Iundwe kamati maalumu ya bunge - yanayoendelea misikitini na makanisani | JamiiForums | The Home of Great Thinkers

Dismiss Notice
You are browsing this site as a guest. It takes 2 minutes to CREATE AN ACCOUNT and less than 1 minute to LOGIN

Iundwe kamati maalumu ya bunge - yanayoendelea misikitini na makanisani

Discussion in 'Jukwaa la Siasa' started by Nemesis, Oct 17, 2012.

 1. Nemesis

  Nemesis JF-Expert Member

  #1
  Oct 17, 2012
  Joined: Feb 13, 2008
  Messages: 3,833
  Likes Received: 1,089
  Trophy Points: 280
  Hakuna anayejua kwa undani yanayoendelea katika misikiti na makanisa yanayotishia amani na utulivu wa nchi. Ni dhahiri vyombo vya dola vimeshindwa na haviwezi tena kurudisha hali kutokana na kampeni zinazoendelea.

  Nimefuatilia matamko mbalimbali ya Waislam (BAKWATA), UAMSHO na wanaharakati wa dini hiyo toka uchaguzi wa 2010. Pia Tumeyaona yaliyofanyika Zanzibar, Mtwara, Mbagala (Temeke) na Kigoma pia. Pia mihadhara inaendelea maeneo mengi ya nchi hasa katika juma hili. Ukisikia yanayoongelewa yanatisha.

  Kwa upande mwingine, kuna msululu wa jumbe za simu (sms) zinazunguka miongoni mwa Wakristo kila siku zikihamasisha maombi na zingine zinapindukia hata kutaka vita (mapambano ya mwili) dhidi ya Waislam. Kwa ujumla hali ni mbaya na inazidi kuwa mbaya kila siku.

  Haya ndiyo yanayosikika, bila shaka yapo mengi na pengine kunamipango ya hatari sana inayoendelea katika misikitio na makanisa au waumini wa dini hizo mbili ambayo yanahitaji kuwa wazi na kuwekewa mikakati ya kuinusuru nchi.

  Miaka ya 2000 nchi ya Rwada ilijenga shaka juu ya yanayoendelea mashule. Bunge la nchi hiyo liliunda kamati ya bunge na kufanya uchunguzi. Yaliyobainika yalikuwa makubwa na kulikuwa na uwezekano wa kurudi kwenye vita vya kikabila baada ya muda fulani (wanafunzi watakapokuwa wakubwa). Kamati hiyo ilitoa mapendekezo ambayo yalilazimisha kufanyika kwa mageuzi makubwa katika sekta ya elimu na kutokomeza kabisa elimu ya chuki na ubaguzi wa kihutu na kitusi.

  Ni rai yangu, kuundwa kamati ya bunge, yamkini tutaondoa chuki, udini na hasira za kidini zinazopandikizwa kwa kasi ya ajabu.
   
 2. Ringo Edmund

  Ringo Edmund JF-Expert Member

  #2
  Oct 17, 2012
  Joined: May 10, 2010
  Messages: 4,895
  Likes Received: 28
  Trophy Points: 0
  thanks.
   
 3. Lyimo

  Lyimo JF-Expert Member

  #3
  Oct 17, 2012
  Joined: Mar 7, 2006
  Messages: 3,828
  Likes Received: 33
  Trophy Points: 145
  Sidhani kama hili watalisikiliza, kwani kwasasa nchi yetu inaongozwa na matukio. Watasubiri mpaka yatakapotokea madhara ndiyo wataunda kamati ambayo majibu yake yatakuwa ya kuwafurahisha wao na si ya kutoa ufafanuzi na utatuzi wa kiini cha tatizo. Tunashangaa jinsi Chama na serikali kilivyobadili majukumu ya usalama wa Taifa. Hii kazi unayopendekeza ingekuwa ilishashughulikiwa zamani sana na usalama wa Taifa na pengine kulidhibiti kabisa. Ila sasa usalama wa Taifa wetu wanafanya kazi za ajabu za kufukuzana na kina Slaa, CDM, Ulimboka nk.
   
