Iweje waliotulia hawaolewi, aolewe huyu asiyetulia?

Iweje waliotulia hawaolewi, aolewe huyu asiyetulia?

mmewadadako

JF-Expert Member
Joined
Mar 29, 2019
Posts
534
Reaction score
850
Si mara zote uhusiano wa ndoa ni matokeo ya upendo kama inavyotarajiwa. Yapo mahusiano mengi tu ya ndoa ambayo kimsingi ni arrangements za watu kujipatia mahitaji mengine kabisa yasiyohusiana na mapenzi. Katika uzi huu, najaribu kuonesha kwamba si kila mwanamke aliyeolewa maana yake ni kuwa anafaa na kadhalika, si kila asiyeolewa hafai.

Sababu za wanaume kuoa hazifanani

Si mara zote uhusiano wa ndoa ni matokeo ya upendo kama inavyotarajiwa. Yapo mahusiano mengi tu ya ndoa ambayo kimsingi ni arrangements za watu kujipatia mahitaji mengine kabisa yasiyohusiana na mapenzi. Ndoa zimeanza kuwa 'fursa' za kujinufaisha kibinafsi na zinameanza kupoteza dhana halisi ya mahusiano. Ndoa zimeanza kuchukuliwa kirahisi kama ubunge na udiwani unaopatikana hata kama huwapendi wapiga kura.

Wapo watu huoa ili waweze kupata uhamisho wa kikazi ‘kumfuata mwenzi’. Wapo wanaooa fedha na elimu na hawafikirii kingine chenye maana 'takatifu' ya ndoa. Wengine wanaoa kupata ‘watumishi wa ndani’ watakaosaidia kupika, kufua, kusafisha nyumba na kadhalika. Wengine wanawachukulia wanawake kama ‘viwanda’ vya kuwazalia watoto. Wapo wanaooa ili kupata ‘heshima’ ya marafiki au jamii kwamba jamaa siku hizi kaoa. Wanataka kufikia matarajio ya wengine. Zote hizo ni ndoa na zaweza kuwa halali.

Kwa hiyo tunaweza kusema kwa hakika, wapo wanaume tena wengi tu huoa si kutafuta utoshelevu wa kihisia kwenye ndoa. Hawana habari na kujua na kujibu mahitaji ya mwenzi na wala hawafikirii namna ya kuwekeza kwenye ndoa ili kadhalika waweze kupata mahitaji ya kihisia. Badala yake, ndoa kwao ni nyenzo ya kujipatia 'raslimali watu' itakayowafaa kwa shughuli nyinginezo, wakijua kuwa mahitaji yao ya kihisia watayakidhi kupitia michepuko.

Si kila anayeolewa ni ‘wife material’

Kwanza haiwezekani kila mwanamke awe wife material. Tofauti ya malezi, imani, mitazamo na mambo mengine kibao, kama usawa wa kijinsia unaopiganiwa siku hizi, vyote hivyo vimewafanya wanawake wasikidhi vigezo vya kuoleka achilia mbali kuolewa kwa sababu ya kuwa na sifa za kuolewa.

Na kama tulivyoona katika aya zilizopita, yapo mazingira ya kutosha kuwafanya wanawake kuolewa kwa sababu nyinginezo nje ya ‘kuwa na sifa za kuolewa’. Pengine wanacho kile kinachotafutwa na baadhi ya wanaume wanaojali ‘mengineyo’ zaidi ya upendo. Hivyo wanaolewa kama bidhaa, vitu, viwanda, wafanya kazi na kadhalika.

Ndio maana unaweza kushangaa wanawake wajeuri, wazinzi, wababe, wasiopenda kwa dhati, bado wanaweza kuolewa kwa sherehe kubwa tu. Kwa nini? Ni kwa sababu wanaume wanaowaoa wanaotafuta bidhaa. Kwa wanaume wa jinsi hii wala usishangae wanawake wenye nidhamu, unyenyekevu na maadili wakaonekana si lolote.

Umejiwekea mazingira ya kukutana na ‘waoaji’?

