ivi kitanda umekumbuka kutandika leo?

I hope wewe sio kakangu wa mfaranyaki!
Sheria ya kwetu, na naishika hadi leo: hakuna kwenda kususua b4 hujatandika kitanda. Na j1 ni usafi wa wiki hadi uvungu unadekiwa!
Siwezi ingia bafuni kuoga kabla sijatandika kitanda! nilifundishwa na Mama yangu tangu nikiwa darasa la 3 kuwa nimarufuku kuingia bafuni subui kabla hujatandika kitanda na hii alikuwa anatufanyia watoto wake wote wakike kwa wakiume.
 
Mi mme wangu ndo huwa anawahi kuamka kitandani na kuniacha nimelala - kutokana na ratiba na umbali wa kazini kwake. So nikikumbuka nitakitandika, otherwise hadi arudi jioni. Kwahiyo si siri hata mimi kwangu ni kama kwa shemeji yako!!!
 
Si bora hata wewe una kitanda, wengine tunavinjari chini ya daraja hamna cha kutandika kitanda wala nini, breakfast unachoma kaa wa Salenda, nini kuku wa Salanda...
 
Nilipokuwa sekondari form I miaka ya 70 nilikuwa sijazoea kutandika kitanda nyumbani, hivyo kila siku nilikuwa napata adhabu kwa kutokutandika kitanda, baada ya hapo mpaka kesho siwezi kuanza kufanya kitu cho chote kabla ya kutandika kitanda. Ukiongezea na zoezi la JKT ndio kabisa. Yaani hata mke wangu asipotandika atakuta mie nimeshatandika tena bila kinyongo, maana hawa wanawake wa siku hizi......Wakati mwingine nikiwa safarini kwenye lodge au hoteli najisahau na kuanza kutandika!!!Mwalimu JK alisema "Usafi ni Tabia"
 
kutandika kitanda inategemea na malez,we mama hatandiki kitanda m ndo nitatandika...mi namshukuru babangu aliekuwa akinicharaza viboko kwa kutotandika kitanda,sahz nikiamka tu,kitanda cha kwanza kujaliwa
 
Dah, nawezaje kwenda bafuni sijatandika kitanda? Siwezi lazima nitandike kitanda ndo mambo mengine yaendelee
 
Back
Top Bottom