ITV wekeni tafsiri ya maandishi 'subtitles'

Kiwi

JF-Expert Member
Sep 30, 2009
1,054
990
Wanajamvi kama mtazamaji wa ITV mara kwa mara nimekuwa nakerwa na tabia ya kuonyesha mtu ama watu wakizungumza kwa lugha ya kigeni hususan kiingereza bila ya kuwa na tafsiri ya kimaandishi (subtitles) ama hata kuweka tafsiri ya juu ya maongezi kwa kiswahili. Leo nilimwona mtu mmoja hakuwa mtanzania (sikulishika jina lake) akizungumza kuhusu kumbukumbu ya mauaji ya kimbari huko Rwanda akieleza vizuri sana hoja yake kwa kiingereza. Alifuatiwa na Danford Mpumilwa aliyezungumza kwa kiswahili. Sasa ile hoja nzuri ya yule aliyetangulia nina hakika kuna wengine wameambulia kutazama picha tu!

Inashangaza sana kwa kituo kama ITV ambacho kinajisifu sana kwa kupata tuzo ya kituo bora cha kutangaza kwa njia ya televisheni kimeshindwa kabisa kutafuta watu wa kufanya tafsiri. Ieleweke ya kuwa bado lugha yetu ya taifa ni kiswahili, na wananchi walio wengi hawafahamu vizuri kiingereza.

Jirekebisheni...
 
Tatizo kubwa Tanzania kuanzia ngazi ya taifa ni kuwa huduma zinazotolewa hazimlengi kikamilifu mwananchi. Huduma inatolewa bila kujali kwamba wananchi wote watafaidika kwa huduma hiyo au la. Kitu kikubwa ambacho kinachoangaliwa ni faida gani tu ambayo wataipata.
 

Similar Discussions

Back
Top Bottom