IVI kwanini wanaume ni waoga kuoa | JamiiForums | The Home of Great Thinkers

Dismiss Notice
You are browsing this site as a guest. It takes 2 minutes to CREATE AN ACCOUNT and less than 1 minute to LOGIN

IVI kwanini wanaume ni waoga kuoa

Discussion in 'Mahusiano, mapenzi, urafiki' started by Tabutupu, Sep 13, 2012.

 1. Tabutupu

  Tabutupu JF-Expert Member

  #1
  Sep 13, 2012
  Joined: Nov 26, 2010
  Messages: 5,650
  Likes Received: 4,412
  Trophy Points: 280
  1. wanaume wanapenda uhusiano wa kirafiki, wa kumaliza haja yake aende kwake.
  2. wanapenda wakiwa na uhitaji wa ile kitu basi iwepo njia rahisi ya kuipata, kama kutafuta mwanamke na kushiba.
  3. inapo tokea mwanamke serious anae taka kuolewa, ndoo utajua neno kupenda linalo toka kinywani mwa mwanaume ni kitu kingine.
  4. kama wanawake wasinge saidia hili, ni wanaume wachache sana wangeoa.

  swali. kwanini wanaume wanaogopa sana to commit themselves kwa dnoa?
   
 2. Preta

  Preta JF-Expert Member

  #2
  Sep 13, 2012
  Joined: Nov 28, 2009
  Messages: 24,113
  Likes Received: 3,037
  Trophy Points: 280
  twende taratibu hapa.....unawaongelea wanaume kama wanaume.....au wanaume kama wavulana......?
   
 3. m

  mossad Member

  #3
  Sep 13, 2012
  Joined: Mar 20, 2009
  Messages: 63
  Likes Received: 0
  Trophy Points: 0
  ..............nadhani wengi wanaogopeshwa na kuongezeka kwa spidi ya wanawake wanaopenda sana kuolewa. wengi wa wanawake siku hizi mkianza relation wiki mbili tu utasikia ''unanioa lini?''. Simaanishi kuwa wanawake wote wana kajitabia haka ndo maana wapo pia wanawake wengi wanaoolewa wenye kujua nini maana mapenzi, ndoa na kuishi na mwanaume.
   
 4. Kiranga

  Kiranga JF-Expert Member

  #4
  Sep 13, 2012
  Joined: Jan 29, 2009
  Messages: 34,607
  Likes Received: 6,197
  Trophy Points: 280
  Kwa nini unafikiri kutotaka kuoa ni lazima kuendane na woga?

  Inawezekana wanaooa ndo waoga, wanaogopa jamii.

  Na wasiooa ndo hawaogopi kusemwa, kuvunjiwa heshima kwamba hawajaoa, kuwekewa maswali uanaume wao etc.
   
 5. N

  Neylu JF-Expert Member

  #5
  Sep 13, 2012
  Joined: May 28, 2012
  Messages: 2,650
  Likes Received: 24
  Trophy Points: 135
  Spidi ya wanawake wanaopenda kuolewa inatokana na spidi ya wanaume waongo kuongezeka.. Ndio maana bi dada inabidi aulize unanioa lini? Wanaume wa siku hizi wanapenda kumega na kukimbia... Wengi wao sio waoaji kama mleta maada alivyosema..
   
 6. Lizzy

  Lizzy JF-Expert Member

  #6
  Sep 13, 2012
  Joined: May 25, 2009
  Messages: 22,224
  Likes Received: 244
  Trophy Points: 160
  Wanaume wanaogopa zaidi wanawake wanaotamani sana ndoa kuliko kuogopa ndoa zenyewe.

  Mwanamke akianza kuitaka/omba/lazimisha sana ndoa mwanaume anashtuka,anasema hayuko tayari alafu anakimbia. Mwanaume huyo huyo anaweza akakutana na mwanamke mwingine na ndani ya muda mfupi akaanza YEYE kuongelea ndoa na kufanya kweli kabisa. Hapo inawezekana kwamba mwanaume hakuwa amempata anayeona anamfaa kwa zaidi ya kuburudishana weekend au aliogopa uhitaji wa mwanamke kuhusu ndoa asije akajitia kitanzi kwa mtu ambae anachotaka ni kuolewa bila kujali na nani/kwa sababu zipi n.k
   
 7. Kongosho

  Kongosho JF-Expert Member

  #7
  Sep 13, 2012
  Joined: Mar 21, 2011
  Messages: 36,126
  Likes Received: 303
  Trophy Points: 160
  kwani hizi ndoa zote nazoziona ni wa kike alone??
   
 8. lara 1

  lara 1 JF-Expert Member

  #8
  Sep 13, 2012
  Joined: Jun 10, 2012
  Messages: 15,444
  Likes Received: 10,123
  Trophy Points: 280
  Uwoga wao ni kukwepa majukumu tu, we mwambie mwanaume una TRUST FUND muoane mbona fasta tu! Wanaume ukiwa unawategemea mbona usiulize harusi!
   
