ITV hizi ni kanzu ! | JamiiForums | The Home of Great Thinkers

Dismiss Notice
You are browsing this site as a guest. It takes 2 minutes to CREATE AN ACCOUNT and less than 1 minute to LOGIN

ITV hizi ni kanzu !

Discussion in 'Habari na Hoja mchanganyiko' started by Ndebile, Nov 28, 2011.

 1. Ndebile

  Ndebile JF-Expert Member

  #1
  Nov 28, 2011
  Joined: Sep 14, 2011
  Messages: 3,632
  Likes Received: 1,991
  Trophy Points: 280
  katika mchezo wa mpira wa miguu kuna aina ya chenga inayofahamika kama kanzu,mpira unapitishwa utosini na adui yako. Taarifa ya habari ya saa mbili leo usiku kuna habari mbili ambazo mkuu wa wilaya ya musoma(naomba kusahihishwa) na mkurugenzi wa soko la samaki feli walipigwa makanzu! Mkuu wa wilaya aliulizwa kuhusu janga la njaa kwa wakazi wa wilaya yake huku tayari mwandishi ameisha kusanya taarifa zinazoonyesha watu wanakula mboga za majani na kumbikumbi kama mlo na mwenyekiti wa kijiji kuthibitisha hali hiyo. Alipoulizwa mkuu wa wilaya alikataa na kuziita habari hizo UZUSHI. Huko feri jamaa(bosi) alishtukia chenga na kuomba aonyeshwe picha za video walizopiga awali na ndipo ajibu maswali ya mwandishi kuhusu kukithili kwa uchafu kwenye soko hilo,nadhani hakuonyeshwa na kilichotokea ni majibu ya uongo.

  Nimependa ubunifu huu,unapiga picha tukio,then unamuuliza bosi mpenda kukaa ofisini. Majibu tofauti na hali halisi!
   
 2. bayonamperembi

  bayonamperembi JF-Expert Member

  #2
  Nov 29, 2011
  Joined: Nov 16, 2011
  Messages: 282
  Likes Received: 50
  Trophy Points: 45
  Duh! kumbe ITV ipo! nina miezi mitatu huku Arusha haijaonekana tangu walipokata mawasiliano. wanaoweza kuona labda ni wenye satelite receiver tu. inaudhi Tv station kubwa km hiyo inashindwa kurudisha huduma kwa zaidi ya miezi mitatu sasa sijui wanatufikiriaje sisi tunaotumia antena za kawaida. it is big shame on you.
   
 3. Don Mangi

  Don Mangi JF-Expert Member

  #3
  Nov 29, 2011
  Joined: Nov 1, 2010
  Messages: 2,206
  Likes Received: 93
  Trophy Points: 145
  mwenyewe niliipenda hiyo...kwa kweli mkuu wa wilaya wakati anajibu na mwanya wake ule unaona kabisa anaongea uwongo kwasababu wadau tushaonyeshwa watu wakila kumbi kumbi huku viongozi wao wakisubiria kwa bashasha kusherekea miaka hamsini ya uhuru...
  Big up ITV nimeipenda style yao hyo
   
 4. cartura

  cartura JF-Expert Member

  #4
  Nov 29, 2011
  Joined: Aug 13, 2009
  Messages: 3,049
  Likes Received: 16
  Trophy Points: 0
  this was sooo good... yaani mkuu ameingizwa kwenye choo cha kike big time; nasubiri kwa hamu kuona hatua zitakazochukuliwa na mamlaka yake ya nidhamu/uteuzi
   
 5. Faru Kabula

  Faru Kabula JF-Expert Member

  #5
  Nov 29, 2011
  Joined: Mar 26, 2009
  Messages: 10,642
  Likes Received: 2,875
  Trophy Points: 280
  'Watawala' wataanza kuikwepa ITV
   
 6. The Finest

  The Finest JF-Expert Member

  #6
  Nov 29, 2011
  Joined: Jul 14, 2010
  Messages: 21,709
  Likes Received: 43
  Trophy Points: 145
  Aisee na mimi nimeiona ITV jana nimecheka sana yule Mkuu wa Soko la Feri anakataa kuwa soko la feri si chafu wakati kuna picha kabisa zinaonyesha kuwa soko ni chafu, halafu bwana afya naye amemkaanga baada ya kukiri kuwa soko ni chafu na aliishatuma barua kwenye halmashauri kuwafahamisha tokea mwezi wa kumi
   
 7. Wisdom

  Wisdom JF-Expert Member

  #7
  Nov 29, 2011
  Joined: Sep 28, 2010
  Messages: 473
  Likes Received: 0
  Trophy Points: 0
  Acha kulalamika analogue inaondoka hamia digital kwa kununua king'amuzi
   
 8. Remote

  Remote JF-Expert Member

  #8
  Nov 29, 2011
  Joined: May 20, 2011
  Messages: 14,875
  Likes Received: 1,562
  Trophy Points: 280
  alafu mkuu wa wilaya still analeta siasa zake kwamba hakuna watu watakaokufa njaa wakati watu wanashndia kumbkumb na majani ya porini, 50yrz of independence.
   
