Iundwe Tume ya kutuleta pamoja kama Taifa

Unafahamu kuwa kuna watu wanavunja katiba na sheria? Na kwamba wanafahamu lakini wanajifanya wendawazimu?
Kichaa kuna wakati anachapwa na anakuwa na adabu.
Na ndio maana nikasema iundwe tume ya kutuleta pamoja kama Taifa,hatupo pamoja wanaocheza na katiba yetu wanaona wako sawa tu ,na pia wanao kemea katiba kutokuchezewa nao wako sawa , Bila busara za kutenganisha hili basi ni hakika tunakwenda pabaya , tume itulete pamoja tuone tumekosea wapi tusameheane ,tulijenge taifa letu
 
Hakuna namna wacha INZI auliwe kwa MAX PRESSURE....ili next tym tuheshimiane
Acha tu nikujibu japo nilipanga kusoma tu. Hivi unafikiri roho za watu ni mpira wa miguu kwamba lazima mshindi apatikane? Watakaoumia sio watu ukuta tu, mali na watu wasio na hatia wataumia pia. Ni vema sisi kama raia wa nchi yetu tukaacha kushabikia hii vita inayotangazwa. Jiulize tena ndo uje kuandika huku
 
Katiba ndicho chombo pekee kilichowekwa kuunganisha nchi. Hilo la kuunda tume ni kupotezeana muda tu. Katiba ya nchi iheshimiwe na kila mtu.
 
Bora tuishi Hivi ili tuheshimiane mkuu
Na ndio tatizo ambalo naliona mkuu ,hatuko pamoja tena tuna mipasuko katikati ya jamii zetu na tukiendelea na hii dhambi ya kubaguana haitaishia hapo ,bado tuna nafasi ya kujirudi na kuendelea na utamaduni wetu wa kuvumiliana ila sio katika mambo ya kipuuzi
 
Katiba ndicho chombo pekee kilichowekwa kuunganisha nchi. Hilo la kuunda tume ni kupotezeana muda tu. Katiba ya nchi iheshimiwe na kila mtu.
Mkuu huko panapotokea machafuko hakuna katiba ?? Je hii katiba yetu ya sasa inaendana na mahitaji yetu ya sasa ? Kuunda tume kutuleta pamoja ni pamoja na kuangalia ni wapi hasa yalipo mapungufu yetu ,kama ni kwenye katiba basi lijulikane cha kufanya ama kama ni kwenye Siasa basi pia njia stahiki zifuate kutatua matatizo yetu
 
Ni wazo jema kama viongozi wetu watakaa pamoja na kuondoa tofauti zao kwa faida ya wote. Kuna faida gani kama upande mmoja ukajiona wao ni wababe na wanaweza kufanya lolote kana kwamba hii nchi ni ya kwao ? Je kuna faida gani kutumia nguvu ya jeshi la polisi kupambana na watu wasiokuwa na silaha ? Je ina maana tumeshindwa kukaa pamoja kutatua tofauti zetu mpaka tuue watu wasiokuwa na hatia ? Ebu kila mmoja atafakari hilo.
 
mimi nadhani ifikie maala kama Taifa tukawa na Maridhiano ya Kitaifa.

Tukaondoa dhana ya Umimi na Uchama, Mfano kukawa na Maridhiano ya Kitaifa Juu ya Serikali ya Mseto, itakayo Jumuisha Vyama vyote katika Muundo wa Serikali bila Kubagua.

Hii italeta si Amanitu. Bali italeta Umoja na Mshikamano wa kitaifa.

Tutengeneze Mfumo wa Kitaifa na Siyo Kichama. Unajua kwa hali ya kisiasa tuliyonayo Sasa kama Taifa Siasa inatakiwa Ituunganishe na Siyo Kutugawa.

Ili kutuleta Pamoja kama Taifa Napendekeza Mfumo Huu ukafikiriwa na Viongozi wetu ili Kutuleta Pamoja.

Najua kuna Wengi watahoji Juu ya Jambo Hili kwamba Hakuna Duniani Pote Jambo kama Hili.

Ila Nasema Sisi ni Watanzania Tunauwezo wa kuanzisha Jambo na Mataifa Mengine Wakaiga na Kujifunza Kutoka Kwetu.

Sasa hivi Dunia siyo Maala salama sana Kutokana na Chuki na Uadui Baina ya watu kwa watu. Chama kwa chama chenzake.

Hivyo basi Kama sisi Watanzania tukatengeneza Mfumo wa kutuleta Pamoja kama Taifa, na Ukajenga Mshikamano na Udugu, basi Jambo hili nila Kheri na Kujivunia na Kuigwa na Mataifa Mengine katika Kusaka Amani.
 