 4. DALLAI LAMA

  DALLAI LAMA JF-Expert Member

  #4
  Oct 17, 2012
  Joined: Jan 31, 2012
  Messages: 8,617
  Likes Received: 401
  Trophy Points: 180
  Kamati na fungu lote la nini? Matunda ya magamba hayo kuendekeza udini kutawala..DHAIFU kacheza rafu sana kudeclare kuwa kuna udini.VIBARAKASHIA WANAONA WANAONEA KUMBE LAA.
   
 5. m

  majiyachai Member

  #5
  Oct 17, 2012
  Joined: Apr 3, 2012
  Messages: 20
  Likes Received: 0
  Trophy Points: 0
  Wa Tanzania tunapenda mambo ya tume saana hata pale ushahidi unapokuwa wazi.
  Kuundwa kwa tume ya watu kama kumi maanake hela zetu ziliwe na hiyo tume. Wakichukua muda wa miezi mitatu kuzunguka mikoani eti kufanya utafiti katika maeneo yote yaliokumbwa na matatizo haya, halafu miezi mingine miwili kutayarisha taarifa yao ni takriban miezi mitano. Utakapokuja kushusha mahesabu ili upate jumla ya pesa zilizotumika na hii tume, usishangae kukuta Bilioni moja imekwisha!
  Tume ya nini na inafahamika wazi kwamba hawa akina Sheikh Ponda ni waislamu wachache sana waliotumwa kuwafanyia vurugu ndugu zetu wakristu. Matendo yao ni ya aibu kwetu sisi waislamu tunaoijua dini.

  KAMANDA MMOJA TU mzalendo, akiwa na kikosi cha askari mia mbili, anaweza kulimaliza hili tatizo ndani ya mwezi mmoja likawa historia!

  Ni uamuzi tu!
   
 6. Safari_ni_Safari

  Safari_ni_Safari JF-Expert Member

  #6
  Oct 17, 2012
  Joined: Oct 5, 2007
  Messages: 22,461
  Likes Received: 5,845
  Trophy Points: 280
  Nchi haina dini.........hiyo kamati itakuwa na wajumbe wa imani gani?
   
 7. CHUAKACHARA

  CHUAKACHARA JF-Expert Member

  #7
  Oct 17, 2012
  Joined: Jun 3, 2011
  Messages: 12,206
  Likes Received: 3,827
  Trophy Points: 280
  Tatizo la waislam ni kuamini katika fujo. Kuweka matatizo yao kuwa yanaletwa na wenzao. Hata hizo kamati zinaweza zisiwe na maana kwa mtazamo wa hawa ndugu zetu. Nani ana chuki na mwenzake? Sijui, lakini jaribu anyway!
   
 8. t

  thatha JF-Expert Member

  #8
  Oct 17, 2012
  Joined: Apr 29, 2011
  Messages: 15,234
  Likes Received: 179
  Trophy Points: 160
  Bunge limepoteza sifa bwana, upuuzi mtupu huo. Wameshindwa kujichunguza weneywe kwenye kashfa ya TANESCO huko watafanya nini?

  Nani kasema Serikali imeshindwa kudhibiti hali hiyo? Serikali ina mkono mrefu wewe usione wamenyamaza kimya ukafikiri hawawezi.
   
 9. The Son of Man

  The Son of Man JF-Expert Member

  #9
  Oct 17, 2012
  Joined: Feb 9, 2010
  Messages: 12,126
  Likes Received: 1,705
  Trophy Points: 280
  To be honest, hatuhitaji kamati yoyote, itakuwa ni kuendelea kutumia resources za mwananchi wa kawaida unnecessarily. Huwa sioni tija katika kamati hizi.
   
