ITV na "Morbid Curiosity", Very Unprofessional! | JamiiForums | The Home of Great Thinkers

Dismiss Notice
You are browsing this site as a guest. It takes 2 minutes to CREATE AN ACCOUNT and less than 1 minute to LOGIN

ITV na "Morbid Curiosity", Very Unprofessional!

Discussion in 'Habari na Hoja mchanganyiko' started by Pascal Mayalla, May 24, 2012.

 1. Pascal Mayalla

  Pascal Mayalla JF-Expert Member

  #1
  May 24, 2012
  Joined: Sep 22, 2008
  Messages: 24,566
  Likes Received: 18,533
  Trophy Points: 280
  Wanabodi,
  Sio mara moja wa mbili nimekuwa nikiilalamikia ITV kwa vitendo vichache ambavyo ni kinyume cha maadili ya uandishi na utangazaji wa habari na kinyume cha haki za binaadamu, kunyeme cha utu na ubinaadamu, ni udhalilishaji mkubwa wa maiti za binaadamu!.

  Leo kwenye taarifa yake ya habari ya saa 5:00, ITV wameonyesha picha za mwanafunzi wa Chuo Kikuu cha Tumaini iliyejinyonga chumbani kwake kwenye hostel inayotumiwa na wanafunzi wa chuo hicho!.

  1. Kabla ya kuonyesha picha za aina ile, mtangazaji wa ITV alipaswa kutoa anyo kuhusu picha mbaya, hakutoa onyo kabla na badala yake aliomba radhi baada ya picha hizo!.
  2. Kuonyesha close -up shot ya mwili wa marehemu inayoonyesha sura ya marehemu, ni kinyume cha maadili ya uandishi wa habari na ni dhihaka kwa marehemu!.
  3. Hakukuwa na sababu za msingi za kuonyesha mwili wa marehemu ukining'inia na kupiga angles mbalimbali na kuzirudia rudia, hivyo inaitwa "morbid curiosity" na ni very unprofessional kwenye tasnia ya picha za habari!.
  4. Kwa kawaida, kwenye ajali zozote zinazohusisha vifo, majina ya marehemu huwa yanapaswa kuwa withheld kwanza mpaka ndugu wanapokuwa notified, kitendo cha Kuonyesha sura ya marehemu at very range na jinsi alivyokufa, sio tuu ni shocking bali ni in humane kwa ndugu kwani zile picha badala ya kutoa taarifa za msiba, zinazidi kuwa traumatize wafiwa!.
  5. Kwa wapenzi wa horor kwao its ok, lakini kwa watu wa kawaida picha hizo ni ofensive na ni very unprofessional!.

  ITV, hata kama lengo la kuajiri unprofesional is to save on salaries, wapiga picha wenu hao amatures, nendeni mkawabrush japo kidogo tuu na media ethics!.

  ITV generally mnafanya kazi nzuri sana, lakini haya mapungufu madogo madogo machache yanawashushia weledi wenu!.

  Badilikeni!.

  Paskali
   
 2. platozoom

  platozoom JF-Expert Member

  #2
  May 24, 2012
  Joined: Jan 24, 2012
  Messages: 7,322
  Likes Received: 2,307
  Trophy Points: 280
  Mimi nimependa unavyochomeka maneno ya kizungu kwenye kila sentesi.............Sina hakika kama huna kamusi
   
 3. F

  FJM JF-Expert Member

  #3
  May 24, 2012
  Joined: Apr 11, 2011
  Messages: 8,088
  Likes Received: 90
  Trophy Points: 145
  Pasco, ITV kuna matatizo sana ya 'ethics' za journalism. Inawezekena kweli wanaajiri watu ambao sio professionals ili kukwepa gharama, lakini pia naamii hawana meaninguful in-house training kwa hao wanowaajiri.

