ITV, Azam, na Channel 10 jiungeni na dira ya Dunia

ITV, Azam, na Channel 10 jiungeni na dira ya Dunia

Bome-e

JF-Expert Member
Joined
Jan 3, 2014
Posts
17,327
Reaction score
26,572
Ombi kwa vyombo tajwa hapo juu,kila ifikapo SAA 3 huwa lazima niangalie dira ya dunia kama niko nyumbani au sehemu yenye access na TV!
Hivi karibuni star TV nimejikuta(tumejikuta) nikiichukia kutokana na chombo hicho kupoteza weledi wa kazi yao na kuwa kama TV ya chama!Hii ni kutokana na matangazo yake ambayo yamekuwa yakikiuka taratibu za utoaji habari ikiwa ni pamoja na kueneza propaganda za kihuni lengo likiwa kuchafua upande mmoja!Wengi ni mashahidi wa hili!
Hivyo basi katika tathimini niliyoifanya nimeona ni hivyo vyombo vitatu vilivyobaki kwenye misingi ya utoaji habari kwa haki!

Kwakuwa nakipenda sana kipindi hicho cha dira ya dunia ambapo naamini wengi wa watanzania wanakipenda,naomba basi muangalie uwezekano (ITV,azam na Chanel 10) wa kuwa mnajiunga na BBC ili watu tuache kuangalia kabisa star TV!
Iwapo mtafanya hili mtajiongezea watazamaji lukuki ambao huwa wanajiunga na star TV kuangalia dira ya dunia!
Wahusika naamini mpo JF,chukulieni hii kama fursa ya kujipanua zaidi!
Nawasilisha!
 
Tumekusikia. Ila unashauliwa kuangalia chaneli nyingine sio lazima uangalie star tv. Na kama unamalalamiko wasiliana na wahusika. Sio kuleta apa jamvini
 
chanel 10 nayo hivyo hivyo hapo wa kuaminika na itv pekee yake.na azam inakuja
 
Tumekusikia. Ila unashauliwa kuangalia chaneli nyingine sio lazima uangalie star tv. Na kama unamalalamiko wasiliana na wahusika. Sio kuleta apa jamvini

Huelewi?Hakuna kipindi cha matukio ya kimataifa bora Tanzania kama BBC Swahili,hapo unapata habari katika ubora wake!Star TV huwa wanajiunga na kipindi hicho,hapa nimewaomba Chanel nyingine waangalie uwezekano wa kuwa wanajiunga na BBC!
Kama una fikra fupi kama wewe huwezi elewa mantiki yangu hapa,Naua ndege wawili kwa jiwe moja!Lengo la pili hii ni namna ya kuwaambia star TV wajirekebishe!
Hivi hata lugha ya mazingira huelewi,tafakari kabla ya kukurupuka kujibu!
 
Ok. Kwani iyo bbc swahili ni muda wote ?? Si hadi sa 3 usiku. Mi naona ikifika sa tatu anaglia iyo bbc. Kisha habari zikiisha unahamisha chaneli. Mi sijawahi kuona wakiwa kwenye kipindi cha bbc kisha apo apo wakaleta habali za ccm au zisizo husiana na bbc.
 
Akasali kesho ni jumapili, asije akaanza kuabudu media. Aende kanisani akitoka apumzike nyumbani na familia yake, aendelee siku za kazi za kawaida!. Au hawaamini wasalishaji/mapadre? kwakuwa alisema wanahongwa!. Ana siku nyingi tu za kuongea atakavyo, lakini kesho aende kanisani akasali ndpo aendelee na mambo yake. Au siku hizi ameanza kuabudu maredio na materevisheni?

Sorry!, hiki kipande kinahusu ile topic ya dr slaa kesho jumapili saa 3 asb kuwepo azam tv kwenye mahojiano, nmejaribu kuifuta nmeshndwa, nmetumia simu ndogo kuandika na bahati mbaya simu haionyeshi mahala pa ku 'delele reply'
 
Ok. Kwani iyo bbc swahili ni muda wote ?? Si hadi sa 3 usiku. Mi naona ikifika sa tatu anaglia iyo bbc. Kisha habari zikiisha unahamisha chaneli. Mi sijawahi kuona wakiwa kwenye kipindi cha bbc kisha apo apo wakaleta habali za ccm au zisizo husiana na bbc.

Ratiba yangu huwa saa 1 Chanel 10,SAA 2 ITV,SAA 3.00 -3.30 star TV!
Sasa jana ile nahamia star tv saa 3 ndio nikakutana na tangazo lililonikwaza sana!Hivi hata kwenye matangazo ya biashara,mfano unauza omo!Unaweza onyesha foma haifai ila Omo ndio inafaa!Kwa uzoefu wangu ni kinyume kisheria kutangaza bidhaa ya mwenzako haifai kwenye matangazo ya kibiashara!Unachotakiwa kufanya ni kuonesha ubora wa bidhaa yako lakini si kukashifu ya mwenzako!
TCRA nao wamekuwa kimya,ujinga nchi ni hadi kwa walioelimika!
 
Wakishajua mmehama wataanza kupachika matangazo hayo,BY the way kwa upuuzi wao hata hiyo BBC nimeitupilia mbali sitaki kuisikia hii chaneli ya MAFUTUHI
Ok. Kwani iyo bbc swahili ni muda wote ?? Si hadi sa 3 usiku. Mi naona ikifika sa tatu anaglia iyo bbc. Kisha habari zikiisha unahamisha chaneli. Mi sijawahi kuona wakiwa kwenye kipindi cha bbc kisha apo apo wakaleta habali za ccm au zisizo husiana na bbc.
 
Ivi ushawahi kuisikiliza. Redio. Kahama?? Na hata sasaivi tambua uharisia wa vyombo vya habari kalibia vyote vimepoteza uzalendo kila mtu natoa habari kulingana na upendo wake wa kimaslahi. Mfano tanzania daima. Haliwezi likaponda habari za chadema. Pia uhuru nalo haliwezi ponda habari za ccm. Ivyo anaemiliki star tv ni moja ya tim ya kampen ya ccm. Ivyo hawezi kuwa. Balans razma aegemee upande m1. Pia mwenye redio kahama ni lembeli nae analusha habari za chadema tu
 
Huelewi?Hakuna kipindi cha matukio ya kimataifa bora Tanzania kama BBC Swahili,hapo unapata habari katika ubora wake!Star TV huwa wanajiunga na kipindi hicho,hapa nimewaomba Chanel nyingine waangalie uwezekano wa kuwa wanajiunga na BBC!
Kama una fikra fupi kama wewe huwezi elewa mantiki yangu hapa,Naua ndege wawili kwa jiwe moja!Lengo la pili hii ni namna ya kuwaambia star TV wajirekebishe!
Hivi hata lugha ya mazingira huelewi,tafakari kabla ya kukurupuka kujibu!
Nunua kisimbusi cha azam wana station zaidi ya moja inayorusha BBC Swahili,eg qtv
 
Back
Top Bottom