Waziri Kamwelwe: Watalii waanza kuingia Tanzania

Nrangoo

JF-Expert Member
May 22, 2017
3,352
5,250
Katika sekta ya utalii nchini ambayo Rais Magufuli amesema itarejesha huduma zote wiki ijayo, Waziri wa Ujenzi, Uchukuzi na Mawasiliano Mhandisi Isack Kamwelwe amebainisha kuwa tayari baadhi ya watalii wameshaanza kuingia nchini.

20200521_205744.jpg
 
Hata corona mna sema imekwisha wakati watu wana kufa. Na mna sisitiza tuvae barakoa. Kama ime isha barakoa za nini?

Sent using Jamii Forums mobile app

Mkuu hawajasema hilo tu, wanasema tujikinge na kufauata ushauri wa madaktari. Hata dawa yetu ya kujifukiza haikutajwa na mkuu tena.

Zaidi ya hapo bado wanasisitiza misaada ya corona ipitie wizara na uchunguzi ufanyike. Ingekuwa imekwisha wasingehitaji haya.

Lakini baya zaidi ni pale waliposema tutaanza kutengeneza barakoa zetu wenyewe. Yeyote mwenye ufahamu wa kutosha anatambua kupitia hili kuwa corona iko.

Ninachokubaliana nao ni kuwa kwenye tropical areas corona haina nguvu sana za kuua. Mazingira yetu ni mabaya kwa kirusi. Hii ndio bahati tuliyonayo na tuna bahati kuwa sehemu hii ya dunia!!
 
Katika sekta ya utalii nchini ambayo Rais Magufuli amesema itarejesha huduma zote wiki ijayo, Waziri wa Ujenzi, Uchukuzi na Mawasiliano Mhandisi Isack Kamwelwe amebainisha kuwa tayari baadhi ya watalii wameshaanza kuingia nchini.
#TourismTanzania Azam TV on TwitterView attachment 1456022
Huyu mzee angalie naona naye anaongea bila kuvaa barakoa. Corona kwa umri wake huo kama kumenya nanasi kwa panga la kuchinjia ng'ombe.
 
Mkuu hawajasema hilo tu, wanasema tujikinge na kufauata ushauri wa madaktari. Hata dawa yetu ya kujifukiza haikutajwa na mkuu tena.

Zaidi ya hapo bado wanasisitiza misaada ya corona ipitie wizara na uchunguzi ufanyike. Ingekuwa imekwisha wasingehitaji haya.

Lakini baya zaidi ni pale waliposema tutaanza kutengeneza barakoa zetu wenyewe. Yeyote mwenye ufahamu wa kutosha anatambua kupitia hili kuwa corona iko.

Ninachokubaliana nao ni kuwa kwenye tropical areas corona haina nguvu sana za kuua. Mazingira yetu ni mabaya kwa kirusi. Hii ndio bahati tuliyonayo na tuna bahati kuwa sehemu hii ya dunia!!
Kama corona imepungua kwa kasi haraka hivi basi kuna mbinu za ziada zimetumika, Brazil ni ukanda wa tropic na hali ya hewa haina tofauti kubwa na baadhi ya mikoa yetu lakini sasa wanakiona cha moto.
 
Katika sekta ya utalii nchini ambayo Rais Magufuli amesema itarejesha huduma zote wiki ijayo, Waziri wa Ujenzi, Uchukuzi na Mawasiliano Mhandisi Isack Kamwelwe amebainisha kuwa tayari baadhi ya watalii wameshaanza kuingia nchini.
#TourismTanzania Azam TV on TwitterView attachment 1456022
Duuuu
Hili ni pigo kubwa sana kwa kundi lile la ufipa. Tegemeo lao ni watu kufa kwa wingi wapate la kusema na uchumi kupolomoka wapate kutangaza sera ya chama chao. Kwani chimbuko la sera za chama chao ni matukio.

Na yule msaliti na kibalaka wa mabeberu (ZZK) nae huko aliko atakuwa yu taabani. Ĺeo nimemsikia analaani vyuo kufunguliwa.

Sent using Jamii Forums mobile app
 
Mhmmm kazi kweli kweli elimu ni muhimu Sana kwa watoto wetu kwani wasomi tulio nao wamesomeshwa na.............. Kwaiyo lazima waongee kama wanavyotakiwa.
 
Hivi wanafikiri utalii ndyo utafufua uchumi wetu kwa sasa? Kwanini nguvu nyingi wanaweka kwenye utalii. Kwanza Rais anadai tupo VITANI alafu watalii/ mabeberu nao wajichanganye vitani!

Ni kujidanganya kuwa uchumi utafufuliwa na utalii.

Huu ndyo muda serikali ilitakiwa kuja na stimulus packages kufufua secta binafsi na viwanda.

Sasa hawaongelei viwanda wao ni utalii tu.

Sent using Jamii Forums mobile app
 
Back
Top Bottom