Kwa upande mwingine, wapo wanawake wazuri, werevu, waadilifu, waaminifu na kila aina ya sifa njema hawaoelewi. Pamoja na sababu nyinginezo, huenda hawajajiweka katika mazingira ya kuonana na waoaji! Tulisema huko nyuma watu huhusiana na wale wanaowajua. Kadri unavyoonana na watu ndivyo wanavyokujua na vetting yao kwako unaweza kuzaa matokeo.

Sasa kama mwanamke kwa sababu moja au nyingine haonani na watu, iwe kwa aibu, kazi nyingi, dharau na kadhalika, inaweza kumwia vigumu sana kuonekana. Kujenga urafiki unaoweza kuelekea kwenye mahusiano serious kunaanzia kwenye kukutana. Hukutani na watu, hata kama unafaa, unajiharibia mwenyewe na baadae unalalamika 'huna bahati'.

Wengine pamoja na uzuri na ‘utakatifu’ walionao, hawajijengei taswira nzuri kwa wanaume ‘waoaji’. Chukulia mfano wanawake wabishi, wenye majigambo, wasiojua kusikiliza, wanaoamini wanajua kila kitu, watetezi wa usawa wa kijinsia uliozidi mipaka na kadhalika. Hawa hata kama wanao uzuri wa nje, wanaweza kujikuta wakiwa ‘bidhaa’ ya wanaume wakora wanaotafuta michepuko na sio mahusiano ya kudumu. Na wakiolewa, hujikuta wakiangukia kwenye kundi la wanaume wanaowachukuliwa wanawake kuwa njia ya kufikia malengo yao mengine ya kimaisha.

Ndio kusema, si kila mwanamke anayeolewa basi ni mwadilifu, na si kila asiyeolewa hafai. Kinachogomba ni umeolewa kwa sababu gani? Umependwa kwa sababu mwanaume anaamini unaweza kujibu mahitaji yake ya kihisia, au umeolewa kama nyenzo ya mwanaume huyo kufikia malengo yake mengine ya kimaisha? Je, hujaolewa kwa sababu hufai, au umeshindwa kujikutanisha na wanaume ‘waoaji’ na kuwathibitishia unavyoweza kujibu mahitaji yao ya kihisia?

Si kila aliyeolewa, ameolewa kwa bahati na mipango ya 'mungu’. Kadhalika kwa wasioolewa.
 
Mwanamke ambae hajatulia (Mwenye wanaume wengi) ana nafasi kubwa ya kuolewa kuliko ambaye ametulia. Hii ni kwasababu,wasichana ambao wametulia kwanza wanachelewa kuanzisha mahusiano...anakaa na bikra yake weeee. 2 Akianzisha anakuwa na mtu mmoja pengine kwa muda mrefu...ikitokea huyo mtu hajamua, anachukua yena muda mrefu kuanzisha mahusiano mengine mwisho wa siku anajikuta umri umeenda.

Lakino yule mwenye wanaume wengi, anakuwa ana nafasi kubwa ya kuolewa kwa sababu kati ya wanaume watatu au wawili alionao mmoja anaweza kumuoa. Akiona hawaeleweki anapiga chini fasta na kuanzisha mahusiano na wengine hivyo kujiongezea nafasi ya kuolewa.
 
Haya mambo tumwachie mungu hiyo imani inatosha.
1: Siku moja mm, boss wangu na secretary tulipiga story sana ni mtu mzima alioa majuzi tu uzeen sijui kwa nini wakati ana uwezo alinambia hivi, luckyline wadada kama wewe chances za kuolewa ni mdogo sana nikamuuliza kwa nini? Akajibu, "yo too real and innocent." Akaongeza sometimes fake fake life, akaniukiza hivi wewe ulishawahi kuumuumiza mwanaume hata kwa kumchaganganya na mwanaume mwingine? Ni kasema hapana😂😂😂 akadakia secretary mm mwanaume akizingua leo kesho Nina mwingine😀😀😀
Na ni kweli huyu Dada sijui haogopi? Yaani yeye kuja na mwanaume mpya ofisini akamtambulisha ni kitu cha kawaida. Akaniuliza hivi wewe luckyline unaweza je kulala peke yako miaka hivyo yote? Unawezake mshahara wako kujilipia kodi ya nyumba? Na wanaume kazi yako ni nn? Nikamjibu akinilipia kodi si atataka kuja kwangu wakati mm sipendi waje kwangu? Akajibu si unahama akileta vurugu. Nilichoka.

