Itakuwaje Dr Slaa asipochaguliwa kuwa rais? | JamiiForums | The Home of Great Thinkers

Dismiss Notice
You are browsing this site as a guest. It takes 2 minutes to CREATE AN ACCOUNT and less than 1 minute to LOGIN

Itakuwaje Dr Slaa asipochaguliwa kuwa rais?

Discussion in 'Uchaguzi Tanzania' started by Simple, Sep 12, 2010.

 1. Simple

  Simple JF-Expert Member

  #1
  Sep 12, 2010
  Joined: Feb 6, 2009
  Messages: 249
  Likes Received: 7
  Trophy Points: 35
  Itakuwaje Dr Slaa asipochaguliwa kuwa rais? Agombee uspika? ili kuendelea kutetea wanyonge bungeni? Aelekeze nguvu kwenye chama ili ifikikapo 2015 Chadema kiwe imara zaidi?
  Najiuliza tu nini hatima ya 'bwana silaha' kwani nadhani waTZ tunamuhitaji huyu bwana kuendelea kuleta chachu ya maendeleo.
   
 2. Ng'wanangwa

  Ng'wanangwa JF-Expert Member

  #2
  Sep 12, 2010
  Joined: Aug 28, 2010
  Messages: 10,175
  Likes Received: 892
  Trophy Points: 280

  Itakuwa ni kipimo kingine cha udhaifu wa Watanzania katika kufikiri na kuamua
   
 3. JOYCE PAUL

  JOYCE PAUL JF-Expert Member

  #3
  Sep 12, 2010
  Joined: Jan 8, 2010
  Messages: 1,007
  Likes Received: 6
  Trophy Points: 135
  Itasababisha yaliyotokea kenya baada ya uchaguzi yatokee na huku Tanzania,halafu tutasuluhishwa na kuunda serikali pamoja na baadae tutabadili katiba kama tanzania visiwani.
   
 4. P

  Paul S.S Verified User

  #4
  Sep 12, 2010
  Joined: Aug 27, 2009
  Messages: 5,933
  Likes Received: 276
  Trophy Points: 180
  Atarudi makao makuu ya chadema na kuendelea na kazi yake ya ukatibu mkuu wa chadema, pia kukipanga chama vizuri zaidi kwa chaguzi zijazo
   
 5. m

  matambo JF-Expert Member

  #5
  Sep 12, 2010
  Joined: May 14, 2009
  Messages: 728
  Likes Received: 9
  Trophy Points: 0
  binafsi, siamini kama Dr Slaa atashinda mwaka huu,maana Chadema hawakuwa wamejiandaa au kumwandaa slaa kimkakati agombee urais, na kama maelezo yanayotolewa kuwa alilazimishwa ni sahihi basi timing ya yeye kuingia kwenye kinyang'anyiro ilikuwa somehow too late. hili linatokana na kuwa asilimia kubwa ya watanzania wanakaa vijijini,bado hawana ufahamu wa kutosha na pia hawamjui kiundani slaa, achana na wale walio kwenye miji midogo yenye maingiliano ya kibiashara na kuwa na makabila mchanganyiko, huko upinzani una nguvu.

  lakini binafsi naamini bado uamuzi wa dr slaa kugombea mwaka huu ulikuwa sahihi maana anajitangaza zaidi ili come 2015 awe anafahamika zaidi,pia iwapo atashindwa urais na kubakia kuwa kiongozi wa chama,naamini atajitahidi kujenga chama kiwe na nguvu zaidi kwenye grassroot kuliko juu tu,naamini atajitahidi kuelimisha watanzania kupitia operesheni mbalimbali. kwenye operesheni zilizopita mbowe alikuwa ndio akiziongoza lakini hajagombea urais so naamini iwapo operesheni zijazo akiziongoza slaa kisha yeye mwenyewe akigombea 2015 ukijumlisha kuwa mwaka 2015 sidhani kama CCM watakuwa na kiongozi madhubuti anayechagulika kuwa rais ,basi ushindi unaweza kuwa wa upinzani
   
 6. Simple

  Simple JF-Expert Member

  #6
  Sep 12, 2010
  Joined: Feb 6, 2009
  Messages: 249
  Likes Received: 7
  Trophy Points: 35
  Sijaelewa kabisa uliyoyaandika,,tafadhali fafanua zaidi, 'TUTASULUHISHWA' kwani tutagombana?
   
 7. PatPending

  PatPending JF-Expert Member

  #7
  Sep 12, 2010
  Joined: Aug 17, 2007
  Messages: 490
  Likes Received: 2
  Trophy Points: 33
  This place will implode. Maana baadhi yetu wamekuwa na unrealistic expectations kuhusiana na hiki kinyang'anyiro. All the same though, maana Roma haikujengwa ndani ya siku moja na mapambano yataendelea tu.
   