  Kuna watangazaji kila nikisikia sauti zao nazima simu. George Marato, na Sam Mahela. Wamegeuza taalum hiyo na kuifanya ime drama! Newsreporter anakuwa a major distraction kwa msikilizaje ni kinyume kabisa na ethics. Alianza Gerge Marato lakini Sam Mahela naona naye anashika kasi. Huku ni kuidhalilisha taaluma yenyewe.
   
  Last edited by a moderator: Jan 4, 2016
 4. zomba

  zomba JF-Expert Member

  #4
  May 25, 2012
  Joined: Nov 27, 2007
  Messages: 17,081
  Likes Received: 49
  Trophy Points: 0
  Siku zingine unaongea vyema. Lakini wakikurushia kibahasha tu, Kimyaaa! wamekunyima mkataba nini?
   
 5. The Son of Man

  The Son of Man JF-Expert Member

  #5
  May 25, 2012
  Joined: Feb 9, 2010
  Messages: 12,124
  Likes Received: 1,707
  Trophy Points: 280
  Nimeiona nkajiuliza kama kweli kitu kama hiyo inakubalika sikupata jibu!!!
   
 6. B

  BigMan JF-Expert Member

  #6
  May 25, 2012
  Joined: Feb 19, 2007
  Messages: 1,097
  Likes Received: 2
  Trophy Points: 135
  pasco usiwe kama hujawahi kuwa reporter katika vituo mbalimbali unataka kuniambia pale newsroom ya itv hakuna wahariri wenye taaluma ya kutosha ya habari ? kwani ninavyofahamu mimi hata kama wapiga picha ni wa kuokoteza mitaani lakini mwenye uamuzi wa kupitisha habari husika ni mhariri aliyeko newsroom si kila habari inayofika newsroom lazima ipite pili kuna watu wa editing ambao naamini kuwa wana qualifications zote
   
 7. Kiranga

  Kiranga JF-Expert Member

  #7
  May 25, 2012
  Joined: Jan 29, 2009
  Messages: 34,607
  Likes Received: 6,185
  Trophy Points: 280
  Mkuu wangu Pasco,

  Mie muda huo sikuwa na uwezo wa kuona hiyo habari - niko mbali na nyumbani bado-, lakini nilikuwa naongea na mtu nyumbani wakati huo huo, akaniambia kuhusu hii habari. Swali langu la kwanza likawa jinsi ilivyoonyeshwa kwa maana najua kabisa swala unalolizungumzia kwamba hakuna sensitivity mara nyingine.

  Sasa ukimjua mtu, au organization, mpaka ukaweza ku predict kutoka thousand of miles away jinsi watakavyoonyesha hiyo habari, hili linaonyesha kwamba hili si jambo la mara moja tu.

  Nashukuru na wewe umeliona hili.
   
 8. Pascal Mayalla

  Pascal Mayalla JF-Expert Member

  #8
  May 25, 2012
  Joined: Sep 22, 2008
  Messages: 24,566
  Likes Received: 18,533
  Trophy Points: 280
  Mkuu Big Man, news editor anakaa newsroom kazi yake ni ku edit news contents haswa kwa upande wa text, (script) baada ya hapo script na footage zinatua editing bench kutengeneza insert, kazi ya editor ni kutumia shots atakazoelekezwa ama na sub editor au reporter aliyekwenda. Mwenye uamuzi picha gani itumike sio photo editor ni sub editor. Kwa jinsi story ya jana ilivyo, mpiga picha alipiga picha chache na concentration ilikuwa ni kwenye mwili wa marehemu tuu ndio maana zilirudiwa 4 times!.
   
 9. mizambwa

  mizambwa JF-Expert Member

  #9
  May 25, 2012
  Joined: Oct 8, 2008
  Messages: 4,409
  Likes Received: 569
  Trophy Points: 280
  .........Stil Loading Network........60%.........
   