 10. Nemesis

  Nemesis JF-Expert Member

  #10
  Oct 17, 2012
  Joined: Feb 13, 2008
  Messages: 3,833
  Likes Received: 1,089
  Trophy Points: 280
  Nimeonja japo kiasi juu ya ninayoyaita "yanayoendelea misikitini na makanisani" ambayo yanahitaji uchunguzi wa kina. Kuna meseji nyingi zinazunguka kwa waumini wa dini hizi mbili.
   
 11. Nemesis

  Nemesis JF-Expert Member

  #11
  Oct 17, 2012
  Joined: Feb 13, 2008
  Messages: 3,833
  Likes Received: 1,089
  Trophy Points: 280
  Hata hivyo, binafsi naona suala hili limevuka upeo wa kisiasa ndiyo maana napendekeza kuchukuliwa hatua za busara zaidi.
   
 12. Nemesis

  Nemesis JF-Expert Member

  #12
  Oct 17, 2012
  Joined: Feb 13, 2008
  Messages: 3,833
  Likes Received: 1,089
  Trophy Points: 280
  Gharama tutakayoikwepa ni ndogo mno ukilinganisha na hatari zinazoweza kutokea. Pia nadhani hali ilipofikia hata huyo kamanda mmoja hataweza kufanya lolote.

  Ukitaka kujua zaidi ktk mtihani wa form four unaoendelea yamefanyika na kusemwa mengi kuhakikisha watoto wa dini fulani aidha wanafeli au wanashindwa kufanya mitihani.

  sms zinazozunguka miongoni mwa wakristo kwasasa zinahamasisha mapambano ya kimwili na waislam.
   
 13. Nemesis

  Nemesis JF-Expert Member

  #13
  Oct 17, 2012
  Joined: Feb 13, 2008
  Messages: 3,833
  Likes Received: 1,089
  Trophy Points: 280
  Hujaijua vizuri Serikali iliyopo.
   
 14. TZ biashara

  TZ biashara JF-Expert Member

  #14
  Oct 17, 2012
  Joined: Mar 9, 2012
  Messages: 523
  Likes Received: 5
  Trophy Points: 0
  Hakuna haki katika nchi na ingekuwa haki inatendeka basi kila mtu asingemnyooshea kidole mwenzake.Hizi chokochoko zinaletwa na wachache halafu waandishi na wao wanachochea kivyao na huku kwenye mitandao kwa sisi watoa mada na maoni tunachangia kwa upande wetu.

  Kama kweli tunapenda amani na utulivu ili tuendelee na maisha yetu kuitafuta riziki,basi tungetulizana badala ya kutoa kashfa na maneno mengine ya uongo na kweli.Uvumilivu ni kitu bora zaidi ya machafuko.Tujiheshimu na kuheshimu wengine na tujadiliane bila ya jazba ili tujuane kila upande wa mwenzake unadai nini au kwanini matukio mabaya yanatokea na kwanini yanapotokea baina ya watu wa chache yakazua balaa na kuchafua nchi nzima?

  Serikali inapaswa kujadiliana na waisilamu pamoja na wakristo na kujua pande hizi mbili ni nini hasa kinachoendelea.Ama kama kuna madai yoyote yanahitajika kwa pande hizi zote basi kwa kutumia katiba ya nchi wasikilizwe ili kuondoa huo mgogoro.Nauhakika kinachohitajika ni maelewano tu hakuna kingine.Na iwepo sheria kali za kuwadhibiti wale wenye kuleta mijadala ya kidini na kusababisha machafuko.

  Wazazi kwa upande wetu nadhani tunahitaji kuwapa masomo mazuri watoto wetu ili waweke heshima zao na heshima kwa wengine.Hawa watoto tukiwafundisha chuki basi tunalitengeneza taifa la kesho likiwa katika chuki na kama tutawafundisha watoto wetu upendo na kuwajali wengine basi tutalitengeneza taifa likiwa na amani kutoka kwa watoto wetu ili na wao waendeleze amani pamoja na taifa lao linalokuja wakati huo sisi tutakuwa wote tumekufa ila wao ndio jukumu tumewaachia.

