Itungwe sheria kudhibiti tabia ya vigogo serikali kutumia magari ya serikali baada ya saa kazi kama kwenda nayo Bar

Nafikiri wakati umefika tuwe na sheri itakayozuia vigogo wa serikali kutumia magari ya serikali kwa shughuli au mambo binafsi kama kwenda nayo Bar au sehemu zingine za starehe huku madereva wakibaki ndani ya magari kusubiri mabosi wamalize starehe zao.
una hoja nzuri sana ingawa kuna watu wengine wanakua kwenye idara nyeti,kazi nyeti au maalum,inawezekana kuja kula na kurudi ofisini
 
Nafikiri wakati umefika tuwe na sheri itakayozuia vigogo wa serikali kutumia magari ya serikali kwa shughuli au mambo binafsi kama kwenda nayo Bar au sehemu zingine za starehe huku madereva wakibaki ndani ya magari kusubiri mabosi wamalize starehe zao.

Hapa napoandika niko kwenye mgawahawa mmoja maarufu katika mkoa fulani na kuna kigogo mmoja kaingia muda tu na yeye sasa hivi anapata kinywaji na mazagazaga mengine huku dereva wake yuko ndani ya gari(shangingi) akiwa anamsubiri.

Binafsi hata ningekuwa boss hili jambo mimi nisingeweza kulifanya kabisa kwani kwanza nisingejisikia huru na pia hata nafsi yangu isingeridhika na kwakeli siwezi kuwa comfortable hata kama ningekuwa na madaraka makubwa kama ya huyu kigogo.


Mimi nashauri tupitishe sheria kali itakayoambata na adahabu kali ikiwemo demotion kwa vigogo watakaokiuka sheria hii au serikali itoe waraka mzito kwa mabosi wote serikalini pamoja na watumishi wengine wa umma wanaotumia magari ya serikali.

Sheria iruhusu matumizi ya aina hii kwa magari ya serikali pale tu panapokuwa na sababu maalumu kama vile mtumishi kuwa kwenye safari ya kikazi,n.k lakini wawe na vibali maalumu.


Sometimes huwa najiuliza hivi mataifa yote duniani yakiwamo yale yaliyoendelea kuna tabia kama hii kwa viongozi wa serikali na wale wa taasisi za serikali?

Ningekuwa Raisi wa nchi hii ningeshusha waraka mzito ambao ungewahusu kuanzia mawaziri mpaka wakurugenzi na kama sheria inawabeba basi ningepeleka Bungeni muswaada wa marekebisho kwa lengo la kufuta huu umangimeza unaochangia matumizi mabaya ya fedha za umma.
Mi nipo bar na stl bado.
 
Nakuunga mkono, sio Ya serikali tu, hata vyama vya siasa, yasitumike kwa shughuli binafsi, nazo ni kodi zetu
 
Back
Top Bottom