 10. Pascal Mayalla

  Pascal Mayalla JF-Expert Member

  #10
  May 25, 2012
  Joined: Sep 22, 2008
  Messages: 24,566
  Likes Received: 18,533
  Trophy Points: 280
  Mkuu Kiranga, unprofessionalism is order of the day pale ITV newsroom, kuna wakati mmiliki akifanya jambo, basi ndio lilikuwa headline yao na insert ya 5, 6 or 7 min!. Editor ni rafiki yangu nikamuuliza hivi inakuwaje news item iwe more than 5 min?!. Kwenye broadcast any news item must be less than 5 min, ikifika 5 min hiyo sasa ni program!. The only exception ni kwenye live repirtage au developing news!. Baada ya Adam Malima kumlipua Mzee bungeni hilo sasa wamejirekebisha.

  Hili la kuweka picha mbaya za vifo vya ajali kwa kuonyesha close up hawakuanza leo, tangu ile ajali ya lori la mafuta kule Mbeya, ITV ilionyesha miili iliyoungua very close na mtangazaji kusema "miili imeungua vibaya na kuonekana mithili ya mbuzi wa ndafu aliyebanikwa!". Juzi juzi wakati wa ajali ya MV Spice walionyesha sura za watoto waliokufa at very close range etc.

  Wakati wa genocide ya Rwanda, CNN walionyesha floating dead bodies zikielea ziwa Victoria at a distance, watu walipiga kelele!. During 9/11 tulionyeshwa tuu black bags zenye miili!. Wenzetu wana heshima ya miili hata namna ya kuubeba, hapa kwetu jana wameonyesha mpaka process ya body removal, hakuna heshima hata kidogo na kamera ndio inang'ang'ania hapo hapo!.

  Yaani, ...we acha tuu!.
   
 11. Lokissa

  Lokissa JF-Expert Member

  #11
  May 25, 2012
  Joined: Nov 20, 2010
  Messages: 7,079
  Likes Received: 155
  Trophy Points: 160
  nakubaliana na ww Pasco
  marehemu ana right to be forgotten
  ITV wangeonyesha chumba au picha yake basi lkn sio yeye akiwa marehemu.
  nadhani wanaoandaa taarifa na kuedit picha shule yao bado ina walakini kuhusu hili
  waige BBC na vyombo vya nje mfano kule marekani sept 11 nani aliona picha za marehemu? hakuna.
  WAANDISHI WA HABARI HAMFANYI MAKONGAMANO MKAELIMISHANA?
   
 12. Mulhat Mpunga

  Mulhat Mpunga JF-Expert Member

  #12
  May 25, 2012
  Joined: Oct 28, 2010
  Messages: 25,479
  Likes Received: 12,758
  Trophy Points: 280
  cheap labour ndo uzuri wake hivyo.pale si naskiaga ajira zao zimekaa kimagumashigumashi tu
   
 13. B

  BigMan JF-Expert Member

  #13
  May 25, 2012
  Joined: Feb 19, 2007
  Messages: 1,097
  Likes Received: 2
  Trophy Points: 135
  mwenye cv ya george marato jamani haiweke hapa jamvini
   
 14. B

  BigMan JF-Expert Member

  #14
  May 25, 2012
  Joined: Feb 19, 2007
  Messages: 1,097
  Likes Received: 2
  Trophy Points: 135

  sawa je hiyo habari isingeenda itv ingefungwa ? Navyofahamu pale it hakuna sub editor na kwa habari kama hiyo kiongozi wa editing room lazima hawajibike
   
 15. N

  Nick Sly Member

  #15
  May 26, 2012
  Joined: Jul 30, 2007
  Messages: 14
  Likes Received: 0
  Trophy Points: 3
  Napenda kumshukuru aliyeandika mada hii na kuwezesha kuchambuliwa kwa ufasaha na ufanisi mkubwa kutoka kwa wachangiaji. Tatizo langu kubwa ni lugha iliyotumika, hivi ni kweli wote waliotumia maneno ya Kiingereza walikosa tafsiri yake kwa Kiswahili? Au ndiyo ufisadi mwingine ndani ya Taifa katika matumizi ya lugha? Angalia sana unapokuwa mkosoaji kwani huenda nawe unahitaji kukosolewa ila hujijui. Tuache mawazo potofu ya kwamba ili ujulikane kuwa umesoma na kuelimika lazima utumie maneno ya Kiingereza katika maongezi yako. Wafaransa, Wajerumani, Wajapani, Warusi, Wachina n.k nao watasemaje? Tuelimike na tubadilike.
   