 8. Simple

  Simple JF-Expert Member

  #8
  Sep 12, 2010
  Joined: Feb 6, 2009
  Messages: 249
  Likes Received: 7
  Trophy Points: 35
  Nakubaliana kabisa na wewe ndugu matambo, nimeshaanza kuingiwa na wasiwasi wa 'kimaandalizi' wa ndugu slaa na Chadema kwa ujumla..isitoshe Afrika baada ya ukoloni hakuna rais aliyewahi kuondolewa baada ya muhula 1 tu wa uongozi.

  Tutakuwa wa kwanza kutengeneza historia hiyo,,,lakini kwa maandalizi haya, nina mashaka tutafanikisha hilo.
   
 9. sblandes

  sblandes JF-Expert Member

  #9
  Sep 12, 2010
  Joined: Apr 25, 2010
  Messages: 2,450
  Likes Received: 782
  Trophy Points: 280
  Ni mapema mno kutabiri matokeo ya uchaguzi mkuu,lakini ikiwa ameshindwa nisingemshauri kugombea Uspika kwani Wabunge wa CCM watapiga kura ya pamoja,hawawezi kutaka Dr Slaaa, ameisumbua mno serikali ya chama chao bungeni.Vile vile Samuel Sitta atagombea Uspika ameishatangaza nia ya kuwania kiti hicho.Lakini Raisi Kikwete kupoza wapinzani anaweza akamteua kuwa mbunge wa kuchaguliwa na hata kuwa mshauri wake.
   
 10. C

  Chamkoroma Senior Member

  #10
  Sep 12, 2010
  Joined: Sep 6, 2010
  Messages: 187
  Likes Received: 0
  Trophy Points: 0
  'Nayaweza yote katika yeye anitiae nguvu,' 'kila muombalo aminini mmesha pata,' naamini kabisa kuwa mwaka huu ni wetu na Drm wa kweli mwana wa mageuzi ya kweli, na slaha ya kweli ni watu lkn kiongozi mkuu wa slaha hiyo ni Mungu alie hai anaeona mateso ya TZ wanaokandamizwa na akina manyuzi ya katani wakidhani hakuna tena, let our beloved Gog decide on this matter,He made the weak man to rule why not Dr. for the poeple of TZ?
   
 11. Butola

  Butola JF-Expert Member

  #11
  Sep 12, 2010
  Joined: Jan 19, 2010
  Messages: 2,221
  Likes Received: 90
  Trophy Points: 145
  It's either now or never.

  Watanzania wanafuata matukio tu, kwa kuwa nje ya Bunge kwa miaka 5 ukiongeza na umri wake, umaarufu wa Dr. Slaa utashuka na hatakuwa na nafasi ya kuleta upinzani wa maana mwaka 2015.

  Wanaoukumbuka umaarufu wa Mbowe katika uchaguzi wa 2005 wataelewa ninachosema.
   
 12. Butola

  Butola JF-Expert Member

  #12
  Sep 12, 2010
  Joined: Jan 19, 2010
  Messages: 2,221
  Likes Received: 90
  Trophy Points: 145
  Hilo kwa Dr. Slaa sahau, ataweza kufanya hivyo kwa CUF na kwa Mzee wa Kiraracha.
   
 13. I

  Interested Observer JF-Expert Member

  #13
  Sep 12, 2010
  Joined: Mar 27, 2006
  Messages: 1,400
  Likes Received: 432
  Trophy Points: 180
  Acha kutokujiamini,
  Mkapa alijiandaa vipi?? Aliiingizwa tu na Mwalimu Nyerere? Mwinyi aliajiandaa vipi? JK je? Tatizo la WaTanzania ndiyo hilo; all the time hawajiamini. Factors zipo very open:
  1. Pamoja na Mkapa kusaidiwa kwenye kampeni na Nyerere lakini Mrema alifikisha karibu Kura 40%. Na unajua factor ya Mwalimu na impact yake.
  2. WAtu wa Vijijini; vijiji vya wapi? Sasa hivi siasa zipo kanisani, misikitini kote huko watu wanajadili haya, ndugu zao nao wapo kwenye mitandao; simu za mikono ndiyo hizo; sms hadi Tunduru.
  3. Kikwete kaboronga mno; na sasa waTanzania wengi washakuwa hawana sympathy, nae, hata aanguke mara kumi;
  CCM wana-chance moja tu; kubuni kuiba kura October 31st.
  4. Vyama vyenye nguvu vipo vitatu sasa hivi, CCM, Chadema, na CUF. CCM na CUF ina wanachama ambao wanaitwa 'base"; yaani wale wa kudumu. Chadema base ni ndogo sana lakini wanategemea zaidi independent kama sisi. Base ya Chadema ni wasomi, Liberals na independent kwa mwaka huu.
  Conservatives wengi wako CUF na CCM; lakini wale wenye rogho nyepesi wengi washaingia CHADEMA nao ndiyo Chadema atawavuna.

