Abdul Said Naumanga
JF-Expert Member
- Jan 28, 2024
- 745
- 1,470
Kumekua na malalamiko na mijadala juu ya uwepo wa utitiri wa raia wa kigeni, hususan Wachina, katika baadhi ya biashara, especially zile ndogondogo hadi zile za kati hasa katika maeneo ya Dar Es Salaam, na hata masokoni ya mikoani. Wengi wamehoji namna wageni hawa wanavyoingia sokoni kwa nguvu ya mitaji mikubwa, miundombinu ya kisasa na mtandao wa kiusafirishaji kutoka China, huku wakishindana moja kwa moja na wafanyabiashara wazawa katika sekta ambazo hazihitaji teknolojia ya hali ya juu, kama uuzaji wa bidhaa rejareja, vipuri, saluni, usafi na ujasiriamali wa kawaida. Sauti za malalamiko haya zimekuwa zikipazwa si tu na wafanyabiashara, bali hata viongozi wa jumuiya za biashara, na hatimaye serikali imeamua kuchukua hatua.
Mnamo tarehe 25 Julai 2025, Waziri wa Viwanda na Biashara, Dk. Selemani Jafo, alitoa amri ya kuzuia raia wa kigeni kujihusisha na baadhi ya biashara “The Business Licensing (Prohibition of Business Activities for Non-Citizens) Order, 2025”
Katika amri hiyo, biashara 15 zimepigwa marufuku kufanywa na raia wa kigeni. Biashara hizo ni pamoja na:
Mnamo tarehe 25 Julai 2025, Waziri wa Viwanda na Biashara, Dk. Selemani Jafo, alitoa amri ya kuzuia raia wa kigeni kujihusisha na baadhi ya biashara “The Business Licensing (Prohibition of Business Activities for Non-Citizens) Order, 2025”
Katika amri hiyo, biashara 15 zimepigwa marufuku kufanywa na raia wa kigeni. Biashara hizo ni pamoja na:
- kuuza bidhaa rejareja (isipokuwa supermarket),
- uhamishaji wa pesa kwa simu,
- urekebishaji wa simu na vifaa vya kielektroniki,
- saluni (isipokuwa ndani ya hoteli au kwa utalii),
- usafi wa mazingira,
- ununuzi wa mazao mashambani,
- biashara ya vibeti na maduka ya vitu vya kale,
- biashara za uwakala na udalali,
- uchimbaji mdogo wa madini
- na nyingine nyingi zinazogusa ujasiriamali wa kawaida wa Mtanzania.
Amri hii imepokelewa kama hatua ya kulinda uchumi wa ndani, ajira na mazingira ya ushindani wa haki. Lakini pia amri hii pia imetengeneza makosa ya jinai na adhabu zake kupitia kifungu cha 3(3). amri hiyo inasema kuwa raia wa kigeni akikiuka marufuku atatozwa faini isiyopungua shilingi milioni 10 au kifungo cha hadi miezi sita, huku Mtanzania anayemsaidia akifungwa hadi miezi mitatu au kulipa faini ya milioni tano.