 16. Mshuza2

  Mshuza2 JF-Expert Member

  #16
  May 26, 2012
  Joined: Dec 27, 2010
  Messages: 4,115
  Likes Received: 1,745
  Trophy Points: 280
  Najihisi kama niko darasani..ndio raha ya JF, nimekubali waandishi tunao!
   
 17. Janjaweed

  Janjaweed JF-Expert Member

  #17
  May 26, 2012
  Joined: Jan 20, 2010
  Messages: 9,528
  Likes Received: 882
  Trophy Points: 280
  Weka yako na ww
   
 18. Chuma Chakavu

  Chuma Chakavu JF-Expert Member

  #18
  May 26, 2012
  Joined: Apr 16, 2011
  Messages: 1,524
  Likes Received: 5
  Trophy Points: 135
  HIVI huyu mleta mada na wengineo mnamsapoti mlikuwa wapi wakati cnn na media nyinginezo walipoonesha kunyongwa kwa saddam na kuuwawa kwa Gaddafi!? hamkuona au tuseme mlikuwa vipofu? mimi nadhani hizo ni chuki binafsi kwa itv na kasumba ya kuona kila lifanywalo na media za nje halina makosa nitakiri kuwa ni kosa kama hawakutoa tahadhari lakini kama wakitoa tahadhari na picha zikabaki zilezile hapo si kosa, ndio maana ya habari.
   
 19. Pascal Mayalla

  Pascal Mayalla JF-Expert Member

  #19
  May 26, 2012
  Joined: Sep 22, 2008
  Messages: 24,566
  Likes Received: 18,533
  Trophy Points: 280
  Chuma chakavu, ile picha ya Saadam iliibwa kwa simu, hakukuwepo na close up yoyote kuonyesha his dead body!. Zile picha za Ghadafi zilionyeshwa na Libya TV na wengine kuzinasa. Pamoja na hayo tabia mbovu ya Wastern media kuwa na double standards dhidi ya wasio wazungu tumeilalamikia sana humu jf. Wengine wetu mimi nikiwa mmoja wao, tulilaani mauaji ya Saadam, Ghadafi hadi Osama.

  Pamoja na chuki Wamarekani waliokuwa nayo dhidi ya Osama jee uliona any close-up shot ya mwili wake?. Kwa taarifa tuu, tukio lote limerokodiwa kwenye video zikionyesha kila kitu mpaka kila risasi ilipoingia in very close range, lakini wali censor nini cha kuonyesha na nini cha kuacha!.

  Hili la ukosoaji wowote kuuita ni chuki binafsi nalo ni tatizo!. Ukipenda chongo huita kengeza. Ukiwa na mapenzi makubwa na ukipendacho huwezi kuwa objective, mfano ni wapenzi wa Chadema humu jf ukiandika any critique dhidi ya Chadema unaishia kutukanwa na kauli kama hizi za chuki binafsi!.

  Siku zote mtoto anaependwa ndiye anaye kanywa tena kwa bakora. Inawezekana sisi wakosoaji ndio tunaosaidia zaidi kuliko hao wasifiaji kwa shangwe na mapambio.
   
 20. Mahanjam

  Mahanjam JF-Expert Member

  #20
  May 26, 2012
  Joined: Sep 3, 2009
  Messages: 325
  Likes Received: 26
  Trophy Points: 45
  Mazoea yana tabu! Sijui wanahisi kuwa ndo tunayotaka kuona? Taarifa inatosha hata wakirusha habari za ajali hali ni hiyo hiyo! They should know that kids also watch the news, EBO!
   
Loading...