 9. Julieth Ms

  Julieth Ms Senior Member

  #9
  Nov 29, 2011
  Joined: Nov 29, 2011
  Messages: 102
  Likes Received: 0
  Trophy Points: 0
  Enzi za Lowasa hawa jamaa wangesimamishwa kazi papo kwa papo.
  Mtumishi wa umma lazima utoke ofisini kwenda kuhudumia wananchi sio kukaa ofisini tu unaangalia mafaili.
   
 10. s

  sawabho JF-Expert Member

  #10
  Nov 29, 2011
  Joined: Feb 25, 2011
  Messages: 4,504
  Likes Received: 946
  Trophy Points: 280
  Mbuzi hula kulingana na urefu wa kamba yake, afadhali yeye ana antanae ya kawaida. Mimi nina ile ya tube light za umeme, yaani kwisha kabisa.
   
 11. YEYE

  YEYE JF-Expert Member

  #11
  Nov 29, 2011
  Joined: Nov 12, 2011
  Messages: 440
  Likes Received: 2
  Trophy Points: 0
  kuna issue nyingine ni za ajabu sana, sa mkuu wa wilaya anapodai ni uzushi wakati watu wananjaa kweli sijui anaogopa nini kusema ukweli?!..kwenye katiba mpya inabidi hivi vyeo vya ukuu wa mkoa na wilaya vifutwe ni mizigo kwa taifa
   
 12. wapalepale

  wapalepale JF-Expert Member

  #12
  Nov 29, 2011
  Joined: Mar 21, 2011
  Messages: 259
  Likes Received: 20
  Trophy Points: 33
  daaaah nilicheka sana jana!!!! endapo angeziona zile picha kabla asingejibu uongo ule!!!!!!!!
   
 13. ndyoko

  ndyoko JF-Expert Member

  #13
  Nov 29, 2011
  Joined: Nov 2, 2010
  Messages: 4,974
  Likes Received: 279
  Trophy Points: 180
  jamani kampeni badooooooooooooo! mbona mntaka kuanza mapema sana, kuna miaka m4 mbele from now, mweeeeeeee!
   
 14. ndyoko

  ndyoko JF-Expert Member

  #14
  Nov 29, 2011
  Joined: Nov 2, 2010
  Messages: 4,974
  Likes Received: 279
  Trophy Points: 180
  Umenikumbusha ile sinema ya mapanki, na makanusho ya mzee wa 'kaya'
   
 15. ndyoko

  ndyoko JF-Expert Member

  #15
  Nov 29, 2011
  Joined: Nov 2, 2010
  Messages: 4,974
  Likes Received: 279
  Trophy Points: 180
  Kiutendaji serikalini, hao mpaparazi kwa 'case' ya uchafu wa soko, mtu sahihi wa kulisemea hilo alikuwa DED. nadhani huyo DC alijiingiza kulisemea hilo for the sake of publicity, na yamemkuta ya kumkuta. Angekuwa mjanja angelitupia hilo swali kwa yule afisa afya, then yeye angekuwa safe. kimsingi DC huwa hana bajeti ya usafi wa soko, mtekelezaji wa hilo ni DED. Kimbelembele kimemponza!
   
 16. bht

  bht JF-Expert Member

  #16
  Nov 29, 2011
  Joined: May 14, 2009
  Messages: 10,341
  Likes Received: 209
  Trophy Points: 160
  Mkuu wa soko alitokwa na macho kaa pima!! amejikalia tu ofini anatafuna vibua kila siku hata hajui wanaomenyeka n akutozwa ushuru wanapata tabu kiasi gani.

  watendaji wetu ni maboksi matupu kabisa....

  soko limeoza na linanuka halafu lijitu zembe linabisha!!! hawa ndo wakutandika bakora kabisa
   
 17. Borakufa

  Borakufa JF-Expert Member

  #17
  Nov 29, 2011
  Joined: May 26, 2011
  Messages: 1,503
  Likes Received: 5
  Trophy Points: 0
  Wewe upo dunia ipi! unatakiwa kuwa na king'amuzi chao ndo utawabamba otherwise huko kwenye antena hawarudi tena kwani lisirikali lenu limewapiga marufuku
   
 18. Don Mangi

  Don Mangi JF-Expert Member

  #18
  Nov 29, 2011
  Joined: Nov 1, 2010
  Messages: 2,206
  Likes Received: 93
  Trophy Points: 145
  enzi zipi za lowasa?
   
 19. bayonamperembi

  bayonamperembi JF-Expert Member

  #19
  Nov 30, 2011
  Joined: Nov 16, 2011
  Messages: 282
  Likes Received: 50
  Trophy Points: 45
  Borakufa;2900483]Wewe upo dunia ipi! unatakiwa kuwa na king'amuzi chao ndo utawabamba otherwise huko kwenye antena hawarudi tena kwani lisirikali lenu limewapiga marufuku

  ninavyojua hadi sasa ITV hawana king'amuzi chao zaidi ya vile vya Startimes (TBC) & Ting (ATN) na hivi ving'amuzi havina chanel zote za bongo. please help me km kuna anaejua ving'amuzi vingine vyenye chanel zote za bongo.
   
 20. Yo Yo

  Yo Yo JF-Expert Member

  #20
  Nov 30, 2011
  Joined: May 31, 2008
  Messages: 11,247
  Likes Received: 73
  Trophy Points: 0
  Hii ndio calibre ya viongozi wetu.......kila kitu ukiwaambia wanakuambia ni uzushi na wivu......sasa ona jamaa walivyoaibika.....
   
Loading...