Elections 2010 Itakuwaje Dr Slaa asipochaguliwa kuwa rais?

Sidhani kama maandalizi ni kikwazo, navyojua mimi ni kuwa Tanzania ya sasa si ya zamani, sasa hivi kuna technologia ya kueneza ujumbe kwa kutumia media mbalimbali kwa haraka sana kuwafikia wananchi hata wa vijijini.

Mpaka 30 oct ifike naamini wananchi wengi watakuwa wamepata ufahamu mzuri kuhusu Dr Slaa na sera zake.

Mzee unaishi dunia gani? hakuna lifanyikalo kiusahihi bila maandalizi ya kutosha,,usikurupuke tu kutoa maoni,,na usitumie imani kwenye siasa,,bali matendo,,,sijaona 'Active Campaigning' kwenye social media zaidi ya hapa JF,,,wahandishi uchwara wote wamenunuliwa,,so weka bayana ni media gani hizo zitatumika?,,nguvu kubwa ilibidi iwekwe kwenye 'Social Media' kwani humo ni vigumu kwa CCM kueneza propaganda zake,,Zitto aliliona hilo ndo maana akafungua blogu yake,,i guess Last month...viongozi wote na chadema kwa ujumla walipaswa kuiga mfano ule na kueneza ushawishi kwe nye,,Facebook,Twitter,Blogs,,Youtube na social media nyingine,,,watanzania vijana haipiti siku hawajaenda humo..
 
Itakuwa kawaida tu kama siku zote.kwani Mrema aliposhindwa 1995 ilikuwaje?Si watu waliendelea na maisha yao.Sanasana wakitokea wahuni na vurugu zao jeshi la polisi litawashughulikia kama kibaka na wananchi wenye hasira.Niliwahi kutuma thread huko nyuma kuulizia mitandao ya chadema iko vipi vijijini lakini naona ilionekana sio muhimu ila kwangu bado ninasisitiza kuwa upinzani kushinda kwa haya ya kwenye mitandao na majukwaani bado ni ndoto maana jamii kubwa ya wa TZ bado hawajaelimika vya kutosha.Ushauri kwa Dk Slaa akishindwa asigombee uspika wala nafasi yeyote bali abaki kuimarisha chama kwa siku za mbele na kwa faida ya miaka ijayo lakini kwa sasa hivi kama ataingia kwenye kinyanganyiro chochote kitakachowahusu wabunge watamuangusha ili kumuua kisiasa.Ila kama atateuliwa na JK kuwa mbunge achukue nafasi hiyo kuendeleza mapambano
 
Kumbe sio lazima kuwa Sheik Yahaya kuwa mtabiri? Hapa naona utabiri... Mbona atakayekuwa Rais anafahamika? Hapa issue ni chama gani kitapa wabunge wengi?
 
Itakuwaje Dr Slaa asipochaguliwa kuwa rais? Agombee uspika? ili kuendelea kutetea wanyonge bungeni? Aelekeze nguvu kwenye chama ili ifikikapo 2015 Chadema kiwe imara zaidi?
Najiuliza tu nini hatima ya 'bwana silaha' kwani nadhani waTZ tunamuhitaji huyu bwana kuendelea kuleta chachu ya maendeleo.


Kumbuka kuwa Dr. Slaa ndiye Katibu Mkuu wa Chedema, hivyo bado ana nafasi ya kutumikia wananchi kwa njia moja au nyingine.
 
Post by Kasheshe
"Kumbe sio lazima kuwa Sheik Yahaya kuwa mtabiri? Hapa naona utabiri... Mbona atakayekuwa Rais anafahamika? Hapa issue ni chama gani kitapa wabunge wengi?"

Unaongea kama Masha kwenye suala la uraia wa Bashe. Unaweza kufafanua kidogo hapo kwenye nyekundu?
 
intrested observer umenikuna na observation zako na inaonyesha ni mchambuzi mzuri. Hebu nifafanulie nafasi ya kushinda kwa kura nyingi hata kama ushahidi kutoka vituoni unaonyesha hivyo na "kutangazwa na tume ya uchaguzi kuwa mgombea fulani kashinda katika mazingira ya tanzania"
 
babuyao bado watu wa vijijini kwa maana ya wakulima hamjaamka vya kutosha, kama walivyoamka wenzenu wafanyakazi.

Wafanyakzi 350,000 tu wameweza kuitingisha serikali ya
ccm na ccm yenyewe kiasi cha kutoa fedha za nyongeza ya mishahara aliyoapa jk kutotoa.

