Jairo scandal na waraka namba 3 | JamiiForums | The Home of Great Thinkers

Dismiss Notice
You are browsing this site as a guest. It takes 2 minutes to CREATE AN ACCOUNT and less than 1 minute to LOGIN

Jairo scandal na waraka namba 3

Discussion in 'Jamii Intelligence' started by naivasha, Sep 14, 2011.

 1. n

  naivasha Member

  #1
  Sep 14, 2011
  Joined: May 13, 2011
  Messages: 94
  Likes Received: 2
  Trophy Points: 15
  Ndg wana jf poleni na pilikapilika.

  Gazeti la mwananchi toleo na 04096 la tarehe 13 septemba 2011 lilitoa mpya juu ya kashfa ya jairo kwamba kuna waraka unaokataza uchangishaji wa fedha. Mwananchi limetaja waraka huu kuwa ni waraka na. 3 kumb. Na. Tyc/a/400/620/18 wa mwezi machi 2011.

  Mi naomba mwana jf yeyote anitumie au auweke umu tuusome vema. Naamini kwa kinachoendelea watanzania tuna haki ya kujua. Kwa sababu viongozi wanaochangisha fedha kwa kazi zilizoko ndani ya bajeti siyo jairo peke yake. Ebu tujuzeni, tupeni mwanga tujue na tujadili.

  Naamini hili ni jukwaa muafaka. Asanteni
   
 2. kikahe

  kikahe JF-Expert Member

  #2
  Sep 18, 2011
  Joined: May 23, 2009
  Messages: 1,273
  Likes Received: 17
  Trophy Points: 135
  wakiweka nitarudi kusoma
   
 3. MJINI CHAI

  MJINI CHAI JF-Expert Member

  #3
  Sep 18, 2011
  Joined: Dec 12, 2010
  Messages: 1,809
  Likes Received: 588
  Trophy Points: 280
  Waraka unasema ni marufuku kuchangisha WANANCHI pasipo 1. wananchi wenyewe waridhie kwenye mkutano wa hadhara 2.makubaliano hayo ya uchangiaji upate kibali kutoka mamlaka yanayohusika..............................

  lakini swala la Jairo si la kuchangisha WANANCHI ni kuchangisha taasisi ndani ya wizara ambalo ni swala la MHIMILI MMOJA WA DOLA ndani ya serikali............

  Hivyo BUNGE letu lilitakiwa kujadili yatokanayo........then kushauri mapendekezo kwa Mhilili ambao Mwana Kondoo Jairo ni Boss wake............Na si kupinga Maamuzi ambayo MHIMILI MKUU umeyatoa bila kuangalia nani katoa.............Tusiwe doubleface waTZ..............serikali si MUCHEZO.....kuna mambo mengi ya kuumiza vichwa.......................

  JAIRO arudishwe kazini.....................Mnaing'ang'ania hii mada kulikoni.................acheni wivu, uroho, husda..............wakati ukifika utapata na wewe...................kila kitu kimepangwa...........


   
 4. mikatabafeki

  mikatabafeki JF-Expert Member

  #4
  Sep 18, 2011
  Joined: Dec 29, 2010
  Messages: 12,837
  Likes Received: 2,101
  Trophy Points: 280
  saaaafi huku limezuka hili huku hili................na bado tho no action will be taken jamba jamba inamtosha
   
 5. Mimibaba

  Mimibaba JF-Expert Member

  #5
  Sep 18, 2011
  Joined: Jul 1, 2009
  Messages: 4,566
  Likes Received: 7
  Trophy Points: 0
  Sikutegemea kuna watanzania wapuuzi kiasi hiki. Wewe ni kati yao ambao, hata nchi ikiuzwa unaona sawa ili mradi unalamba makombo
   
 6. Mwakalinga Y. R

  Mwakalinga Y. R Tanzanite Member

  #6
  Sep 18, 2011
  Joined: Oct 22, 2008
  Messages: 2,718
  Likes Received: 52
  Trophy Points: 145
  Katika watanzania wenye mawazo potofu na fikra hasi wewe ni mmojawao
   
 7. n

  naivasha Member

  #7
  Sep 19, 2011
  Joined: May 13, 2011
  Messages: 94
  Likes Received: 2
  Trophy Points: 15
  Mjini Chai katoa mawazo yake. Thats fine. Japo ameonekana hajui alisemalo.

