ITV ipi habari kati ya vifo vya watu watu 3 na Rais kuongea na machinga au Makamba kumfukuza kazi msemaji wa Tanesco?

sifi leo

JF-Expert Member
Mar 30, 2012
5,013
8,369
Uhandishi wa habari ni taaluma, na Nina imani kwa walio isoma wataniunga mkono.

Nimewashangaa ITV leo, kwa mpangilio wa habari zao mpaka nikashindwa kuwaelewa katika kupanga habari lazima muangalie ni habari gani Ina masilai mapana ya nchi mfano, habari zinazo usu kuyumba kwa Hali ya amani nchini ni habari nyeti sana.

Habari ya vifo vya watu watu mkoani rukwa ni habari ambayo ilitakiwa kutangazwa mapema kabla ya kutujulisha yakuwa Raisi alikutana na machinga Ikulu na kuwapooza wasiandamane baada ya kuwafukuza kutoka mahali waliko kuwa wakifanyia biashara na kuwapeleka pahala penye changamoto.

Lakini habari ya kuuawa kwa Watanzania wenzetu na watu wasio julikana ni muhimu kuliko hii ya Makamba kumfukuza msemajii wa Tanesco kwa kutopokea simu za wateja wanao piga simu kuuliza Kwa Nini umeme umekatika Ili hali msemaji sio fundi wa jenereta.

Msemaji ni mzembe anashindwa kupokea simu na kuwajibu wananchi yakuwa umeme unakatika kwa sababu sasahiv ni serikali ya awamu ya 6 Iko madarakani kipindi kire ilikuwa ya awamu ya Tano.
 
Makamba kumfukuza msemajii wa Tanesco kwa kutopokea simu za wateja wanao piga simu kuuliza Kwa Nini umeme umekatika Ili hali msemaji sio fundi wa jenereta
 
Swali ni je ni kweli kitengo hicho cha mawasiliano ndiyo tatizo kwenye shirika?
Hao wanapukutua na kupukuchua majani, ilhali mashina na mizizi ya matatizo yangali intact! Shame!


 
Sijui nani alitukaririsha kua habari kutoka ikulu iwe ndio habari ya kuanza nayo, au kuweka kwenye muhtasari
 
Uhandishi wa habari ni taaluma, na Nina imani kwa walio isoma wataniunga mkono.

Nimewashangaa ITV leo, kwa mpangilio wa habari zao mpaka nikashindwa kuwaelewa katika kupanga habari lazima muangalie ni habari gani Ina masilai mapana ya nchi mfano, habari zinazo usu kuyumba kwa Hali ya amani nchini ni habari nyeti sana...
Kwanza rekebisha hapo katika Neno Uhandishi wa Habari na liwe Uandishi wa Habari sawa?

Pili ukitaka uelewe ni kwanini ITV na Television zingine ( na za Kimataifa ) hupenda kuanza na Habari za Marais au Viongozi tafuta Kitabu cha Journalism kilichoandikwa na Author Melvin Mencher hasa Kipengele Muhimu cha NEWS VALUES naamini hutorudia tena Kuwashangaa hawa Super Brand ITV Tanzania.

au nitafute nikupige Journalism Course.
 
Kwanza rekebisha hapo katika Neno Uhandishi wa Habari na liwe Uandishi wa Habari sawa...
Kipi chenye value vifo vya watu watatu tena vifo vya watu waliouawa na wasio julikana? Au Rais kuongea na kundi jipya maalumu aliro liongeza yeye? Hacheni kukalili walichokiandika watu zamani Tena wazungu journalism kozi siitaji mkuu.
 
Kipi chenye value vifo vya watu watatu tena vifo vya watu waliouawa na wasio julikana? Au Rais kuongea na kundi jipya maalumu aliro liongeza yeye? Hacheni kukalili walichokiandika watu zamani Tena wazungu journalism kozi siitaji mkuu.
Mara hii umeshamaliza Kukisoma Kitabu cha Journalism cha Author Melvin Mencher?

Mbona hii response yako inaonyesha kuwa hujakisoma na kama umekisoma basi hujakielewa?
 
Back
Top Bottom