Jahazi imezama wakati ikielekea Mafia kutoka Kisiju

chongoe

JF-Expert Member
Mar 22, 2019
1,128
2,717
Habari zenu wakuu

Kwanza nawashukuru kwa wale wote walionipa ushauri, kwa sasa nipo vizuri nimeachana na mawazo ya kufakufa.

Kuna jambo limetokea na mpaka sasa hakuna taarifa ya hawa watu wako wapi. Kuna jahazi imetokea Kisiju ikalala kisiwa cha Koma. Siku ya pili ikatoka Koma kuelekea Mafia (namaanisha Leo Jumanne asubuhi)

Kwa habari zilizopo mpaka sasa wamezama sababu kulikuwa na boti ilikuwa ikivinjari maeneo ya bahari ndipo wakaona ishara ya kuombwa msaada baada ya wenye jahazi kuwapungia wakitaka msaada. Boti wakati inaenda kuwasaidia ndio ile jahazi imezama mazima ikiwa na watu wanaofikia sita mwanamke akiwemo.

Binafsi katika hao sita ndugu zangu wapo watatu na mpaka sasa hawajaonekana wamezama kati ya Nyororo na mkondo
wa Nyara.

Taarifa zaid nitawajuza

NB: Picha haihusiani na ajali ya leo

======

Jahazi, Mashua ya Mizigo iliyokuwa Ikitoka Kisiju kuelekea Kilindoni Mafia. Mashuhuda wanadai Mashua hiyo ilikuwa na Wafanyakazi watano.

Inadaiwa hapakuwa na upepo mkali wa kuzamisha Jahazi hivyo wanahia inawezekana Jahazi ikawa imegonga Fungu(sehemu ya Mchanga) au ikawa imegonga Mwamba.

Ashuhuda wanadai Jahazi lilizama saa tatu asubuhi, lilikuwa limepakia Cement. Kati ya Watano waliozama, Wawili wamepatikana, watatu bado hawajapatikana.

Waliopatikana wakiwa hai ni:

1. Haji Salum Mkazi wa Kisiju na Mafia
2. Msiwao Mkazi wa Mafia.

Ambao hawajapatikana ni;

3. Hanifa Mohamed Mkazi wa Mafia
4. Ally Omary Mkazi wa Mafia
5. Saidi Mkazi wa Mafia
 
Tanzania kubwa Sana,,

Poleni sana

Naomba muhame huko maana kwa style ya usafiri huo ni kama kuishi jangwani kipindi Cha mvua.
 
Poleni sana ..
Vipi Boti haikuwa na vifaa vya kujiokolea.
Mkuu kwenye Jahazi au Mashua suala la vifaa vya kujiokolea ni kitendawili. Humo ukikuta life jacket basi ni machache na yamechoka sana.

Kama ni msafiri unajali usalama bora uwe nalo binafsi.
 

Similar Discussions

Back
Top Bottom