Bams
JF-Expert Member
- Oct 19, 2010
- 16,717
- 41,495
Wote wenye akili timamu na uelewa wa kutosha, walifahamu kwa uwazi kabisa kuwa taarifa ile kuwa Acacia walikuwa wanadaiwa kodi ya sh. Trilioni 360, walijua kuwa ni uwongo na hadaa ya hali ya jui.
Thamani ya mauzo ya dhahabu yote toka migodi yote ya dhahabu nchini Tanzania tangu migodi hiyo ianze uzalishaji, ilikuwa haifikii shilingi trilioni 360.
Ingewezekana vipi kampuni moja idaiwe kodi ya sh. Trilioni 360? Ile ilikuwa ni dhaharau kubwa kwa umma. Hawa watu waliwaona Watanzania hawana akili, ni watu wa kumeza uwongo wa kila aina toka kwa watawala.
Kama msemo wa wenye hekima unavyonena, njia ya mwongo ni fupi. Sasa Kabudi na Mwigulu wamelazimika kukiri hadharani kuwa waliudanganya umma.
Katiba yetu inatamka wazi kuwa umma ndiyo mamlka ya juu kuliko mamlaka zote. Hawa walioudanganya umma, na wapo hai, waachwe tu kwa uovu huo walioufanya? Hili moja wamekiri wazi kuwa walidanganya, je waliudanganya umma kwa mambo mangapi?
Leo hii tuna vijana wengi, hasa ndani ya UVCCM wamejazwa ujinga na kutetea mambo mengi ya uwongo na ujinga kutokana na uwongo waliolishwa na hawa watawala. Madhara haya waliyoyapata hawa vijana wa UVCCM kiasi kwamba wengi wao wanapojadili hoja za uchumi, uwekezaji, demokrasia au utawala bora, wanaonekana kama ni watu wenye uelewa duni kabisa, watafidiwa vipi kwa haya madhara waliyoyapata? Na nani atalipia?
Angalao ili kuweza kuwaondoa ujinga kutoka katika mioyo na akili, hasa za vijana wa UVCCM ambao kiufahamu wameharibiwa kutokana na kudanganywa na watawala, kuundwe tume itakayochunguza na kitoa taarifa ya wazi juu ya mambo yote ambayo watawala waliwadanganya wananchi, ili watu wautambue ukweli kuliko kuendelea kuishi kwenye ujinga na hadaa walizolishwa kwa muda mrefu.
Pia oundwe sheria kali, ambayo itamfanya kila kiongozi mwongo kutumikia jela. Na viongozi wanaowaharibu vijana kifikra na kimaadili, wasiwe na mbadala wa adhabu, zaidi ya kifungo.
Mmoja amesikika huko Mbeya akiwahamasisha vijana wa UVCCM kufanya uovu. Viongozi kama hawa wanaowaharibu vijana mahali pao salama palitakiwa kuwa jela.