ITV hakika kwa kikosi hiki nyie ni SUPER BRAND!

MINOCYCLINE

JF-Expert Member
Apr 2, 2015
8,018
16,801
  1. Jackline Silemu.
  2. Zainab Chondo.
  3. Farhia Mildred.
  4. Shamim Mlacha.
  5. Magreth Cosmas.
nilikuwa siyo mpenzi wa kuangalia taarifa zenu za habari lakini siku hizi nipo radhi niache hata kula chakula nitizame habari ITV saa 2 kamili usiku kwani najua nikifungua tu nitamkuta mmoja wa hao niliowataja hapo juu. nitoe tu rai yangu kwenu uongozi wa ITV naomba hao watangazaji muwaongezee mshahara na ikibidi muwalee vizuri huku mkiwadekeza ili wabaki hapo kwani nisipoona mmoja wapo kati ya hao anasoma news bulletin ya saa 2 mbili kamili usiku basi naachana nanyi na narudi zangu kuangalia runinga zinazojielewa kama CNN, BBC, SKY NEWS, FOX, AL JAZEERA, RT, CCTV, DW, SABC na I24.

labda kwa kuanzia tu naomba mnisaidie kuniambia nani kati ya hao juu hapo anategemea kusoma taarifa ya habari ya kesho jumapili tarehe 7, february 2016? kwa kikosi hicho murua kabisa sasa nimejua kwanini mtangazaji Fatma Almasi Nyangasa alikimbia hapo huku mwanadada Ufo Saro akipotezwa kabisa. shikamoo ITV hakika nyie ni Super Brand.
 
Namba moja na namba tatu nawakubali sana kwa kweli ila lakini godwin gondwe ndo kinara wa woooote hapo ITV ila sam mahela anakuja vizuri sana pia kwa habari za saa mbili.
 
Farhia middle bonge moja la msomaji huyu mlacha anakodoa mimacho tu yy ni km muoga hivi wa Kamera anababaika mda mwingine
 
Namba moja na namba tatu nawakubali sana kwa kweli ila lakini godwin gondwe ndo kinara wa woooote hapo ITV ila sam mahela anakuja vizuri sana pia kwa habari za saa mbili.

mkuu huyo godwin gondwe na sam mahela wako ni wanawake? muwe mnasoma basi uzi kwa uangalifu mkubwa ila mkiwa mnajibu msitoke katika mstari. hata hivyo nakushukuru kwa juhudi zako za kujitutumua kujibu.
 
Hakuna mahali ume recommend kuwa tuwajadili wanawake tu! Labda ungekuwa umetanabaisha kuwa tuijadili jinsia moja tu, zaid nimefikiri hao ndio the best kwako sikujua kama anazaid ya hapo, bt umeeleweka kijana
 
ITV wana Watangazaji wazuri sana sijui huwa wanawatoa wapi.....
Tatizo la ITV ni ubora wa picha na sauti, Mengi wekeza kwenye hiyo studio wape Kamera mpya
 
  1. Jackline Silemu.
  2. Zainab Chondo.
  3. Farhia Mildred.
  4. Shamim Mlacha.
  5. Magreth Cosmas.
nilikuwa siyo mpenzi wa kuangalia taarifa zenu za habari lakini siku hizi nipo radhi niache hata kula chakula nitizame habari ITV saa 2 kamili usiku kwani najua nikifungua tu nitamkuta mmoja wa hao niliowataja hapo juu. nitoe tu rai yangu kwenu uongozi wa ITV naomba hao watangazaji muwaongezee mshahara na ikibidi muwalee vizuri huku mkiwadekeza ili wabaki hapo kwani nisipoona mmoja wapo kati ya hao anasoma news bulletin ya saa 2 mbili kamili usiku basi naachana nanyi na narudi zangu kuangalia runinga zinazojielewa kama CNN, BBC, SKY NEWS, FOX, AL JAZEERA, RT, CCTV, DW, SABC na I24.

labda kwa kuanzia tu naomba mnisaidie kuniambia nani kati ya hao juu hapo anategemea kusoma taarifa ya habari ya kesho jumapili tarehe 7, february 2016? kwa kikosi hicho murua kabisa sasa nimejua kwanini mtangazaji Fatma Almasi Nyangasa alikimbia hapo huku mwanadada Ufo Saro akipotezwa kabisa. shikamoo ITV hakika nyie ni Super Brand.
Kama unadhani BBC, CNN, ALJAZEERA, FOX ni tv zinazojielewa, basi wewe ndio hujitambui. Kwa habari za nyumbani Azam two.
 
Ni FarhiavMiddle sio Farhia Midred. Huyu mdada anaonekana mtamu sana kwenye mambo yenu yaleeeeeeeee.... Mi kiukweli sipati raha ya kutazama TV akiwepo.
 
ITV wako vizuri,
udhaifu ninaouona, taarifa zao nyingi zimejaa mambo mabaya tu yanayoipata jamii yetu, kipindupindu,mafuriko,ufisadi,wizi,ajali,migogoro,magonjwa mbalimbali, hizi ni nzuri na tunaipenda lkn ni vizuri pia kuyapa au kuongeza coverage mambo makubwa mazuri + yanayoendelea ktk jamii yetu.
vinginevyo tutakuwa kama mashirika ya magharibi CNN,BBC,SKY,ITV,etc wanavyoitangaza afrika kwa ndugu zao, ni shida tu.
 
Mtoa mada inaonyesha aliona ITV miaka 4 iliyopita,Zainab Chondo ana zaidi ya miaka mitatu hayupo hapo,Ulikuwa ALBANIA nini
 
Tangu rais mstaafu aseme kuna vijana 49 walipewa kazi maalumu kufanya promotion, nyuzi kama hizi naziona zinaangukia humo humo. Anyways, sio jambo baya pia!
 
Back
Top Bottom