Iundwe Tume ya kutuleta pamoja kama Taifa

UncleBen

JF-Expert Member
Oct 27, 2014
9,598
11,993
Ndugu zangu Watanzania kuna kila sababu ya kuundwa tume ya kutuleta Watanzania pamoja kama Taifa,

Taifa hili liliundwa kwa misingi ya Kuvumiliana ,Kupendana ,Kuheshimiana na Kushirikiana katika lile lilolo jema kwa mustakabali wetu.

Kadri siku zinavyokwenda vivyo hivyo vinavyo tuweka pamoja kama taifa vinazidi kutoweka.

Sisi wote ni Watanzania haijalishi huyu ni CCM,CHADEMA ,CUF ,WASIO NA VYAMA Nk Ama WAPARE,WAMASAI ,WAZIGUA ,WAHAYA,WACHAGA ,WASUKUMA NK

Atokee japo mmoja mwenye busara aseme neno TAIFA LIPONE
Kwa sasa hivi tunaishi kama tupo nchi tofauti vile wakati wote ni Watanzania

Tujifunze na tujisahihishe tulipo kosea ili tuweze kusonga mbele,

Sote ni ndugu ,watoto wa baba mmoja

MUNGU IBARIKI AFRIKA
MUNGU IBARIKI TANZANIA
 
Kuvumiliana tushavumiliana vya kutosha,hii ni nchi yetu sote madaraka ni dhamana tu,.

UKUTA
uko palepale!
Ni kweli tumevumilina na kuvumiliana kwenyewe matunda yake ndio hichi kinacho fanya tuitwe Watanzania , achilia mbali ukuta kuna maeneo mengine mengi tumeyumba
 
Tatizo siyo kuwa hakuna mwenye busara bali mtukufu rais wetu ni mkali mkali tu so kila mtu anaogopa akimshauri atatumbuliwa mara moja. Mtu kama Masaju sijui anamshaurigi nini rais yeye akiwa kama Attorney General

Lkn muda bado upo acha waendelee kupasha ila napo ikishindikana basi tutajua nini kitatokea mbele kwa mbele.
 
Matamko ya utani yamezidi, labda iundwe tume ya kumshauri mtoa matamko aanze sasa kufuata katiba na sheria za nchi,
Tunamshukuru makonda na ummy kwa kutengua baadhi ya matamko
 
Mkuu busara ni pamoja na ujasiri ,unataka kuniambia taifa hili lote halina watu wa kumwambia ukweli kisa wanamuogopa ??
 
Hakuna namna wacha INZI auliwe kwa MAX PRESSURE....ili next tym tuheshimiane
Mkuu hakuna heshima ,kwenye mauaji ,ukimbizi ,ubakaji,haya kama matokeo ya vita, bado tuna nafasi ya kujirudi
 
ACHA TU TUJENGEANE UKUTA TU

OVA
Ukuta sina tatizo nalo mkuu ,ila matokeo yake ndio yanipa wakati mgumu nikilifikiria hili swala ,badala ya kutuleta pamoja mpasuko unaongezeka
 
Hatuhitaji tume wala neno la mtu, KATIBA KAZI YAKE NINI??? ifuatwe tu kila kitu kitakua kwenye mstari
Ni kweli kabisa ,Katiba na sheria nyingine zipo ,ila pia ni ukweli usiopingika uchaguzi wa mwaka jana uliacha nyufa kubwa ,inahitajika busara kutuweka pamoja badala ya maguvu na ubabe
 
Ukuta sina tatizo nalo mkuu ,ila matokeo yake ndio yanipa wakati mgumu nikilifikiria hili swala ,badala ya kutuleta pamoja mpasuko unaongezeka
Mbona huku uraiani tushaanza kuishi kwa kujengeana ukuta mkuu....wa huku wa huku wa kule wa kule....

Ova
 
Matamko ya utani yamezidi, labda iundwe tume ya kumshauri mtoa matamko aanze sasa kufuata katiba na sheria za nchi,
Tunamshukuru makonda na ummy kwa kutengua baadhi ya matamko
Ni sawa Mkuu ,ila unaamini kabisa kauli zake ni utani ? Ukiachilia hili la kufyatua watoto ,unakumbuka mgomo fulani wa madereva wa Malori ?
 
Tume? Kwani katiba imefutwa?
Mkuu kwani mpasuko umeletwa na kutofuata katiba pekee ,? Imefikia sehemu kama taifa baadhi ya watu wanaona wanakandamizwa na kunyimwa haki yao ,haki huwa haiombwi inapiganiwa watakapo amua kufanya hivyo unafikiria kama taifa tutakuwa na umoja wetu ?
 
Mbona huku uraiani tushaanza kuishi kwa kujengeana ukuta mkuu....wa huku wa huku wa kule wa kule....

Ova
Na ndio tatizo ambalo naliona mkuu ,hatuko pamoja tena tuna mipasuko katikati ya jamii zetu na tukiendelea na hii dhambi ya kubaguana haitaishia hapo ,bado tuna nafasi ya kujirudi na kuendelea na utamaduni wetu wa kuvumiliana ila sio katika mambo ya kipuuzi
 
Mkuu kwani mpasuko umeletwa na kutofuata katiba pekee ,? Imefikia sehemu kama taifa baadhi ya watu wanaona wanakandamizwa na kunyimwa haki yao ,haki huwa haiombwi inapiganiwa watakapo amua kufanya hivyo unafikiria kama taifa tutakuwa na umoja wetu ?
Unafahamu kuwa kuna watu wanavunja katiba na sheria? Na kwamba wanafahamu lakini wanajifanya wendawazimu?
Kichaa kuna wakati anachapwa na anakuwa na adabu.
 
Back
Top Bottom