 9. Tabutupu

  Tabutupu JF-Expert Member

  #9
  Sep 13, 2012
  Joined: Nov 26, 2010
  Messages: 5,650
  Likes Received: 4,412
  Trophy Points: 280
  Hata walioko kwenye ndoa, hawataki wake zao wa ndoa, utasikia wanasingizia chochote kile ile wale ma house girls. hata mke awe na penzi kubwa kiasi gani bado hawa vidume watataka kutest nje.
   
 10. Tabutupu

  Tabutupu JF-Expert Member

  #10
  Sep 13, 2012
  Joined: Nov 26, 2010
  Messages: 5,650
  Likes Received: 4,412
  Trophy Points: 280
  Hizo ni za wale wanawake waliowasadia wanaume wao wakubali kuwaoa. mwanaume siku zote ni kama toto fulani jeuri, lisilo taka kula hadi kwa fimbo.
   
 11. m

  mossad Member

  #11
  Sep 13, 2012
  Joined: Mar 20, 2009
  Messages: 63
  Likes Received: 0
  Trophy Points: 0
  Uyasemayo sio kweli neylu, hata hao wanaume unaowaongela hapo sio wanaume bali ni vivulana kama preta alivyosema hapo awali kwenye mchango wake. Kama hao wanawake wanataka kuolewa na vivulana basi wajue wataendelea kudanganywa hivyo hivyo hadi siku ya mwisho, vivulana vyenyewe vinategemea sabuni, hela ya vocha, nguo n.k kutoka kwa wazazi, atapata wapi uwezo na ujasiri wa kuoa? Cha msingi dada zetu tulieni muwapo kwenye mahusiano na wanaume ambao mna uhakika kweli wapo commited, habari ya ndoa hufuata baadae na sio kunilazimisha nikuoe, lazima nitajiuliza kunani hapa huyu mdada anataka kuficha nini nisikijue fasta kutoka kwake?
   
 12. N

  Neylu JF-Expert Member

  #12
  Sep 13, 2012
  Joined: May 28, 2012
  Messages: 2,650
  Likes Received: 24
  Trophy Points: 135
  Mmmh... Mie hapa siongelei hivyo vivulana ndugu, naongelea wanaume wenye kuanzia 32 and above.... Wenye kazi zao na maisha yao..! Ila Kama definition yako ya vivulana ni kwenye hiyo miaka niliyoitaja, itanibidi niwe mpoleee...
   
 13. Cynic

  Cynic JF-Expert Member

  #13
  Sep 14, 2012
  Joined: Jan 5, 2009
  Messages: 5,154
  Likes Received: 628
  Trophy Points: 280
  wavulana ni subset ya wanaume. na wanaume wengi tu (mimi mmoja wao) wanaoa/walioa wakiwa wavulana
   
 14. m

  mzabzab JF-Expert Member

  #14
  Sep 14, 2012
  Joined: Aug 18, 2011
  Messages: 6,981
  Likes Received: 585
  Trophy Points: 280
  simply put women luk for the security that marrige provides. unfortunately that security for now means having cash which alot of men have found out is the key to getting women to open their legs.
   
 15. m

  mzawahalisi JF-Expert Member

  #15
  Sep 14, 2012
  Joined: Jan 11, 2010
  Messages: 744
  Likes Received: 56
  Trophy Points: 45
  ujue hatujapata wa kuoa. Tofauti iko hapa, mwanamke yupo tayari kuolewa na yeyote yule hata kama haja mpenda ilimradi anaweza kumuhudumia, na mwanaume anaangalia nani atamfaaa kwenye kifungo cha maisha. amini nakwambia mwanaume asipompata Mwanamke anaye stahili akajikuta ameangukia kwa gumegume, basi maisha yake ni mafupi na machungu sana hapa duniani.
  Bilashaka ukiona sielekei kukuoa ujue hujatimiza vigezo.
   
 16. Columbus

  Columbus JF-Expert Member

  #16
  Sep 14, 2012
  Joined: Nov 5, 2010
  Messages: 2,010
  Likes Received: 22
  Trophy Points: 135
  Muulizeni Zitto swali hilo, halafu pamoja na woga wote huo anataka tumchague awe raisi wetu! pfuuuu hilo litakuwa ni kosa lingine kwa watanzania.
   
 17. fazaa

  fazaa JF-Expert Member

  #17
  Sep 14, 2012
  Joined: May 20, 2009
  Messages: 2,986
  Likes Received: 11
  Trophy Points: 0
  Inawezekana wanawake wasiku hizi mnatisha :biggrin1:
   
 18. Shark

  Shark JF-Expert Member

  #18
  Sep 14, 2012
  Joined: Jan 25, 2010
  Messages: 20,139
  Likes Received: 7,391
  Trophy Points: 280
  Wa kuolewa wenyewe wapo basi!!???

  Wao wanawaza zaidi lile tendo la kuolewa ili nao wasidharaulike, but majukum ya ndoa hawako tayari kwayo.

  Unataka nikuoe wakati kupika hujui, nguo unafuliwa na housegirl, n.k.

  Mtasubiri sana kwa kweli!!!
   
 19. Tabutupu

  Tabutupu JF-Expert Member

  #19
  Sep 14, 2012
  Joined: Nov 26, 2010
  Messages: 5,650
  Likes Received: 4,412
  Trophy Points: 280
  Hilo nalo neno
   
Loading...