Wakulima kwa mamilioni katika kila mkoa mnangoja nini kutumia wingi wenu kudai mambo yeney maslahi kwenu kama vile kuishinikza serikali kuongeza kodi kwa bidhaa zitokanazo na mazao ya kilimo kama vile mafuta ya kula kutoka nje, juisi za aina mbali mbali kutoka nje, nguo kutoka nje n.k kwa nia ya kuhakikisha kuwa soko la ndani la mazao ya kilimo linakua na kuwahakikishia wakulima bei nzuri?

Hebu tazama wakulima wa mahindi wanavyotabika na mahindi yao hata katika kipindi hiki cha kampeni 2010 kwa sababu tu ccm na serikali yake haitaki kuwaruhusu wauze mahindi yao popote ilihali serikali imeshindwa kununua mahindi hayo?

Katika mazingira hayo mkulima lazima atabaki kuwa maskini tu. Ndio maana wapenda mabadiliko tunaona wenzetu bado mmelala sana, wakati wa kumaka umefika sasa!!!!!!
 
Itasababisha yaliyotokea kenya baada ya uchaguzi yatokee na huku Tanzania,halafu tutasuluhishwa na kuunda serikali pamoja na baadae tutabadili katiba kama tanzania visiwani.

Acheni kuwatisha wa watanzania eti yatatokea yaliyotokea Kenya, kama ni lazima ashinde kuna sababu gani kupiga kampeni, si angekaa tu nyumbani asubiri kuchaguliwa kwa bahati nzuri uliokusudia kuwatisha ndo kwanza hata Jf hawaijui. Sasa cha muhimu ni kuheshimu matokeo. Sasa hapo kenya kuna kitu gani kipya huyo raila waliomtaka sivyo walivyofikiri ingekuwa. JF ndo wakwanza kupinga mambo yakitabiri halafu kwa mlango wa nyuma mnayaabudu, au kwa kuwa umesema si dr slaa si utabiri? Kweli hatudanganyiki.
 
Nakubaliana kabisa na wewe ndugu matambo, nimeshaanza kuingiwa na wasiwasi wa 'kimaandalizi' wa ndugu slaa na Chadema kwa ujumla..isitoshe Afrika baada ya ukoloni hakuna rais aliyewahi kuondolewa baada ya muhula 1 tu wa uongozi.

Tutakuwa wa kwanza kutengeneza historia hiyo,,,lakini kwa maandalizi haya, nina mashaka tutafanikisha hilo.

What about Ghana 2008?..YES WE CAN
 
Mzee unaishi dunia gani? hakuna lifanyikalo kiusahihi bila maandalizi ya kutosha,,usikurupuke tu kutoa maoni,,na usitumie imani kwenye siasa,,bali matendo,,,sijaona 'Active Campaigning' kwenye social media zaidi ya hapa JF,,,wahandishi uchwara wote wamenunuliwa,,so weka bayana ni media gani hizo zitatumika?,,nguvu kubwa ilibidi iwekwe kwenye 'Social Media' kwani humo ni vigumu kwa CCM kueneza propaganda zake,,Zitto aliliona hilo ndo maana akafungua blogu yake,,i guess Last month...viongozi wote na chadema kwa ujumla walipaswa kuiga mfano ule na kueneza ushawishi kwe nye,,Facebook,Twitter,Blogs,,Youtube na social media nyingine,,,watanzania vijana haipiti siku hawajaenda humo..

Wewe ndio uko kwenye dunia ya kusadikika! Asilimia ngapi ya Watanzania vijana wapigakura for that matter wenye uwezo wa kuingia kwenye facebook, twitters na blogs etc etc? Kwa taarifa yako wengi walio kwenye zana hizo za internet ni wale walio nje ya nchi ambao hata si wapigakura bali ni mashabiki tu. Mtanzania kijana anayefukuzana na ubangaizaji akitafuta maisha bora ambayo hayaoni ana muda gani wa mambo hayo? Lakini inapofika kwenye mikutano ya hadhara inayofanywa na wagombea hivi sasa hiyo ndiyo determining factor ya nani anaweza kuibuka mshindi na wala si useless blogs za akina Zitto za kujitafutia umaarufu wa kwenye internet!
 
you are not living in the past, you are living in present, try to forget historical background

Akishindwa Urais mfanye Mzee(Prof) Baregu kuwa Mshenga wake akahalalishe kimada chake kwa kupeleka Posa kwa wazazi wake japojuwa amepora tutamsihi Mwenye Mke ASAMEHE kama alivyosamehe mzazi mwenzie Slaa aliezaa nae watoto wawili akamtembezea kibuti.
 
Back
Top Bottom