  Jamii Forum na wao wachukue tahadhari ya kuruhusu kila mtu kutoa mada anayohisi inamfurahisha lakini inajenga chuki.Freedom of speech wakati mwingine inaweza kuhatarisha amani katika nchi yetu.
   
 15. nngu007

  nngu007 JF-Expert Member

  #15
  Oct 17, 2012
  Joined: Aug 2, 2010
  Messages: 15,871
  Likes Received: 56
  Trophy Points: 145
  Kamati Sio Lazima; Ni Kiongozi wa NCHI ndiye anayetakiwa kuwa na HEKIMA za kusuluhisha JAMBO HILO MIAKO 50 ya UHURU hatukuwa na UCHOMAJI wa NYUMBA za DINI;
  RAIS, ANATAKIWA awe IMARA KIDOGO...
   
 16. BinMgen

  BinMgen JF-Expert Member

  #16
  Oct 17, 2012
  Joined: Jun 18, 2008
  Messages: 1,816
  Likes Received: 28
  Trophy Points: 145
  Acha kumlaumu jk alie asisi udini nchi ni Nyerere

  Sent from my GT-I9300 using Tapatalk 2
   
 17. Heavy equipment

  Heavy equipment JF-Expert Member

  #17
  Oct 17, 2012
  Joined: Oct 13, 2012
  Messages: 930
  Likes Received: 251
  Trophy Points: 80
  Wakristo wana imani MUNGU anaye angamiza mwili na roho katika jehanamu waislamu wana imani ya uchomaji wa makanisa kamati itashindwa la kufanya, JK alishapanda mbegu imeota sasa analaghai wakristo
   
 18. WABHEJASANA

  WABHEJASANA JF-Expert Member

  #18
  Oct 17, 2012
  Joined: Jun 22, 2011
  Messages: 4,225
  Likes Received: 7
  Trophy Points: 135
  Kamati ya kazi gani mura?,wacha tu muda ukifika kila mmoja atakamata pange tughechane tu basi yaishe kwanza maisha magumu halafu bado kamati ambayo inakula pesa nyingi,ahaaaaa!

  Swali zuri sana mjeshi limelenga penyewe.

  Mi niataka nishauri yanini kuandikia mate wakati wino upo unakuja,tusubiri muda ukifika basi kitaeleweka kama imepangwa hata ukiunga kamati yenye mjumbe kutoka kila dhehebu na kutoka katika kila ubalozi,bado yatatimia tu wacha kuzuia jambo hili.

  Ushaui mzuri kaka kila mmoja aplay party yake.

  Ni kweli amiri jeshi wangu lakini kumbuka kama imepangwa itakua tu,hata liJK likitumia busara ya namna gani kitaeleweka tu,hapa cha msingi kila mmoja aanze kuandaa makao yake mahali apajuapo,na kama pesa hakuna msuri mfukoni ni hatari tupu.
   
 19. M

  MVENGEVENGE Senior Member

  #19
  Oct 17, 2012
  Joined: Sep 15, 2011
  Messages: 158
  Likes Received: 1
  Trophy Points: 0
  naona tusikwepe hoja tatizo liko misikitini na sio makanisani huku ndio kunatakiwa kitu kifanyike.
   
 20. Bitabo

  Bitabo JF-Expert Member

  #20
  Oct 17, 2012
  Joined: Sep 27, 2011
  Messages: 1,896
  Likes Received: 124
  Trophy Points: 160
  Kama kamati itaongozwa na wakinga "Ngwilizi" itakuwa haina maana. Mwache JK aendelee kuzubaa tu atakuta nchi inaongozwa na Kardinali Pengo
   
Loading...