Its My Wedding Annivesary

Hongera sana mkuu.
Sina mengi ya kusema maana
mimi ndo kwanza nina miezi 8 kwenye hiyo club.
Nawatakia siku njema.

Nyie bado mko kwenye honey moon.

Mtunze mwenzako and it shall all be well with you.

Ndoa ni baraka toka kwa Mwenyezi Mungu maana ndio the very first institution ktk historia ya mwanadamu.
 
Asante sana kwa ushauri wako mkuu, be blessed.
 
Wana JF nimeona nisikae kimya bila kuwajuza wema wa Mungu kwangu.

Najua wengine mtakuwa mmevaa kijani/njano kusherekea "chama chetu cha mapinduziiii chajenga nchi" (itikia ni wimbo) huku wengine (pengine) mmevaa nguo nyeusi kuashiria maombolezo kitaifa.

Leo ninatimiza miaka 11 toka nimekula kiapo cha kuishi (kama mume na mke) na huyu mdada.
Tulikutana 1994 na ndoa ikafungwa miaka 6 baadae
Ndani ya miaka hii 11 Mungu kanijalia kuwa baba wa boy-10 na girl-7 na ukiwaangalia ni dhahiri hakunichakachua labda awe amechakachua na mdogo wangu, hahaahahaaa!!!

Ni miaka ya kuishi na mwanamke ambaye alichukua nafasi ya mama na dada yangu katika maisha.

Miaka 11 imenifundisha nisimwamini kila mtu ninaposigana na mke wangu. Nakumbuka in our early years niliwahi kushare na mchungaji juu ya tofauti zangu na mke wangu only for the pastor to use my story in his preaching the next sunday. Siku hizi nayasovu mwenyewe tu, no outsiders!

Miaka 11 ya kutambua kwamba vitu vidogo sana (thanks, sorry, karibu, darling..) vinajenga uhusiano na vitu vidogo pia huwasha moto.

Jamani wakati mwenzenu nashereheka 11 years kuna experience zipi (nzuri/mbaya/vituko) umewahi pitia kwenye mahusiano yako.

Karibuni tuzungumze!!!!!!!!!!!!!!!!

Real Man,

Kwanza nikupe hongera kwa kutimiza miaka hiyo 11 na hongera hizi pia zimfikie Mkeo.

Pili, nikupongeze na kukuuliza pia hapo kwenye red umeweza kutambua nafasi yake kwako na sijui umetambuaje,ilikuwa lini ?, Na kwa sababu hiyo je umemshukuru au unamshukuru kwa namna gani?

Tatu,hapo kwenye blue nikusihi usiache kutimiza wajibu wako kila siku na leo pia wakati mnapongezana usiyasahau hayo maneno.Nashukuru sana kwa kunikumbusha hasa hapo kwenye red na blue naminiko kwenye ndoa kwa muda wa miaka mitano sasa nafuata nyayo zako.

Mungu akujalie maisha marefu yenye mafanikio tele wewe,mkeo na watoto wenu.

Mbarikiwe sana
 
Mwenzetu Nakushukuru sana kwa kututakia heri.

Kuhusu wife kuchukua nafasi ya mama na dada yangu ni swali gumu kwa vile si rahisi kuelezea ila ilikuwa ni process. Tuli-date for 6yrs lakini akiwa kwao, nikiwa kwangu. Utamjua kwa sehemu ndogo sana during dating bila kujali ni muda mrefu kiasi gani.
Sasa mgogoro unakuja baada ya ndoa pale unapotarajia a-behave kama mama yako au dada simply because nimelelewa na kukua karibu na hawa watu wawili.

Mama yuko vile kwa sababu yeye ni mke wa baba na wanaume wengi huwa tunatarajia the same wakati mke wangu amelelewa akimwona mwanamke (mama yake) tofauti na mama yangu anavyo-behave kwa mume wake.

Ni pale nilipokubali kwamba she can not act as my mother maana si mama yangu ndipo uhusiano wetu ukawa released to higher levels kwa sababu sijaribu tena kuleta vigezo/kumlinganisha na mama yangu. Kumbe issue ni kutengeneza your own brand na si lazima iwe replica ya baba na mama.

Process hii ilikuwa 18 months za mwanzo ktk ndoa ingawa haimaanishi kwa we were just fighting.

Huwa napenda kumshukuru kwa vitu vigogo vidogo kama kumpa first priority, compliments, unexpected lunch box, a bouquet of flower, namwagia maji on her birth days, out of home love making n.k. Ila niliwahi (out of the little resources) kujipinda mtoto wa kiume nikamnunulia kiusafiri.

Asante kwa kunitia moyo na Mungu anisaidie kutimiza wajibu wangu as a husband and father!!!
 
RealMan hongera sana hapo sasa ndio usilegeze kamba kaza buti ndio upo kwenye kile kipindi kila mtu anakisema ni kigumu ajabu 10-20 yrs of mariage.
Sina matatizo mengine ambayo yanawaface wanandoa wengi kama sijui gubu, uchoyo, kiburi,heshima yako sawasawa,tatizo ni cheating tu,mimi niliishi kama niko paradise na mme wangu na watoto wetu pia mpaka ilipotimu miaka 12 kwenda 13.kivumbi kikaanza ila naona kwenye swala zima la ndoa mwanaume ndio anaweza kufanya ndoa ikawa stable au ikateteleka sababu ni kama ameshika mpini wa jembe na mwanamke kashika kwenye makali.
Kwa hiyo jitahidi sana kwenye hili la cheating maana naona ndio tatizo sugu ambalo majeraha yake kuyatibu si kazi ndogo.
HAPPY ANNIVERSARY :clap2::clap2::clap2::clap2::clap2::clap2:
 
Hongera Realman.....nimejifunza kutoka kwako.....mpe hongera zetu na wifi....Mungu aendelee kuwatunza na familia yako.
 