  Kwa kuwa msemakweli ni Waraka Na. 3 ni vema ukawekwa bayana ili pumba na chuya ikajulikana. Naamini tukiuona wengi tutakuwa na msingi wa kuchangia.

  Tangu baadhi ya magazeti yaandike juu ya uwepo wa Waraka huo hakuna mamlaka yoyote iliyokanusha. Silence means what? Lkn tunajua kila Wizara ina bajeti yake kila mwaka na bajeti hiyo imejumuisha bajeti za kila idara. Sasa tupate msingi sasa wa wizara mama kuzichangisha taasisi zake. Pia tunafahamu mchakato wa bajeti unaanzia huko huko kwenye idara/taasisi za kila idara. Je, kuna kifungu katika idara/taasisi kinachoombewa fedha na kutengewa fedha kwa ajili ya kuichangia wizara au kuiwezesha bajeti yake kupita? Maswali ya kujiuliza ni mengi na watanzania wanahitaji majibu kulika shutuma. Hakuna mwenye wivu katika hili. Ebu tueleweshane.

  Watanzania tufahamu kwamba mambo ya namna hii yanapoibuliwa kumekuwa na ujanja wa kuyafukia na hatimaye kutufumba macho na masikio watanzania. Ujanja wa siku zote umekuwa ni kuunda tume au kamati za uchunguzi. Naam, tume na kamati hizi zmara nyingi zinaelekezwa cha kufanya au kupewa adidu za rejea rather than Tume au Kamati kujiandalia zenyewe Adidu za Rejea kwani The subject matter inakuwa wazi. Hivyo, hata kama tume au kamati itafanya vema lkn endapo matokeo ya uchunguzi ni tofauti na na anavyotaka mkubwa basi taarifa itaishiwa kuwekewa viraka au itawekwa kwenye shubaka na ndo unakuwa mwisho wa kila kitu.

  Hivyo, lazima ifike mahali watanzaania tuamke, kwanini masuala kama hayo ya kijinai yaundiwe tume wakati tuna vyombo vya dola vyenye mamlaka ya kisheria? Jambo la maana ni kuviagiza ili vichukue hatua. Lkn je mambo ya jina yanapoundiwa tume hatuoni kwamba ndo mwanzo wa kuvifumba macho vyombo vya dola? Asanteni sana wana JF.
   
 8. M

  MpendaTz JF-Expert Member

  #8
  Sep 21, 2011
  Joined: May 15, 2009
  Messages: 1,579
  Likes Received: 116
  Trophy Points: 160
  Uchambuzi wako ni sahihi kabisa na haya ndiyo madhara ya kuwa na katiba ambayo ni ya chama kimoja. Ni itikadi ya hicho chama iliyobatizwa na kuitwa Katiba ya nchi. Halafu kinachofuata ni Mkuu wa nchi anakuwa amelimbikiziwa madaraka ya kuchagua viongozi wote huwezi acha kuona mizengwe na mazingaombwe katika nchi.

  Majirani zetu Kenya wamepiga hatua abayo sisi itatuchukua miaka 50 kufikia, kuthubutu kutangaza hadharani nafasi ya jaji Mkuu wa nchi na Makamu wake na watu waka-apply na kuchekechwa hadharani. Hii hatua si ndogo maana yule jaji atahakikisha analitumikia taifa na siyo Chama tawala wala Mkuu wa nchi na si waziri wala Katibu wa chama!

  Mimi binafsi ninawapongeza sana.
   
 9. MJINI CHAI

  MJINI CHAI JF-Expert Member

  #9
  Sep 27, 2011
  Joined: Dec 12, 2010
  Messages: 1,809
  Likes Received: 588
  Trophy Points: 280
  Ni uvivu wako wa kufikiri ndio unaokufanya kupayuka bila Tafakuri ya kina.............Rejea kwenye Mihimili mikuu ya Nchi Kazi zake, mipaka yake na mahusiano yake na mihimili mingine..............Una Mdomo 'MCHAFU'.........
   
