Salary Slip
Platinum Member
- Apr 3, 2012
- 49,325
- 152,136
Kifungu hiki kinataamka: "Mshahara na malipo mengine yote ya Raisi havitapunguzwa wakati Raisi anapokuwa bado ameshika madaraka yake kwa mujibu wa Katiba hii."
Hicho ni kifungu cha Katiba ya Jamuhuri ya Muungano wa Tanzania ya mwaka 1977 kinachoongelea Mashariti ya Kazi ya Raisi.
Kwa ufahamu wangu, Raisi anahesabika kuwa bado yupo madarakani mpaka pale mrithi wake (Raisi Mteule) atakapokuwa amekula kiapo cha kushika madaraka ya uraisi.
Hofu yangu hapa ni kuwa baada ya kuambiwa sasa Raisi atalipa kodi,jambo hili linaweza likasahaulika na mwisho wa siku tukaambiwa ilishindikana kukata kodi kiinua mgongo cha Raisi kwasababu katiba haikubadilishwa na wakati huo hata Bunge linaweza kuwa limeshavunjwa.
Kingine cha msingi hapa ni je sheria imetoa timeframe kwamba Raisi awe amelipwa kiinua mgongo chake wakati gani au iko kimya juu ya hili?
Nauliza hivi kwasababu Raisi ana privilege nyingi kiasi kwamba hata kiinua mgongo chake huenda hulipwa mapema kabisa kabla hata hajastaafu hivyo kunaweza kutokea contradiction kati ya sheria na katiba baada ya mabadiliko haya yanayoruhusu Raisi nae sasa kukatwa kodi ya kiinua mgongo.
Je,hili haliwezekani kutokea?
Kwanini uamuzi huu wa Bunge wa kukata kodi kiinua mgongo cha Raisi usiende sambamba na kubadili moja kwa moja kifungu hiki cha Katiba kwa kuongeza sharti jipa katika katiba hii juu ya Raisi sasa kukatwa hii kodi?