H1N1
JF-Expert Member
- May 29, 2009
- 4,217
- 1,579
haya ndiyo matatizo ya uhuru wa kutoa maoni kila mmoja anaelewa atakavyo,nini maana ya kukebehi ? kama maudhui ya kilichoonyeshwa kinamuudhi mtu hiyo si tatizo la ITV ni tatizo la anaudhika,tufikie pahara tukubali kutokubaliana kwa amani, huyu anayedhani ITV wameonyesha kipindi kisichofaa yeye ndiye mwenye matatizo na anakebehi vipindi vya ITV. ndani ya ITV kuna vipindi vingi sana na vingine "vinakebehi" misimamo na matakwa ya mtu mmoja mmoja au kundi fulani na kufurahisha au kuelimisha kundi jingine. Ni vema tuwe na utamaduni wa kutafakari na kukubali changamoto ambazo wengine huziona ni kebehi... UHURU WA KUTOA MAONI si lazima maoni yawe ni ya kufurahisha jamii nzima, kwa mtazamo wangu maoni yako kuhusu ITV na Zanzibar ni kuwadhalilisha wazanzibar kanakwamba uwezo wao wa kufikiri ni pungufu