 10. MJINI CHAI

  MJINI CHAI JF-Expert Member

  #10
  Sep 27, 2011
  Joined: Dec 12, 2010
  Messages: 1,809
  Likes Received: 588
  Trophy Points: 280
  Hebu eleza mawazo pevu na fikra chanya tuyaone.......Tatizo la wengi wenu ni Bendera fuata upepo hamtafakari.............Je Wabunge wanayo haki ya kuingilia maamuzi ya Mhimili mwingine wa serikali?.............Je? ikitokea ukaambiwa kuwa ulikuwa ni mpango wa kuvunja Baraza la mawaziri ambao uliandaliwa na wasioitakia mema nchi yetu utasemaje?............... Si kila kitu kitamu mdomoni ni chakula kingine ni SUMU.......Hiiiiiiiiiiiiiiiiiiiiiiiiiiiiiiiiiii ni JF ni zaidi ya Forum nyingine...........think........ think...... think........
   
 11. n

  naivasha Member

  #11
  Sep 27, 2011
  Joined: May 13, 2011
  Messages: 94
  Likes Received: 2
  Trophy Points: 15
  aWana JF, Kweli TECHMAN ana matatizo siyo utani! Lakini kabla ya kusaidiwe naye awe tayar kuupokea msaada vinginevyo ataendelea kulia aghhhhhhhhhh!. Anadai anatumia mavioo yake ya kuweka machoni. Mi kwa kumsaidia mavioo asiyaweke machoni atajipofusha bure!!!!!!!!!
   
 12. W

  We acha tu New Member

  #12
  Oct 15, 2011
  Joined: Aug 1, 2011
  Messages: 3
  Likes Received: 0
  Trophy Points: 0
  Tuoneshwe waraka unasema nini tujadili kwa pamoja tuache mawazo ya MTZ huyu ambaye pengine kutokana na mtizamo wake anaona yeye ni suala la wivu, tusikatae mawazo yake, ila ipo siku na yeye atakubaliana na mawazo ya walio wengi katika nchi hii...Jairo bye bye hata nafasi ambayo JK alikuwa mpe ya kuwa Katibu Kiongozi imeota mbawa!

  Mwenye waraka jamani auweke hapa tuuone maana wadanganyika sisi hatujui kitu ndiyo maana nikitokea twapiga kelele ikipita mwezi tumesahau makubwa sijui nani atatutoa humu
   
 13. Nico1

  Nico1 JF-Expert Member

  #13
  Oct 15, 2011
  Joined: Mar 18, 2011
  Messages: 746
  Likes Received: 138
  Trophy Points: 60
  Wewe unayejiita baba yawezekana ulikuwa mmoja wa wale vbaraka waliopewa kazi ya kusukuma gari la rafiki yako jairo bila aibu na li suti lako naona unamachungu.
   
 14. Bigjahman

  Bigjahman JF-Expert Member

  #14
  Oct 15, 2011
  Joined: Jan 5, 2011
  Messages: 644
  Likes Received: 86
  Trophy Points: 45
   
 15. N

  NewOrder JF-Expert Member

  #15
  Oct 15, 2011
  Joined: Apr 11, 2011
  Messages: 489
  Likes Received: 73
  Trophy Points: 45
  Mjini Chai, nina hakika unaweza kujifunza kufikiri kwanza kabla ya kuuliza maswali. Kati ya matatizo tuliyonayo katika nchi yetu ni, "yaliyopita si dwele, tugange yajayo". Na mmoja wa waumini wa hilo ni wewe. Inashangaza hata hujui kuwa ni Bunge ndilo hutunga sheria, ni Bunge hupitisha bajeti na ninadhani hujui kuwa ni Bunge linaweza kumwondoa Rais (mkuu wa nchi na serikali ya Tanzania).

  Kama watu wanahoji Richmond/Dowans ya 2006, kwanini wasihoji jambo la 2011. Jambo kuu la topic ilikuwa ni kuweka jamvini barua husika. Sio kubishania uwepo wa mada hii wala mantiki ya mwandishi!!
   
Loading...