Main news story waliyoanza nayo ITV usiku huu wamedai JK na vyama vya siasa n.k wamekubaliana BMK lisitishwe mpaka baada ya uchaguzi mkuu.
Wakamweka John Cheyo, Mwenyekiti wa Taasisi ya Demokrasia, akisoma taarifa ya makubaliano hayo. Yeye kasema, very clearly tena kwa kurudia rudia, kwamba kura ya maoni imesitishwa mpaka baada ya uchaguzi.
Sasa kipi ni kipi, Bunge Maalum linasimama au linaendelea?
Hili stensheni la ITV linaajiri mijitu gani ya kutaarisha national news jamani?
Nimecheka sana mpaka mwanangu wa nursery anayejiandaa kwenda shule akaniuliza...baba mbona unacheka asubuhi kuna nini?Tbc nao ndio madudu zaidi. Uchanganyaji picha za matukio ni hovyo kabisa. Mtangazaji anasema'tupate taarifa kamili',taarifa haitokei,anabaki yeye kwenye screen katoa macho kama mjusi kabanwa na mlango. Hii inatokea kila siku kwenye taarifa ya habari!
Main news story waliyoanza nayo ITV usiku huu wamedai JK na vyama vya siasa n.k wamekubaliana BMK lisitishwe mpaka baada ya uchaguzi mkuu.
Hujalazimishwa kuangalia vituo ni vingi chagua kinacho kufurahisha.