Mkuu huko panapotokea machafuko hakuna katiba ?? Je hii katiba yetu ya sasa inaendana na mahitaji yetu ya sasa ? Kuunda tume kutuleta pamoja ni pamoja na kuangalia ni wapi hasa yalipo mapungufu yetu ,kama ni kwenye katiba basi lijulikane cha kufanya ama kama ni kwenye Siasa basi pia njia stahiki zifuate kutatua matatizo yetu

Hiyo tume unayoitaka wewe si itaishia kuwa kama ile ya rasimu ya katiba, mwisho maslahi ya ccm yanatangulizwa kama ndio maslahi ya taifa! sasa kuna haja gani ya kuwa na tume za kutafuta miafaka ikiwa ccm haitaki mambo yabadilike? Wananchi hawana jukwaa la kusemea kero zao, sasa wachache wanaotumia majukwaa ya siasa kuelezea hisia zao halafu serikali haitaki inataka wananchi wawe mabubu wakati wanagharamia uendeshaji wa serikali waliyoiweka madarakani? Tangu lini boss akanyanyaswa na mtu aliyemuajiri?
 
Hiyo tume unayoitaka wewe si itaishia kuwa kama ile ya rasimu ya katiba, mwisho maslahi ya ccm yanatangulizwa kama ndio maslahi ya taifa, sasa kuna haja gani ya kuwa na tume za kutafuta miafaka ikiwa ccm haitaki mambo yabadilike?
Kuna vitu kwenye maisha ya mwanadamu vinahitaji real time response ,Pengine hizo tume za wakati huo walipima madhara yake ,ila hili la kutuleta pamoja kama Taifa sidhani kama wataliweka kwenye mashelfu yao ,dhambi ya ubaguzi kwenye taifa hili itatupeleka pabaya ,Bado tuna nafasi

Inawezekana kabisa kwa jana ulipuuza kula ,leo vile vile unaweza kupuuza kula na keshokutwa vilevile unaweza kufanya hivyo ,baada ya keshokutwa kitakachofuata ni nini ??

Kwa sababu jambo lilipuuzwa jana haina maana litapuuzwa milele kuna kikomo
 
Ni kweli tumevumilina na kuvumiliana kwenyewe matunda yake ndio hichi kinacho fanya tuitwe Watanzania , achilia mbali ukuta kuna maeneo mengine mengi tumeyumba
Vyombo vilivyotakiwa kutoa taswira ya mshikamano na kuheshimiana kama bunge ndivyo vilivyoanza kuonesha mitafaruku, picha iliyooneshwa na wabunge walio wengi bungeni na kiongozi wao wakati wa bunge la katiba na bunge hili la bajeti imekifedhehesha sana chombo hicho

Inapotokea mtu anataka kurekebisha wanatokea watu kama kibajaji kuhororoja, inakatisha tamaa sana na taifa linaangamia kwa ujinga wetu wenyewe
 
Vyombo vilivyotakiwa kutoa taswira ya mshikamano na kuheshimiana kama bunge ndivyo vilivyoanza kuonesha mitafaruku, picha iliyooneshwa na wabunge walio wengi bungeni na kiongozi wao wakati wa bunge la katiba imekifedhehesha sana chombo hicho

Inapotokea mtu anataka kurekebisha wanatokea watu kama kibajaji kuhororoja, inakatisha tamaa sana na taifa linaangamia kwa ujinga wetu wenyewe
Asante sana mkuu umeelewa sasa mantinki ya kupata wa kutuleta pamoja kama Taifa ,Taasisi nyingi zimeyumba kusimamia mamlaka zao ,tunahitaji kitu cha kutuleta pamoja na ndio nikaja na wazo la tume Mkuu
 
Ndugu zangu Watanzania kuna kila sababu ya kuundwa tume ya kutuleta Watanzania pamoja kama Taifa,

Taifa hili liliundwa kwa misingi ya Kuvumiliana ,Kupendana ,Kuheshimiana na Kushirikiana katika lile lilolo jema kwa mustakabali wetu.


Kadri siku zinavyokwenda vivyo hivyo vinavyo tuweka pamoja kama taifa vinazidi kutoweka.

Sisi wote ni Watanzania haijalishi huyu ni CCM,CHADEMA ,CUF ,WASIO NA VYAMA Nk Ama WAPARE,WAMASAI ,WAZIGUA ,WAHAYA,WACHAGA ,WASUKUMA NK

Atokee japo mmoja mwenye busara aseme neno TAIFA LIPONE
Kwa sasa hivi tunaishi kama tupo nchi tofauti vile wakati wote ni Watanzania

Tujifunze na tujisahihishe tulipo kosea ili tuweze kusonga mbele,

Sote ni ndugu ,watoto wa baba mmoja


MUNGU IBARIKI AFRIKA
MUNGU IBARIKI TANZANIA
Tume ya nn? Una evidence gan kuwa taifa limegawanyika? Come with solid evidence .. Lakin ujue kitaa maisha yanaendelea japo yamebana. Apa niko Na wanaukawa pmoja Na uvccm but we share each & everything....so no need of tume . Otherwise itakuwa n kuwapa shavu wanasiasa tuu
 
Siyo kila kitu unachokiona kizuri kinafaa wakati wowote, au mahala popote "maji ya chumvi hayafuliwi nguo"
 
Back
Top Bottom