Itangazwe Rasmi Clouds Fm ni Radio ya Taifa

Itangazwe Rasmi Clouds Fm ni Radio ya Taifa

General Mangi

JF-Expert Member
Joined
Dec 21, 2013
Posts
15,316
Reaction score
23,178
Ni mara nyingi sana viongozi wa ngazi ya juu nchini kuitumia clouds fn na hata Tv kutolea matamko.
Kibaya zaidi viongozi hao huenda wenyewe kutoa matamko.

Mwanzoni nilifikiri Clouds huwafuata ofisini kuwahoji. Kiukweli sijawahi sikia Makonda kaenda tbc kuhojiwa au kutolea sintofahamu iliyojitokeza.

Tunashuhudia hata Rais akiipa Kick radio hii na kuzidi kupata umaarufu zaidi ya TBC. Tuliona Rais akipiga simu clouds kuwapongeza na kutolea ufafanuzi kuhusu mshahara wake.

Juzi Rais nae anasema anatamani angehudhuria Fiesta, tamasha ambalo linaongozwa na Clouds media.

Kifo cha TBC medi kinakaribiaa.
 
mm huwa najiuliza redio zingine zinajisiaje? wangekuwa wanafanya hayo tbc wala tusinge shangaa ila kupendelea radio moja binafsi huwa sielewi
 
Unataka Fiesta ipigwe marufukuuuuuuuuu!!!!!!!
 
Clouds ndo media inayosikilizwa zaid Tanzania....hata hvyo hyo siyo sababu ya kukimbilia pale viongozi wanakosea.... japo Mara nying clouds huwatafuta viongozi na Mara chache viongozi huenda wenyewe
 
Viongozi wetu hawana tabia ya kuthamini vya kwetu acha TBC ife tu,tupunguze zigo la mishahara ya bure wanayopewa wafanyakazi maana hakuna haja ya kuwa nayo wakati haitumiki kwa shughuli za kiserikali
 
Pamoja na majungu yote, ukweli clouds fm ni wabunifu na kufanya kuvutiwa na kusikilizwa na watu wengi. Kamaunataka kusikika mbali na kwa watu wengi utachagua kipazasauti kitakachowezesha hilo.
 
...Kiukweli sijawahi sikia Makonda kaenda tbc kuhojiwa au kutolea sintofahamu iliyojitokeza..

TBC wameimaliza kabisa baada ya kufuta Bunge live ila TBC haitakufa kwa kuwa wewe na mimi tupo kulipa kodi ili iendelee kuwepo.
 
Huu Uzi Ulitakiwa Kupata Mchango Wa Member Mmoja Ambaye Kwasasa Kawa Adimu Sana Anaitwa Kigogo
 
Kama wanawapa limbwata viongozi wetu wa juu, maana hata awamu iliyopita walikuwa wamewabamba kikwelikweli
 
Back
Top Bottom