Malilambwiga
JF-Expert Member
- Jul 19, 2015
- 485
- 296
Leo tarehe 26.09.2015 kituo cha ITV mtangazaji Sam Maela ameonekana akiruka kusoma vichwa vya habari vinavyoonyesha Lowassa kuongoza kwa asilimia 54 ktk utafiti wa TADIP.
Naomba kuwauliza ITV mmetishwa au ni makusudi. Unapoacha kusoma habari kuu tena iliyokolezwa kwa wino kisha unasoma habari ndogo kama kidokezo hamuitendei vyema taaluma yenu.
Kuna maana gani ya jina Independent Television
Naomba kuwauliza ITV mmetishwa au ni makusudi. Unapoacha kusoma habari kuu tena iliyokolezwa kwa wino kisha unasoma habari ndogo kama kidokezo hamuitendei vyema taaluma yenu.
Kuna maana gani ya jina Independent Television
Asubuhi nilikuwa nafuatilia habari za magazetini kutoka ITV. Najua ITV imepata pongezi kwa kutoa taarifa bila upendeleo. Lakini hili nililoliona leo hii linanipa shaka kwa mtangazaji ambaye nilikuwa namchukulia kama mtangazaji mahiri hapa nchini naye ni Sam Mahela. Yafuatayo niliyaona wakati anaripoti taarifa za kutoka magazetini.
1. Alianza na gazet la habari leo na kuripoti habari za vifo vya mahujaji na ndugu Kombani.....Hii iko sawa japo huwa
wanaanza na gazeti la Nipashe sijui kama ni utaratibu.
2. Habari za Lowasa na UKAWA hazikuripotiwa mfano Lowasa kidedea, Lowasa 54% Magufuli 40% hizi zilikuwa headlines
kwenye Tanzania daima na Majira lakini alizizima kwa makusudi.
3. Aliripoti habari za Magufuli kwenye Uhuru kuwa hakamatiki, na hali tete ya chadema kama ilivyoripotiwa na Uhuru.
Zaidi ya yote alikuwa ana ripoti habari ya Magufuli kwa upendeleo.
Yawezekana ni mtazamo wangu lakini nilichokiona kimenitia shaka weledi wa watangazaji wetu. Hata kama una mapenzi na chama au mgombea fulani usioneshe mahaba kwenye kuripoti kwani uko kazini na lazima uhheshimu taaluma yako.Naomba uongozi wa ITV /Radio one ukemee vitendo hivi na kuhakikisha habari zenye uzito ziripotiwe kama zilivyo kwenye vyombo vyao vya habari bila upendeleo. Wananchi tunahitaji taarifa sahihi ili tufanye maamuzi.
ITV endeleeni kuwa superbrand kwa kutokwenda nje ya mstari.