Gaga!!!!!!
Thank you very much, maneno yako yamejaa ukweli 100%.
Nitaweka tahadhari dada yangu maana wanasema aliyesimama aangalie asianguke.

Na ni kweli pia sisi wanaume ni chanzo cha uimara ama kutetereka kwa ndoa nyingi. Hatuko on the receiving end na pengine ndio maana tunajisahau.

Unadhani kwa nini baadhi ya wanaume wanabadilika ktk kipindi hiki (10-20)??

Asante kwa kushea experience yako maana inatujenga wengine, tumeona kina Msindima ndo kwanza ana 8months.
 
Asante sasa Sister!

Toka nimejoin JF ni kama kukutana na ndugu yako mlokuwa hamfahamiani.
Wifi atapata salaam maana siku hizi akiona nacheka huku nimeshika simu husema "Jamii Forums hao"!!!!!!!!
 
Hongera, mkuu nakutakia uzima ili uje utujuze tena kwenye your 50th Annivesary

Thanks VoR,

Kama Mungu anatupa uzima wote wawili, 50th anniversary ntakuwa kibabu fulani hivi natoa nasaha kwa wajukuu.
 
Ups and Downs tumezipitia kwa kweli.

Ujauzito wake wa kwanza was like hell to me, she was too moody.
Kaka nimewahi kuamka saa 8 usiku nikatafute kuku wa kuchoma, mwanaume nikaingia mtaani!!

Real Love! Hongera kaka :clap2: :clap2: :clap2: :clap2: :clap2: :clap2: :clap2: :clap2: :clap2: :clap2: :clap2:
 
Mkuu hongera sana.......sio mchezo.
Im sure mtakua mna kula raha tu saa hizi
 
Asante sana B,

Leo tunapeana special treat,
Hatukutaka kwenda nje ya nyumbani basi watoto wanatucheka jinsi tunavyofanya vituko
 
Wana JF nimeona nisikae kimya bila kuwajuza wema wa Mungu kwangu.

Najua wengine mtakuwa mmevaa kijani/njano kusherekea "chama chetu cha mapinduziiii chajenga nchi" (itikia ni wimbo) huku wengine (pengine) mmevaa nguo nyeusi kuashiria maombolezo kitaifa.

Leo ninatimiza miaka 11 toka nimekula kiapo cha kuishi (kama mume na mke) na huyu mdada.
Tulikutana 1994 na ndoa ikafungwa miaka 6 baadae
Ndani ya miaka hii 11 Mungu kanijalia kuwa baba wa boy-10 na girl-7 na ukiwaangalia ni dhahiri hakunichakachua labda awe amechakachua na mdogo wangu, hahaahahaaa!!!

Ni miaka ya kuishi na mwanamke ambaye alichukua nafasi ya mama na dada yangu katika maisha.

Miaka 11 imenifundisha nisimwamini kila mtu ninaposigana na mke wangu. Nakumbuka in our early years niliwahi kushare na mchungaji juu ya tofauti zangu na mke wangu only for the pastor to use my story in his preaching the next sunday. Siku hizi nayasovu mwenyewe tu, no outsiders!

Miaka 11 ya kutambua kwamba vitu vidogo sana (thanks, sorry, karibu, darling..) vinajenga uhusiano na vitu vidogo pia huwasha moto.

Jamani wakati mwenzenu nashereheka 11 years kuna experience zipi (nzuri/mbaya/vituko) umewahi pitia kwenye mahusiano yako.

Karibuni tuzungumze!!!!!!!!!!!!!!!!

Kiongozi pongezi sana kwa kutimiza miaka 11 ya ndoa na my wife wako.

Wakati mwingine tukikutana na watu mlio na uzoefu wa kiwango hicho inakuwa ni chachu kwetu.

Mimi ndo nakamata miaka mitatu sasa, naomba Mungu aniwezeshe na kunijaalia ili siku moja nifikie hapo ulipo, nadhani siku hiyo nitakukumbuka Realman.

Kwa kweli niwatakie maisha marefu zaidi ya yenye furaha zaidi.

Naomba leo umwagie maji mengi zaidi kwa niaba ya JF!!
 
Gaga!!!!!!
Thank you very much, maneno yako yamejaa ukweli 100%.
Nitaweka tahadhari dada yangu maana wanasema aliyesimama aangalie asianguke.

Na ni kweli pia sisi wanaume ni chanzo cha uimara ama kutetereka kwa ndoa nyingi. Hatuko on the receiving end na pengine ndio maana tunajisahau.

Unadhani kwa nini baadhi ya wanaume wanabadilika ktk kipindi hiki (10-20)??

Asante kwa kushea experience yako maana inatujenga wengine, tumeona kina Msindima ndo kwanza ana 8months.

Nafikiri wengi wakifikia miaka hiyo wanaleta mazoea kwemye ndoa wanaanza kupunguza care flaniflani hivi na mwanamke anakuwa bize sana na malezi ya watoto kuliko mumewe majukumu pia nayo yanaongezeka pia, sasa hapo usipoangalia vizuri mwanaume anaanza kuwa na company ya marafiki mbalimbali ambao wana tabia tofautitofauti hapo ndipo inapoanza kasheshe.
 
Asante sasa Sister!

Toka nimejoin JF ni kama kukutana na ndugu yako mlokuwa hamfahamiani.
Wifi atapata salaam maana siku hizi akiona nacheka huku nimeshika simu husema "Jamii Forums hao"!!!!!!!!

teh teh teh teh :clap2::clap2:
 
Back
Top Bottom