Itakuwaje siku Muungano ukivunjika?

Itakuwaje siku Muungano ukivunjika?

Tunatakuwa tujifunze kwanza kati ya Ethiopia na Eritrea.

Ila ninacho kijua
ZRA itakuwa imezidi kuimarisha nguvu zake.

Chuo Cha ufundi kitabaki vile vile

Polisi kamishna wa Zanzibar atakuwa Inspector jenerali wa Zanzibar

Uhamiaji kamishna wao atakuwa Kamishna jenerali wa Zanzibar na mamlaka yake yatakuwa kamili

KVZ ndio litakuwa jeshi la nchi ya Zanzibar

Jku itachukuwa atam ya jkt kule Visiwani

Volunteer ndio itakuwa mgambo kule kwao

Kmkm ndio Navy Yao kule Zanzibar

Tutaanza ugomvi wa mpaka kama Malawi kwenye maji
 
Salaam wakuu,

Najaribu kuwaza itakuwaje siku muungano wa Tanganyika na Zanzibar ukivunjika,

Je Tanzania nayo itakufa, maana ni zao la muungano huo.

Katika mambo haya ambayo tunashirikiana chini ya muungano, ni ipi hatma yake.

-Ulinzi na usalama wa taifa
-Mambo ya nje (diplomasia)
-Uraia
-Sarafu na benki kuu
-Usajili wa vyama vya siasa
-Elimu ya juu
-Uhamiaji
-Posta na mawasiliano
-Kodi ya mapato ya kitaifa
-Leseni za viwanda vya kimataifa
-Huduma za anga
-Mambo ya mafuta na gesi


Pamoja na kwamba Zanzibar itakuwa ni taifa huru, je imejipangaje kiuchumi pale utakapoyumba kutokana na kutegemea zaidi misaada au rasilimali kutoka Tanganyika?

Vipi kuhusu utaifa?

Naomba kufahamishwa katika hayo kwanza japo ya kuuliza ni mengi.
Itakuwa heri na nafuu kwa Tanganyika na shari kwa Visiwani kwa sababu kutakuwa na mataifa m awili ya Pemba na Unguja baina ya mabaki ya waarabu na yale ya watumwa. Pia, watakulana kwa sababu ardhi haitatosha. Watanganyika watatua zigo la kubeba watu wasio na faida kwao.
 
Itakuwa heri na nafuu kwa Tanganyika na shari kwa Visiwani kwa sababu kutakuwa na mataifa m awili ya Pemba na Unguja baina ya mabaki ya waarabu na yale ya watumwa. Pia, watakulana kwa sababu ardhi haitatosha. Watanganyika watatua zigo la kubeba watu wasio na faida kwao.
NIliwahi kusikia mahali kwamba kwa kule zanzibar
Wanabaguana wao kwa wao, pemba na unguja.

Lina ukweli hili???
 
Back
Top Bottom