  Kama uchaguzi utafuata haki, CCM, CHADEMA na CUF kunawezekana kabisa kisitokee chama kitakachofikisha 51% ya kuwa na Rais.

  Therefore Dr. Slaa ana nafasi kubwa sana hasa kuchukua wanachama wengi wa CCM kupigia kura yeye.
   
 14. Plato

  Plato JF-Expert Member

  #14
  Sep 12, 2010
  Joined: Aug 28, 2010
  Messages: 421
  Likes Received: 5
  Trophy Points: 33
  Kwani kilitokea mbowe aliposhindwa urais,aliendelea na majukumu ya kukijenga chama.na hatua kiliyofikia chadema.hata hivyo hakuna uwezekano wa slaa kushindwa.amesema sahihi aliyesema kama kenya.kwani dr.atashinda na kivuitu wetu atatangaza na jaji mkuu wetu atafanya vya kwake.so mauaji yatazuka.
   
 15. k

  kamalaika Senior Member

  #15
  Sep 12, 2010
  Joined: Mar 16, 2007
  Messages: 187
  Likes Received: 4
  Trophy Points: 35
  Sikuelewi unachosema. Umaarufu wa Dr Slaa ulianzia bungeni ambapo wengi walianza kum notice na kuona kuwa huyu ni mtetezi wa wanyonge. Ndio maana ya huu umaarufu wake. Mbowe umaarufu wake ni wa majukwani kuhamasisha watu na usisahau wakati wake watu wengi walienda kuangalia helikopta.
   
 16. Butola

  Butola JF-Expert Member

  #16
  Sep 12, 2010
  Joined: Jan 19, 2010
  Messages: 2,221
  Likes Received: 90
  Trophy Points: 145
  Nadhani umesahau kuwa Mbowe alikuwa ni mbunge makini na mwenye ushawishi zaidi wa Chadema katika bunge la 2000-2005.

  Na umesahau pia kuwa at Dr. Slaa anatumia helikopter.
   
 17. B

  Babuyao JF-Expert Member

  #17
  Sep 12, 2010
  Joined: Jun 6, 2009
  Messages: 1,734
  Likes Received: 29
  Trophy Points: 145
  Mijitu mingine bwana! Hivi sisi watu wa vijijini tuna nini? Mbona mnatuandama sana kwamba tu wajinga, hatujui kitu? Hiyo kauli mimi inaniudhi sana. Jamani tupeni heshima yetu. Sisi wa vijijini tumeamuka sana kuliko mnavyofikiri. Pengine wengi hawana kompyuta na internet lakini kisiasa tuko macho. Tunajua kinachoendelea; tunajua nani tumpe kura na nani tumnyime: kwa uafahamu kabisa. Hii lugha ya kutudhalilisha wa vijijini ikome.
   
 18. Mwita Maranya

  Mwita Maranya JF-Expert Member

  #18
  Sep 12, 2010
  Joined: Jul 1, 2008
  Messages: 10,569
  Likes Received: 104
  Trophy Points: 145
  Hapa hakuna swala la kutochaguliwa kwa Dr. Slaa, ukweli uko dhahiri kabisa kwamba Dr. Slaa anakubalika kwa watanzania wengi na wako tayari kumchagua kuiogoza nchi hii. Jambo tunalopaswa kujiuliza hapa, itakuwaje "Kivuitu wetu" (Jaji Makame) asipomtangaza Dr. Slaa kuwa Rais?
   
 19. h

  hagonga Senior Member

  #19
  Sep 12, 2010
  Joined: Sep 11, 2010
  Messages: 141
  Likes Received: 1
  Trophy Points: 0
  Sidhani kama maandalizi ni kikwazo, navyojua mimi ni kuwa Tanzania ya sasa si ya zamani, sasa hivi kuna technologia ya kueneza ujumbe kwa kutumia media mbalimbali kwa haraka sana kuwafikia wananchi hata wa vijijini.

  Mpaka 30 oct ifike naamini wananchi wengi watakuwa wamepata ufahamu mzuri kuhusu Dr Slaa na sera zake.
   
 20. Anyisile Obheli

  Anyisile Obheli JF-Expert Member

  #20
  Sep 12, 2010
  Joined: Dec 13, 2009
  Messages: 3,304
  Likes Received: 19
  Trophy Points: 135
  you are not living in the past, you are living in present, try to forget historical background
   
Loading...