- Source #1
- View Source #1
Kuna taarifa zisizo lasim kwamba Raisi wa Ivory Coast kapinduliwa na haijulikana alipo, Sasa sijapatavtaarofa rasimi. Huenda Wafaransa wamefanya yao huko.
- Tunachokijua
- Madai
Mei 21, 2025 zilizuka taarifa katika mitandao mbalimbali ya kijamii zikidai kuwa kuna mapinduzi yametokea nchini Ivory Coast.
Mtumiaji mmoja wa mtandao wa X aliandika โBREAKING NEWS โThere's a coup d'รฉtat going on currently in Ivory Coast. Abidjan is burning. Alassane Ouattara the French puppet President of Cรดte d'Ivoire has either been killed yesterday or has flee the country. GOD is busy freeing Africa from the sheckles of oppressionโ akimaanisha kuwa;
โkuna mapinduzi ya kijeshi yanaendelea nchini Ivory Coast, Abdijan inawaka moto
Rais wa Cรดte d'Ivoire, Alassane Ouattara, ambaye ni kibaraka wa Wafaransa, ama ameuawa jana au amekimbia nchi.
MUNGU yuko kazini kuiweka Afrika huru kutoka kwenye minyororo ya uonevuโ
Uhalisia wa madai hayo
JamiiCheck imefuatilia madai hayo na kubaini kuwa si ya kweli. Hakuna chanzo chochote cha kuaminika kilichochapisha taarifa hiyo ya mapinduzi ya kijeshi huko Ivory Coast.
Rais wa Ivory Coast Outarra alionekana amehudhuria baraza la mawaziri katika makazi ya Rais Mei 21, 2025. Ukurasa wa Facebook wa Rais wa Ivory Coast ulipost taarifa iliyosomeka โRais wa Jamhuri, Alassane Ouattara, aliongoza Baraza la Mawaziri siku ya Jumatano, Mei 21, 2025, katika Ikulu ya Jamhuriโ.
Tovuti ya baraza la Ulaya Mei 21, 2025 iliripoti kuwa Rais wa Baraza hilo atakwenda nchini Ivory Coast ambapo atapewa tuzo ya UNESCO lakini pamoja na mambo mengine atakutana na Rais wa taiafa hilo, Ouattara. Baadhi ya maneno yaliyosomeka kwenye taarifa hiyo ni;
โRais wa Baraza la Ulaya, Antรณnio Costa, atasafiri kwenda Abidjan, Cรดte d'Ivoire kupokea Tuzo ya Amani ya UNESCO Fรฉlix Houphouรซt-Boigny tarehe 22 Mei 2025.
Pamoja na hafla hiyo, atakutana pia na Rais wa Cรดte d'Ivoire, Alassane Ouattara, kujadili mahusiano ya pande mbili, utulivu wa kikanda, na maandalizi ya mkutano ujao wa kilele kati ya Umoja wa Ulaya na Umoja wa Afrika utakaofanyika baadaye mwaka huuโ.
Ukurasa wa Facebook wa Rais wa Ivory Coast ulichapisha taarifa kuelezea ajenda ya Rais wa nchi hiyo kwa siku ya Alhamisi Mei 22, 2025, saa 4:00 asubuhi ni kuhudhuria Sherehe ya Kiheshima ya Tuzo ya Fรฉlix HOUPHOUรT-BOIGNY โ UNESCO kwa Ajili ya Utafutaji wa Amani.