Mimi hapa ninapoishi ni mwaka wa 5sijawahi hama ila yeye hawezi kumaliza miezi 6 sehemu mwanaume akimletea vurugu. Akipata mpya anamlipia kodi wanahama. Mm haya maisha siyawezi sipendi kurupushani na kuendeshwa na mwanaume ambae hajanioa. Huyu binti na mikikimikiki aliyonayo full kubadilisha wanaume yeye hana stress she is happy. Kweli dunia haiko fair.
 
Mwanamke ambae hajatulia (Mwenye wanaume wengi) ana nafasi kubwa ya kuolewa kuliko ambaye ametulia. Hii ni kwasababu,wasichana ambao wametulia kwanza wanachelewa kuanzisha mahusiano...anakaa na bikra yake weeee. 2 Akianzisha anakuwa na mtu mmoja pengine kwa muda mrefu...ikitokea huyo mtu hajamua, anachukua yena muda mrefu kuanzisha mahusiano mengine mwisho wa siku anajikuta umri umeenda.

Lakino yule mwenye wanaume wengi, anakuwa ana nafasi kubwa ya kuolewa kwa sababu kati ya wanaume watatu au wawili alionao mmoja anaweza kumuoa. Akiona hawaeleweki anapiga chini fasta na kuanzisha mahusiano na wengine hivyo kujiongezea nafasi ya kuolewa.
huu ndio ukweli usio pingika
 
Hahahaha
 
Haya mambo tumwachie mungu hiyo imani inatosha.
1: Siku moja mm, boss wangu na secretary tulipiga story sana ni mtu mzima alioa majuzi tu uzeen sijui kwa nini wakati ana uwezo alinambia hivi, luckyline wadada kama wewe chances za kuolewa ni mdogo sana nikamuuliza kwa nini? Akajibu, "yo too real and innocent." Akaongeza sometimes fake fake life, akaniukiza hivi wewe ulishawahi kuumuumiza mwanaume hata kwa kumchaganganya na mwanaume mwingine? Ni kasema hapana[emoji23][emoji23][emoji23] akadakia secretary mm mwanaume akizingua leo kesho Nina mwingine[emoji3][emoji3][emoji3]
Na ni kweli huyu Dada sijui haogopi? Yaani yeye kuja na mwanaume mpya ofisini akamtambulisha ni kitu cha kawaida. Akaniuliza hivi wewe luckyline unaweza je kulala peke yako miaka hivyo yote? Unawezake mshahara wako kujilipia kodi ya nyumba? Na wanaume kazi yako ni nn? Nikamjibu akinilipia kodi si atataka kuja kwangu wakati mm sipendi waje kwangu? Akajibu si unahama akileta vurugu. Nilichoka.

Mimi hapa ninapoishi ni mwaka wa 5sijawahi hama ila yeye hawezi kumaliza miezi 6 sehemu mwanaume akimletea vurugu. Akipata mpya anamlipia kodi wanahama. Mm haya maisha siyawezi sipendi kurupushani na kuendeshwa na mwanaume ambae hajanioa. Huyu binti na mikikimikiki aliyonayo full kubadilisha wanaume yeye hana stress she is happy. Kweli dunia haiko fair.
Na ndyo ukweli wanawake wanaoruka ruka mara nyingi ndyo wanakuwa na furaha sana kuliko Yule anayetulia na mwanaume mmoja Kwa kipindi kirefu mm na mwambiaga mchepuko wangu[emoji23][emoji23][emoji23] ili uishi na furaha lazima uchague kulia au kucheka ukitaka kulia tulia na mmoja ukitaka kucheka na kufurahia maisha vuruga Yule anayekuvuruga hutajutia maishani na utapata umtakaye siyo anayekutaka
 
Back
Top Bottom