikuwa ameshabweteka na hata kushuka kiwango sana. Hii ndio dawa ya mtu mvivu na asiyejituma, mletee mtu wakushindana naye vinginevyo asugue bench.
Halafu nadhani ndani ya wachezaji wa yanga kuna KAROHO ka kwanini na wivu. Inawezekana wanaopewa majukumu yakumlisha mipira wakafanya FITINA za kimpira dhidi yake ili aonekane hafai. Ikumbukwe ujio wa kina Jaja na Continho umewafunika sana kina Ngasa, Tegete na wenzao, hivyo kwa hulika zetu ngozi nyeusi ni wazi hawafurahii kuona majina yao yanafunikwa na kina Jaja. Kinachobaki ni kufanya FITINA za uwanjani ambazo sio rahisi kuzibaini. Mechi ya ngao ya hisani kati ya Yanga na Azam ukiangalia utaona jinsi jaja alivyokuwa anapewa ushirikiano mkubwa sana na baada tu ya ile mechi ndio ikawa habari ya mjini. Jaja, Jaja. Hakuna cha ngasa, Tegete wala nani.

NADHANI JAJA NA CONTINHO WANGEKUWA AZAM WANGEFANYA VIZURI SANA. Azam hakuna SIASA kama Simba na Yanga. Azam wapo ki Professional zaidi
Ningeweza kukubaliana na wewe, lakini hili la professionalism ya Azam, mmmhhhhhh....!
 
Back
Top Bottom